Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 10 August 2021

VODACOM YAZINDUA KAMPENI YA “KIMBIZA NA 4G YA UKWELI”

Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Kimbiza na 4G ya Ukweli". Uzinduzi wa kampeni hii unalenga kuifahamisha jamii kuhusu kasi na uhakika wa mtandao wake unaowezeshwa na uwekezaji makini katika teknolojia pamoja na upana wa huduma inazotoa kwa wateja wake.
  • Vodacom Tanzania PLC ina mtandao mpana wenye kasi kuliko mingine nchini kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye minara na vifaa vingine.
  • Kuna ofa mbalimbali zilizobuniwa kulingana na matumizi ya mteja.
  • Kampeni inalenga kuifahamisha jamii kuhusu mtandao wa Vodacom, ubora wake kiteknolojia na manufaa yake kwa jamii.
10 August 2021, Dar es salaam - Kampuni ya teknolojia na mawasiliano inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania Plc imezindua kampeni mpya inayokwenda kwa jina la “Kimbiza na 4G ya Ukweli”. Kampeni hii inalenga kuifahamisha jamii kuhusu kasi na uhakika wa mtandao wake unaowezeshwa na uwekezaji makini katika teknolojia pamoja na upana wa huduma inazotoa kwa wateja wake. Uzinduzi huu umefanyika jijini Dar es Salaam.

Akiongea na wakati wa zuinduzi huo, kwa niaba ya Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano bi Rosalynn Mworia, alisema, “Vodacom tumekuwa tukiendelea kuwekeza na kuboresha mtandao wetu ili kuhakikisha tunawapa wateja wetu teknolojia ya kisasa kabisa pamoja na bidhaa na huduma za kibunifu kuliko zingine sokoni.”

Aliongeza kwamba dhamira hii imezaa mtandao bora wa 4G na wa kuaminika, ulio mpana na wenye kufikia maeneo ambayo wengine bado wanajifikiria kufika. Upana huu wa kipekee pamoja na uwezo kiteknolojia unawapa watumiaji wake huduma bora kabisa za sauti, ujumbe mfupi na kupata intaneti yenye ubora zaidi.

Kwa muda mrefu sasa, Vodacom Tanzania Plc imekuwa ikiwekeza kwenye mtandao kwa kiwango kikubwa kuliko kampuni zingine za mawasiliano na sasa inamiliki zaidi ya minara 3,500 ya 2G, zaidi ya 3,000 ya 3G na zaidi ya 2,000 ya 4G, jambo ambalo linaipa Vodacom mtandao mpana zaidi na wenye kasi zaidi kuliko mingine nchini. Mtandao huu unawafikia asilimia 92 ya wananchi.

Katika hafla hiyo, ilielezwa kuhusu matokeo chanya ya mtandao huo kwa jamii. Matokeo haya yametokana na dhamira ya kampuni ya Vodacom kutimiza mkataba wake na Jamii, mkataba unaoiongoza katika jitihada za kujenga Jamii ya Kidijitali, Ushirikishwaji kwa Wote na Kujali Dunia. Kupitia uwezo wake mkubwa wa teknolojia, Vodacom Tanzania inatumia mtandao wake kutoa huduma muhimu, mawasiliano ya uhakika na rafiki hivyo kuwawezesha watanzania wengi zaidi kuonja maisha ya kidijitali.

Akifafanua zaidi jinsi mtandao wa Vodacom unavyowawezesha watumiaji wake, Mworia alisema, “Vodacom Tanzania ina mpango wa kuhakikisha taifa zima linakuwa na jamii inayozingatia ujuzi na uelewa kupitia matumizi ya TEHAMA, wakati huohuo tukipunguza utofauti kati ya upatikanaji wa mawasiliano pamoja na kuboresha huduma zetu za data na sauti. Dhamira hii imetupelekea kuongeza idadi ya huduma zetu kwa wateja mpaka kufikia sehemu sasa tunatoa huduma anuwai zaidi ya mawasiliano peke yake.”

Mtandao wa Vodacom unawapa watumiaji wake jukwaa rafiki linalowawezesha kufanya manunuzi, malipo, kupokea na kutoa miamala, mikopo huku wakiwekeza na wakati huohuo wakidhibiti na kufuatilia matumizi yao.

Mtandao huu wenye kasi kubwa na wa uhakika, pia unawawezesha watumiaji kuwa na taarifa mpya juu ya matukio muhimu. Kwa wanafunzi na waelimishaji, inawapatia jukwaa bora kabisa nchini lenye maudhui mbalimbali ya elimu na sasa linatumika hata kufuatilia maendeleo ya wanafunzi mashuleni na kuwapa wazazi taarifa muhimu za Watoto.

Katika kampeni hii, kila mteja atapata ofa maalum inayoitwa “Ya Kwako Tu”, inayotoa vifurushi vilivyoandaliwa maalum kwa watumiaji wa Vodacom kuendana na matumizi ya kila mteja.

Kumalizia, Mworia alifafanua sababu ya kufanya kampeni hii na inamaana gani kwa wateja wa Vodacom, “Kupitia kampeni hii ya ‘Kimbiza na 4G ya Ukweli’ tunataka watumiaji kupata ufahamu kuhusu kasi na ubora wa mtandao wetu na pia kujielimisha juu ya vifurushi maalum vilivyopo ili kuongeza tija wanayopata kutokana na kutumia mtandao wetu supa. Tunawahimiza wateja wa Vodacom kuendelea kufurahia kasi bora ya intaneti kupitia mtandao wetu”.

Ili kupata vifurushi hivi maalum, mteja anatakiwa kubofya namba *149*01# kisha kuchagua namba 1 – “Ya Kwako Tu” halafu achague kati ya vifurushi maalum vitakavyoonyeshwa.

Katika mkutano huo, pia kulikuwa na fursa kwa waliohudhuria kujionea wenyewe teknolojia na huduma za Vodacom. Ambapo pia Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano aliwahamasisha watumiaji wa Vodacom kuendelea kutumia mtandao huo na kwa ambao hawajajiunga kufanya hivyo ili kujionea ubora wa mtandao unaoaminika kuliko mingine nchini.

No comments:

Post a Comment