Foreign Exchange Rates

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Monday, 7 December 2020

WATEJA BENKI YA NCBA WAFURAHIA PUNGUZO LA BEI MADUKA YA GSM

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya NCBA, Julius Konyani akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni ya “ Nenda shopping na punguzo kutoka NCBA” ambapo wateja wa benki ya NCBA wataweza kupata punguzo la asilimia 10% watakapofanya manunuzi kupitia maduka ya GSM kote nchini kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu. Kulia ni Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Utaifa wa Benki hiyo, Caroline Mbaga.
Afisa Masoko wa GSM, Fatma Farah akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni ya “ Nenda shopping na punguzo kutoka NCBA” jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya NCBA, Julius Konyani (katikati) akipeana mikono na Afisa Masoko wa GSM, Fatma Farah mara baada ya uzinduzi wa promosheni ya “ Nenda shopping na punguzo kutoka NCBA” ambapo wateja wa benki ya NCBA wataweza kupata punguzo la asilimia 10% watakapofanya manunuzi kupitia maduka ya GSM kote nchini kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu. Kulia ni Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Utaifa wa Benki hiyo, Caroline Mbaga. Hafla ya uzinduzi imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Watumiaji wa kadi za NCBA Bank VISA Debit na VISA Credit card kupata punguzo la bei la 10% wanapofanya manunuzi katika maduka ya GSM Retail

Desemba 7, 2020 - Benki ya NCBA inawazawadia wateja wake wa NCBA Visa Debit na Visa Credit card kwa punguzo kubwa la gharama kila mara wanapofanya manunuzi katika maduka ya GSM Retail msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya “ Nenda Shopping na punguzo kutoka NCBA” iliyofanyika katika mojawapo ya maduka ya GSM jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya NCBA , Bw Julius Konyani alisema promosheni hii ni sehemu ya utamaduni wa benki hiyo wa kuwaheshimu na kuwazawadia wateja wake, ili kuwahamasisha wafikie malengo.

“Wateja wa Benki ya NCBA watapata punguzo la bei la asilimia 10% papo kwa hapo, kila mara watakapofanya manunuzi ya TSH 150,000 au zaidi na kutumia kadi zao za NCBA Bank VISA Debit na NCBA Bank Credit card kufanya malipo katika maduka ya GSM Retail,” alisema Konyani.

Naye Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Utaifa wa Benki ya NCBA, Caroline Mbaga aliongeza kuwa lengo la promosheni hiyo ni kuongeza matumizi ya malipo kwa njia za kidigitali kama njia ya uhakika, salama na rahisi kufanya malipo kote duniani.

“Benki ya NCBA ni kinara wa matumizi ya mifumo ya kifedha ya kidigitali, Tulikuwa benki ya kwanza kabisa nchini kuzindua kadi za Visa Credit card. Katika msimu huu wa sikukuu, msimu wa furaha, utulivu, kugawa zawadi na kujenga kumbukumbu za kudumu na unaowapenda; NCBA tunarudisha shukrani zetu kwa wateja wetu ambao wanatumia mifumo ya kidigitali kufanya malipo,” alisema.

Naye Afisa Masoko wa GSM Retail, Fatma Farah alifafanua kuwa promosheni hiyo ya inahusu maduka ya GSM Retail yaliyopo Msasani, Mlimani City, Aura Mall na barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam, pamoja na miji ya Dodoma na Arusha.

“Nawakaribisha wateja wote watembeee maduka yetu ya GSM Max, Babyshop, Splash, Shoe Express, Courtefiel na Home Box ili wajipatie bidhaa bora kwa bei nafuu pamoja na kufurahia punguzo hili kabambe la bei kutoka benki ya NCBA,” alisema Farah.

No comments:

Post a Comment