Baadhi ya Wakurugenzi wa NHC wakifuatilia Mkutano huo. |
Wadau wa Sekta ya Ardhi wakifuatilia mkutano huo. |
Waziri Mabula ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa Sekta ya Milki Tanzania ulioandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadau mbalimbali wa uendelezaji milki wakiwemo Shirika la Nyumba la Taifa na kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kisenga uliopo Millenium Towers, Kijitonyama Dar es Salaam.
Waziri Mabula amesema kuwa Wizara imeshawabaini wahusika wa kampuni hizo na kwamba wameanza kuzichukulia hatua mbalimbali na kuzitaka zile kampuni zinazotaka kujaribu kufanya mambo kama hayo kuacha mara moja kwani ni kinyume cha sheria na haivumiliki kuwatendea wananchi mambo hayo.
“Kama mmeshaanza kuibia watu basi muishie hapo msiendelee, tunahitaji kila mtu awe na makazi yaliyopangwa na yenye huduma zote muhimu suala la kupia viwanja vya mita za mraba 300 na kuwacha wananchi bila huduma muhimu halifai,”alisema.
Alisema Serikali haitaki kuwaibia wananchi kwa tamaa za haraka haraka, za watu wa chache na kwamba Serikali inahitaji uzingatiaji wa taaluma ili kusudi watu wapate huduma za kijamii ambazo zinafaa.
Mpima yeyote atakayepitisha upimaji wa ina hiyo hataruhusiwa, katibu mkuu hawa wapima wa namna hiyo kama wataendeleza hilo basi sisi na weo tutapambana.
Akizungumzia utengwaji wa maeneo Waziri Mabula amesema, kuna maeneo mengi nchini ambayo miji inaendelea kwa kasi hivyo halmashauri kupitia Wakurugenzi wake zinapaswa kuhakikisha zinatenga maeneo ya uwekezaji kwa lengo la kumuwezesha Mwekezaji atakapopatikana asipate tabu.
‘’Ni vizuri katika kipindi hiki ambacho baadhi ya miji inakuwa kwa kasi halmashauri zikatenga maeneo ya uwekezaji na kuyahaulisha kwa lengo la kuwarahisishia wawekezaji watakapokuja kuwekeza katika halmashauri husika,’’ alisema Mabula.
Aidha, Waziri Mabula amezitaka pia halmashauri kuhakikisha zinapanga miji maeneo yaliyopo pembezoni kwa kuanishwa matumizi yake kama vile kilimo, ufugaji na maeneo ya kuchezea kwa kutumia watendaji wa ngazi za chini badala ya kusubiri wataalamu wa mipango miji.
Alisema, upangaji miji mapema kwa kutumia watendaji wa ngazi za chini utasaidia wataalamu wa mipango mijini watakapokuja baadaye kutopata shida katika kupanga maeneo hayo hasa katika ile miji inayokuwa kwa kasi kwa kuwa miji hiyo itakauwa imepangwa na kuainisha matumizi mbalimbali.
‘’Hawa watendaji wa chini wakipewa elimu wataweza kuipanga miji yao kama ilivyokuwa wakati wa vijiji vya ujamaa maana sasa hivi mtu anaweza kujenga kiwanda katikati ya makazi ya watu’’ alisema Mabula.
Waziri amesema kuwa kuna uhaba mkubwa wa nyumba bora na za gharama nafuu hivyo ni wakati sasa Serikali na wadau wakatoa mao kuweza kupata muafaka wenye kuwezesha kupata nyumba bora.
Amesema pamoja na jitihada zote za taasisi za ujenzi wa nyumba nane za Serikali zimeweza kujenga nyumba 13,837 tu ndani ya miaka 12 kwa wastani wa ongezeko la nyumba 1,153 kwa mwaka , wakati mahitaji yaliyopo ni zaidi ya nyumba 200,000 kwa mwaka.
Amewataka wawekezaji wa uendelezaji miliki kuweza kujikita katika maeneo ya vijijni ili kuweza kuwa na makazi bora, kwani isipofanyika sasa basi kutakuwa na makazi holela yanayokuwa kwa kasi katika maendeo hayo.
Akizungumzia riba kwenye mikopo ya nyumba amesema imekuwa kubwa kati ya asilimia 13 mpaka 19 na hivyo kuzorotesha upatikanaji wa mikopo hiyo hivyo kutoa wito kwa Benki kuu kupitia mabenki na taasisi za fedha zikaona namna ya kupunguza riba ili kuboresha sekta ya makazi nchini.
“Wote ni mashahidi kwamba miji yetu sasa imeharibika imechafuka imejengwa hovyo, ni wakati sasa tukakimbizana na mazoezi ya urasimishaji kwenye mamlaka ya urasimishaji pamoja na kupanga miji ili kusudi kuwza kuipanga miji yetu ,”alisema.
Amesema kwamba ana imani kuwa kwa kushirikiana kwa pamoja na kuendeleza sekta ya miliki ikatilia mkazo Mabadiliko ya tabia nchi husababisha athari kwenye ardhi m hivyo akahimiza taasisi zikajenga nyumba zinazozingatia dhana ya ujenzi wa kijani yaani green building kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Mkutano huo wa Wadau wa Sekta ya Milki nchini unafanyika kwa siku mbili ukiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali zinazojihusisha na Ujenzi wa Nyumba, Taasisi za fedha na mabenki, watafiti wa ujenzi, madalali, waendelezaji miliki binafsi na wadau wengine una malengo ya kufahamu changamoto za sekta husika na kuzipangia mikakati. Kaulimbiu ya Mkutano huo ni Ukuaji wa Sekta ya Milki kwa maendeleo enelevu ya jamii na uchumi.
No comments:
Post a Comment