Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 17 June 2021

BENKI YA TPB YAZINDUA BIMA MAISHA KWA WATEJA WAKE

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Alliance Life Assurance (kushoto) Byford Mutasisakwa wakisaini mikataba mara baada ya kuongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa huduma mpya ya BIMA Maisha kwa wateja wa Benki ya TPB. Uzinduzi huo mfupi ulifanyika jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Benki hiyo.

Alhamisi, Tarehe 17 Juni 2021 - Benki ya TPB kwa kushirikiana na Kampuni ya Alliance Life Assuranceimezindua Bima Maisha kwa Wateja wenye Akaunti binafsi katika Benki ya TPB ambalo ni fao linalotolewa kwa wateja wenye akaunti binafsi wa Benki ya dhidi ya tukio la kifo cha mteja, mwenza, watoto (Wasiozidi wane) na ulemavu wa kudumu wa mteja unaotokana na ajali. Fao hili ni kwa wateja wa Benki ya TPB wenye akaunti binafsi.

Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya TPB, Bw Francis Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema, “Kuna mafao mawili ambayo yatakuwa yakitolewa ikiwemo fao la kifo na fao la ulemavu wa kudumu.” “Fao la kifo ni fao kwa wateja wenye akaunti za akiba dhidi ya tukio la kifo cha mmiliki wa akaunti, mwenza na watoto wasiozidi wanne (4),” aliongeza Kaaya. Benki ya TPB itatoa kifuta machozi kwa mteja au familia kama rambirambi ili kutatua baadhi ya gharama zinazohusiana na mazishi.

“Kwa upande wa fao la ulemavu wa kudumu, hili linapatikana kwa mteja/wateja tu ambaye ni mmiliki wa akaunti anayekabiliwa na ulemavu wa kudumu uliotokana na ajali, benki ya TPB itatoa mkono wa pole kumsaidia mwathirika aliyekumbwa na tatizo au familia yake”, alisema Bw. Kaaya.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi aliupongeza uongozi wa Alliance Life Assurance kwa kuweza kugundua umuhimu wa hii huduma kwa wateja wa benki ya TPB. “Benki ya TPB inatambua umuhimu wa bima katika maisha ya kila binadamu, na kwa sasa nchi yetu inakabiliwa na ufinyu wa watu kujiandikisha na bima mbalimbali,” alisema Moshingi. “Huduma hizi hazitokuwa na gharama ya juu, kwa mfano kwa fao la kifo mteja atapata Milioni 2, Mwenza wa Mteja milioni 2 na watoto wa mteja (wasiozidi wane) kila mmoja Milioni1 na kwa upande wa fao la ulemavu wa kuduma ni mteja tu atapata Milioni 2,” aliongeza Moshingi.

Mambo muhimu ya kuzingati katika huduma hii ni pamoja na mafao haya ni kwa wamiliki/mmiliki wa akaunti tu, mnufaika lazima awe mteja wa benki ya TPB mwenye akaunti ya akiba, akaunti lazima iwe hai, hakuna kipindi cha kusubiri, hakuna kikomo cha umri, vifo vya asili na vya ajali vinalipwa na mdai/mteja lazima awasilishe madai yote. Jinsi ya Kudai mteja atahitajika kuwa na nyaraka zifuatazo;-
  1. Nyaraka za Madai lazima ziwawasilishwe kwenye tawi lolote la bank 
  2. Nakala ya cheti cha mazishi / kifo 
  3. Nakala ya cheti cha kuzaliwa ili kuthibitisha uhusiano 
  4. Nakala ya cheti cha ndoa
  5. Ripoti ya polisi kwa kesi zinazohusiana na ujambazi na PF 3 kwa kesi za ajali 
  6. Fomu ya madai iliyojazwa
  7. Nakala ya vitambulisho (NIDA, leseni ya kuendesha gari au pasipoti
  8. Nyaraka Nyingine yoyote ambayo au bank itaomba au kutoa maelekezo Zaidi. 
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Alliance Life Assurance Bw Byford Mutimusakwa aliupongeza uongozi wa Benki ya TPB na kuhakikisha kuwa wateja wote wa benki ya TPB watapata huduma hii pasipo na usumbufu wowote na kusisitiza wananchi nchini wawe na tabia ya kutumia bima ili kuepuka majanga mbalimbali katika maeno wanayoishi na wanayofanya kazi.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tawi la Benki ya TPB lililoko karibu nawe au piga simu +255 765 767 683, +255 788 767 683, +255 658 767 683, +255 773 767 683 au barua pepe info@tpbbank.co.tz, insurance@tpbbank.co.tz au Whatsapp +255 714 846 840

Anwani kamili:-

Benki ya TPB, Makao Makuu,
Jengo la LAPF gorofa ya 10,
Barabara ya Bagamoyo, linatazamana na Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama,
P.O BOX 9300, Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment