Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 29 June 2022

TIGO TANZANIA YAPATA MAGARI KUTOKA ISUZU TANZANIA


Tarehe 28 Juni 2022 - Specialized Rentals Limited (SRL) ni mtoa huduma bora anayechipukia katika nafasi ya ukodishaji wa uendeshaji wa vifaa vya moto nchini Tanzania, ikitoa magari bora zaidi na yenye kiwango tofauti cha magari yaliyozoeleka kwa mteja na vifaa hivi vya moto vina matumizi ya muda mfupi hadi muda mrefu na yanaendana na kasi kubwa zaidi inayomfaa na kumpa urahisi mtumiaji.

Hivi karibuni Specialized Rentals Limited imepewa Oda ya Ugavi wa Pickups 45 Mpya kabisa za ISUZU D-MAX kwa kampuni ya TIGO Tanzania (MIC TPLC), ambayo imeendeleza falsafa yake ya kutoa huduma bora kwa mteja.


Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kwenye Ukumbi wa Maonyesho ya Al Mansour, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Specialized Rentals Limited, Bw. Mihir Patwardhan alisema “Tunajisikia furaha kubwa kuchaguliwa na Tigo Tanzania kwa utaratibu huu adhimu. Shukrani zetu za dhati kwa Bw. Anurup Chatterjee na timu yake kwa kuweka imani tena katika huduma zetu bora tunazozitoa. Tuna uhakika wa kutumia uzoefu wetu tulionao ili kuhakikisha ufanisi unapatikana na unakuza biashara zetu na shughuli zetu zinazofanyika kwenye makampuni yetu zikidhi matakwa ya wateja wetu".


Bw. Patwardhan aliendelea na kuongeza, “Tunaishukuru Serikali ya Tanzania, kwa kuweka mkazo katika kujenga miundombinu ya barabara zenye viwango vya kimataifa nchini kote, hivyo kuwezesha na kuvutia uwekezaji nchini na miundombinu hii bora imekuwa kichocheo kinachohitajika kwa wawekezaji wa ndani na wa nje ya Nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Bw. Innocent Rwetabura alisema “Ushirikiano wetu wa kimkakati na Specialized Rentals Limited ambao wanaungwa mkono ipasavyo na kampuni maarufu ya Al Mansour (Isuzu) Tanzania unaonyesha dhamira yetu ya kuipa kampuni yetu ya Tigo Tanzania inayotoa huduma zake Tanzania nzima magari yenye uhakika na ufanisi zaidi ili kukuza jitihada za kuwafikia na kuwapatia wateja wetu wote bidhaa na huduma bora kote nchini”.



Bw. Anurup Chatterjee, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Al Mansour – Isuzu alisema “Al Mansour kama mfanyabiashara aliyeidhinishwa wa ISUZU amewekeza dola milioni 1.5 katika soko la Tanzania tangu kuanzishwa kwake na uwekezaji huu pia unaonyesha imani ya ISUZU katika sekta ya vifaa vya moto hususani magari na soko lake limekuwa imara katika uchumi wa kikanda katika muongo huu na ujao”.



Akihitimisha, Bw.Anurup Chatterjee aliongeza “ Kwa miaka mingi tumeonyesha juhudi katika kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa usafiri hasa usafiri wa kutumia magari na imehakikisha wanatoa huduma bora za usafiri nchini ikiwa ni sehemu ya msaada wake katika kuhakikisha huduma za usafiri zinakuwa bora na nafuu nchini Tanzania".



Aina za magari ya Isuzu yameunganishwa mahususi na kurekebishwa kuendana na hali ngumu ya kimiundombinu ya Afrika Mashariki. Aidha, Isuzu imeweka mtandao imara baada ya mauzo ili kusaidia wateja wake katika sekta binafsi na ya umma, ili kuhakikisha magari yao yanaendelea kutumika katika eneo lolote lile, na kwa vipengele hivyo tunatarajia kuleta matokeo chanya kwa wateja wa Tigo Tanzania na wateja wetu wengi zaidi Tanzania.”

KUHUSU 
AL MANSOUR

Kundi la Al Mansour ni shirika la kimataifa, linalomilikiwa na familia na lina wafanyakazi 60,000, linapatikana katika zaidi ya nchi 100 na mapato ya jumla yanayozidi dola bilioni 6. Kundi hili lilianzishwa zaidi ya miaka 60 iliyopita, linasimamia biashara zilizofanikiwa katika sekta kadhaa na lina ushirikiano wa muda mrefu na baadhi ya chapa zinazoongoza duniani ikiwa ni pamoja na Isuzu. Al Mansour Auto EA iliteuliwa mnamo tarehe 1 Julai 2020 na Isuzu East Africa kama muuzaji rasmi wa magari wa Isuzu nchini Tanzania, baadae waliwekeza takribani dola milioni 1 ili kuanzisha biashara jijini Dar es Salaam. Uuzaji huu ulizinduliwa rasmi tarehe 14 Januari, 2021. AL Mansour Tanzania ni kampuni tanzu inayomilikiwa kikamilifu na Mansour Group ambayo ni muungano wa kimataifa ulioanzishwa nchini Misri, unaoendesha shughuli zake kote ulimwenguni. Kampuni hiyo ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Misri kwa mapato. Ni muuzaji mkubwa wa General Motors ulimwenguni, na msambazaji wa tano kwa ukubwa wa Caterpillar Inc.

Specialized Rentals Limited (SRL) ni sehemu ya Kundi Maalumu la Cos, lenye makao yake makuu nchini Tanzania. Kundi hili limejikita katika sekta mbalimbali kama vile Usafirishaji na Usambazaji wa vifaa vya moto, biashara ya bidhaa za Uhandisi na wamejikita pia katika Teknolojia ya mtandao. Kupitia makampuni yake ya Specialized Hauliers Pvt Ltd, Specialized Engineers Tz Pvt Ltd. & Specialised IT Solutions Pvt Ltd. Kundi hili limezidi kukuwa kwa kasi na kwa kipindi cha miaka 28 ya kuwepo kwake na daima limejiimarisha kama moja ya kundi linalotoa huduma bora kwa wateja.

KWA MASWALI ZAIDI

Barua pepe: ndeshi_rajabu@mactanzania.com
Nambari ya mawasiliano: +255 785 967434





No comments:

Post a Comment