- Ni kupitia kampeni yake ya Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo imelenga kutoa elimu juu ya matumizi yenye tija ya mtandao wa 4G
Tukio la utiaji saini makubaliano hayo lilifanyika katika makao makuu ya Zantel yaliyopo eneo Amani-Zanzibar na kushuhudiwa na menejimenti ya Wasafi pamoja na waandishi wa habari.
Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga alisema kampuni hiyo ina imani kubwa na msanii huyo kutokana na ukweli kuwa ni moja ya kipaji kutoka Zanzibar na anaufahamu vema mtandao wa Zantel.
“Zantel kwa sasa tunaendesha kampeni yetu inayojulikana kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ ambayo inalenga kufanya uelimishaji juu ya matumizi yenye tija ya mtandao wa 4G.Zuchu amekuwa mfano mzuri wa namna anavyotumia mtandao wa 4G kuendeleza kipaji chake na ameweza Kupasua Anga kitaifa na Kimataifa,” alisema Muga.
Aliongeza kuwa mbali na uelimishaji, kampeni hiyo imelenga kuinua na kutambua vipaji mbalimbali kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo za michezo, muziki pamoja na uchekesahji ‘comedy’.
“Sote ni mashahidi juu ya namna gani msanii huyu alivyoweza ‘Kupasua Anga’ na kuwa mmoja ya msanii wa kike mashuhuri hapa nchini. Zuchu anakwenda kuwa balozi wa Kampeni yetu hii ya Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo itafanyika kwa muda wa miezi 6 mfululizo,” alisema.
Katika ulimwengu huu wa kidigitali, simu ya mkononi imekuwa sehemu muhimu sana ya maisha yetu.Kupitia simu tu,unaweza kufanya mambo mengi sana kwa haraka na urahisi zaidi. Mfano, kukata tiketi za safari mbali mbali kama ndge au boti, kununua na kuuza bidhaa mbali popote ulimwenguni,kujiendeleza kielimu, kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki na mengine mengi.
Kwa kutambua hilo, Kampuni ya Zantel tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtu anafikiwa na mtandao wetu hasa intaneti yenye kasi ya 4G ili kuishi maisha ya kidigitali.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Zuchu alisema “Nimefurahi sana kuwa balozi wa kampeni hii ya Pasua Anga Ki Zantel 4G, ukizingatia mimi ni moja ya wasanii kutokea Zanzibar hivyo naifahamu vizuri Zantel,” alisema na kuongeza
“Intaneti ni kitu muhimu sana kwangu, siwezi kukaa masaa 24 bila kuwa na mtandao hasa mtandao wa 4G ambao utaniwezesha kufanya mambo mbalimbali kwa haraka zaidi,” alisema Zuchu.
Zuchu anakuwa balozi wa kampeni hiyo ambayo itadumu kwa miezi sita ambapo atafanya mambo mbalimbali ya uelimishaji kupitia matamasha ya muziki pamoja na mitandao ya kijamii.
Pasua Anga Ki Zantel 4G!
No comments:
Post a Comment