Foreign Exchange Rates

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Monday, 7 December 2020

AKIBA COMMERCIAL BENKI YADHAMINI VICOBADAY 2020

Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Innocent Ishengoma akizungumza na wanavicoba pamoja na wateja wa Benki hiyo wakati wa maadhimisho wa siku ya Vicoba day 2020 iliyodhaminiwa na Benki ya ACB, yenye lengo la kuwainua wanavicoba na wafanya biashara ndogondogo waweze kufikia malengo yao kupitia Benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa PTA sabasaba jiji Dar es Salaam hivi karibuni. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu wa Baraza la Uwezeshaji wa Kiuchumi Bi Beng'i Issa.
Meneja Mahusiano wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Judith Kipingu akimfungullia akaunti mteja mpya wa Benki hiyo, Joyce Charles wakati wa hafla ya wakati wa maadhimisho wa siku ya Vicoba day 2020 iliyodhaminiwa na Benki ya ACB. Kulia ni Afisa Mauzo wa Benki ya ACB, Elizabeth Masolwa.
Baadhi ya wanavicoba na wateja wa Benki ya ACB wakiwa katika hafla ya Vicoba day.
Meneja Mahusiano wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB),  Judith Kipingu akimkabidhi zawadi ya tisheti Mteja wa kwanza aliekwenda kufungua akaunti katika Benki hiyo, Joyce Charles wakati wa hafla ya maadhimisho wa siku ya Vicoba day 2020 iliyodhaminiwa na Benki ya ACB. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa PTA sabasaba jiji Dar es Salaam hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment