Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 6 August 2021

BENKI YA BIASHARA TANZANIA YAONGOZA KUUNGANISHA HUDUMA ZA KIBENKI MTANDAONI NA MIFUMO YA MALIPO


Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imekuwa benki ya kwanza nchini kuunganisha huduma zake za kibenki mtandaoni na mifumo yote ya kitaifa ya malipo.

Afisa Mtendaji Mkuu wake, Bw, Sabasaba Moshingi, amesema maboresho yaliyofanyiwa mfumo wa soluhisho hiyo ya kidijitali unaifanya huduma ya TCB Internet Banking kuwa ya kipekee na isiyokuwa na mpinzani sokoni.

“Suluhisho hii imebuniwa na kutengenezwa na wataalam wetu wenyewe bila gharama yoyote na ubora wake dhidi ya mifumo mingine ni kuunganishwa kwake na mifumo yote ya kitaifa ya malipo,” Bw Moshingi alitabainisha jana wakati wa unzinduzi wake jijini Dar es Salaam.

“Tungeinunua sokoni ingetugharimu kati ya dola 300,000 na 500,000,” alifafanua akionyesha unafuu wake kwani bei hizo ni sawa na TSh milioni 695.7 na karibu TSh bilioni 1.16 mtawalia.

Kwa mujibu wa Bw. Moshingi, uwekezaji wa kuboresha huduma ni sehemu ya mpango mkakati wa kuimarisha suhuhishi za kibenki za TCB na kuzifanya za kisasa zaidi ili ziendane na mahitaji ya soko.

Alisema maboresho ya TCB Internet Banking pia yanalenga kuiwezesha benki hiyo kujipanga vizuri zaidi kibiashara na kujiimarisha kiushindani sokoni.

Serikali imeipongeza benki hiyo kwa kufanya maboresho hayo na kusema yataongeza thamani kwenye mifumo ya kitaifa ya malipo.

Akizumgumza kabla ya kuizindua rasmi huduma hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw Emmanuel Tutuba, alisema uwekezaji huo pia unalipa na kuifanya TCB kuwa tishio.

Kiongozi huyo amewahasa wananchi na taasisi zote kujiunga na mfumo huo mpya wa TCB ili waweze kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi, usalama na uharaka ili waweze kuongeza ufanisi katika shughuli zao.

“Nimefurahi kusikia kuwa mfumo huu pia umeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa MUSE ili kurahisisha taasisi za serikali kufanya malipo pasipo na ulazima wa kutembelea benki,” Bw. Tutuba alisema.

MUSE ni mfumo wa ulipaji serikalini ambao ni sehemu ya mchakato wa serikali mtandao kwa ajili ya kuziwezesha taasisi za umma na makundi mengine kama watumishi, raia, wanafunzi na wafanyabiashara kupata taarifa na huduma kwa njia ya intaneti.

Katibu Mkuu Tutuba ameichagiza TCB kutumia umahiri wake wa ubunifu kusaidia kutafuta ufumbuzi wa maswala mbalimbali na kusaidia kutatau changamoto mbalimbali kama kupunguza gharama za mikopo na riba kubwa.

Akiutambulisha mfumo huo, Meneja Mkuu Suluhishi za Biashara wa TCB, Bw Leonard Katamba, alisema huduma hiyo imebuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na maendeleo ya kidijitali ya siku za usoni.

“Huduma ya TCB Internet Banking itatoa wigo mpana wa huduma za kibenki kwa wateja wetu; taasisi za serikali, makampuni, mashirika ya dini na mengine yasiyo ya kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wafanyakazi, vikundi mbalimbali, taasisi za elimu pamoja na mtu mmoja mmoja,” alifafanua.

“Mfumo huu pia unawazesha wateja kufanya miamala ya kibenki ndani na nje ya nchi kupitia mifumo kama TISS, EFT na SWIFT, ukusanyanji mapato ya serikali na tozo kieletroniki (GePG), miamala ya simu, malipo ya mishahara na kupata taarifa zote muhimu za kibenki.”

No comments:

Post a Comment