Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 12 May 2022

BIMA YA KILIMO YA BENKI YA NMB YAMKOMBOA MKULIMA


Tunafahamu kilimo chetu Watanzania kinategemea hali ya hewa, hivyo hasara ya kutokupata mazao inaweza kutokea. Ikishirikiana na makampuni ya bima, Benki ya NMB inamlinda mkulima dhidi ya hasara ya itakayotokana na mvua ya mawe, moto, ukame, mvua nyingi, uharibifu wa baridi, mafuriko na radi.

Kwa mujibu wa NMB, bima hii inahusisha mazao yote ya biashara ikiwemo; Ngano, mahindi, shayiri, mpunga, chai, kahawa, miwa, tumbaku, mazao yote ya mbogamboga, maua na mazao ya miti.

Pia, unaweza kununua bima hii kwa ajili ya mali na vifaa vya kilimo pamoja na mazao yaliyovunwa, shamba kitalu na vifaa vya umwagiliaji.

Vile vile, bima hii inategemea na thamani ya pembejeo au bei ya soko iliyokubaliwa mapema ya mazao yaliyopandwa.

Faida ukiwa umebima shamba lako kupitia Benki ya NMB;
  • Utapata mikopo ya kilimo kwani hati ya sera ya mazao inakubaliwa na taasisi za kufadhili kama njia mbadala ya dhamana.
  • Kujikinga dhidi ya hasara kwa kupewa kiinua mgongo kipindi cha msimu mbaya wa mazao.
  • Elimu ya biashara ya kilimo kupitia wataalamu wetu katika sekta hio. 
Bima hii ya mazao ni uvumbuzi wa kifedha ambao huchochea uwekezaji katika sekta ya kilimo kupitia kuongezeka kwa ufikiaji wa fedha na motisha kwa wadau wote.

Kisichokingwa na bima hii ni hasara yoyote ya mazao itokanayo na majanga ambayo hajakatiwa bima, kupungua kwa mazao na kupungua ubora kwasababu ya usumbufu au ajali katika mchakato mzima wa kazi.

Pia, hasara itokanayo na ucheleweshwaji uvunaji, kukamatwa au kushikiliwa, kuzuia mazao au vifaa, makosa katika matumizi ya dawa kwa kushindwa kufuata mapendekezo juu ya taratibu za matumizi, wizi, upotevu usieleweka na hasara isiyohesabika.

Kiwango cha bima kinategemea aina ya mazao, eneo, ukubwa wa shamba na idadi ya vihatarishi. Kiwango hiki ni kati ya asilimia 4.5 na 6 kwa ujumla inayokatiwa bima.

Unachohitaji ni;
  1. Fomu ya maombi iliyojazwa kikamilifu na malipo ya bima
  2. Ripoti ya mazao kupandwa iliyoandaliwa na mtoa bima
  3. Muafaka wa madai
  4. Hasara ya mazao/uzalishaji
Malipo yote ya madai yatafanyika mwisho wa msimu wa mazao, hata hivyo inapotokea hasara kubwa inayohitaji kuotesha mazao upya basi malipo yatafanyika kuwezesha kuotesha mazao upya.

Tembelea tawi lolote la benki ya NMB lililopo karibu yako kujipatia bima hii.

Umebima-SiNgumuKihivyo!

No comments:

Post a Comment