Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 18 July 2024

BENKI YA EXIM YATOA VITANDA VYA WAJAWAZITO MKOANI MOROGORO

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro - Mhe. Judith Nguli (wa pili kushoto), ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akikagua moja ya vitanda vya wodi ya wazazi vilivyokabidhiwa na Exim Bank Tanzania kwa Mkoa wa Morogoro. Wengine ni Dkt. Best Magoma (kushoto) -  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stanley Kafu (wa pili kulia) - Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo na Ibrahim Ukwaju - Meneja wa Tawi la benki hiyo Morogoro. Vitanda hivyo ni sehemu ya kupunguza tatizo la uhaba wa vitanda vya kujifungulia wajawazito katika Mkoa wa Morogoro na tukio hilo limefanyika tarehe 18 Julai katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania - Stanley Kafu akikabidhi vitanda vya kujifungulia wajawazito kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro - Mhe. Judith Nguli ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambapo vitanda hivyo vinaenda kupunguza changamoto za vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua ikiwa ni sehemu ya malengo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kusaidia jamii na kuboresha huduma za afya nchini, Exim Bank Tanzania imetoa vitanda vya hospitali kwa wodi za wazazi katika Mkoa wa Morogoro. Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya mapambano ya kupunguza vifo vya wamama na watoto wakati wa kujifungua.


Benki ya Exim Tanzania imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii katika sekta za mazingira, elimu, uchumi, utalii, michezo, na afya. Kwa mjibu wa taarifa za wizara ya afya, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya kina mama na watoto kutoka 556 mwaka 2016 mpaka kufukia vifo 104 mnamo mwaka 2023 ingawa bado hali sio salama sana.

Kwa kutambua changamoto hii pamoja na zingine zikiwemo uhaba wa vifaa vya matibabu, upungufu wa vitanda, madawa, na uchache wa watoa huduma za afya, benki ya E xim inaona ina nafasi kama taasisi kusaidia Serikali kupunguza tatizo la vitanda vya wajawazito.

No comments:

Post a Comment