Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema kumekuwa na mafanikio makubwa katika uhamasishaji wa matumizi yasiyohusisha pesa taslimu na kuwataka wateja kuendelea kutumia kadi zao na Vituo vya Mauzo (PoS), ili kujiongezea nafasi ya kushinda katika fainali.
Droo hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NMB, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam, ilichezeshwa chini ya uangalizi wa Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili, ambaye aliwahakikishia wateja kuwa washindi hupatikana kwa njia halali na kwamba vigezo na masharti vinazingatiwa.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Fatma Hassan Toufiq, amefanikiwa kuwa miongoni mwa washindi 100 wa droo ya 10 ya msimu wa tatu wa Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu na alikiri kwamba yeye ni mteja wa muda mrefu wa NMB, na kwamba kwa kipindi chote hicho amekuwa ‘Balozi Mwema’ wa benki hiyo - miongoni mwa jamii inayomzunguka, wakiwemo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaoshirikiano nao.

Kujiweka kwenye nafasi ya kushinda droo ya mwisho ya ‘Grand Finale’ ni rahisi, endelea kutumia NMB Mastercard kufanya malipo mtandaoni, kwa QR code au POS na unaweza kujiweka kwenye nafasi nzuri yakuingia kwenye draw.
No comments:
Post a Comment