Dar es Salaam - Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imetangaza kupunguza gharama za tozo za miamala ikiwa ni kuitikia wito wa maelekezo ya yaliyotolewa hivi karibuni na serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango kwa watoa huduma kupunguza tozo za miamala ya simu ili kuwezesha wateja kufaidika na huduma hiyo kwa punguzo la hadi asilimia 50%.
Serekali ilitoa maelekezo hayo kwa watoa huduma kufanya marekebisho ya punguzo la Tozo ya serikali zinatozwa kwa wateja wa huduma za fedha kwa njia ya simu (Mobile Money) kwa lengo la kuendelea kurahisisha huduma hiyo ili kufikia malengo ya kukuza na kupanua huduma hiyo kila mahali,
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda amesema Airtel Money inaendelea kuwa huduma nafuu na salama zaidi kwani tayari Tumeshapunguza tozo hiyo kwa asilimia 50, tunaishukuru serikali kwa usikivu wake kwa wananchi kwa punguzo hili la TOZO ili kutoa unafuu zaidi.
“Vilevile Airtel Money tunawahakikishia wateja wetu wote kwamba tunaendelea na Ofa yetu ya kuwalipia TOZO wateja ikiwa ni kuunga mkono dhamira hii ya serikali kuitikia wananchi na kutoa punguzo la Tozo la asilimia 50 kwenye miamala ya fedha kwa mtandao, “Ukitumia Airtel Money sasa Kutuma Pesa au kutoa pesa kwa Airtel Money hadi 29,999 utatuma au kutoa pesa Bila TOZO, pia kwa wale wateja wanaotumia Aplikesheni ya Airtel wataweza kutuma au kutoa hadi Tsh 5,000,000 Bila TOZO yoyote kabisa, Airtel italipa TOZO yote kwa serekali kwa niaba ya mteja wa Airtel Money”.
Nchunda aliongeza kuwa “Airtel Money tunasonga mbele na dhamira yetu ya kuwahudumia wateja wetu wote kwa gharama nafuu na kuwafikia pia wateja ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa kusogeza huduma za Airtel Money Branch kila kona ya Tanzania, sasa tunajivunia kuwa na zaidi ya Airtel Money Branch 3000 nchi nzima”.
“Tumafanya maboresho ya upatikanaji wa huduma kwa kiasi kikubwa ili kuleta mapinduzi kabambe kwenye sekta ya fedha kwa kutoa huduma ya Airtel Money kwa lengo kuleta wepesi kwa wateja na kuchochea Uchumu Jumuishi” alisema Nchunda
Ni Imani yetu kuwa Muendelezo wetu wa BILA TOZO utawafanya watanzania wengi Zaidi waweze kutumia huduma zetu za Airtel Money kwa kuokoa kiasi walichotakiwa kulipia Tozo kwa kufanyia malipo mengine na kupunguza changamoto mbalimbali.
Airtel Money imekuwa ni huduma ya fedha kwa njia ya mtandao inayojipambanua kwa upekee kwa kutanuka Zaidi kwa kuwa na wakala zaid ya 160,000 waliosambaa nchni kote wakihudmia wateja masaa 24 siku 7 za wiki kam njia mojawapo ya ajira.
No comments:
Post a Comment