Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akionesha mfano wa hudi hizo juu mara baada za kukabidhiwa. |
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea mfano wa hudi ya shilingi milioni 100 zilizochangwa na wakimbiaji wa NMB Bima Marathon, fedha zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa watoto kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akikabidhi hundi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede, pamoja naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ambao ni waratibu wa mbio hizo, alisema wameguswa na kundi hilo la wagonjwa wa saratani ambao wanaitaji msaada hivyo kuamua kuwasaidia kwa kiasi kilichopatikana.
Baada za Waziri Mkuu Majaliwa kukabidhiwa hundi hizo, alimkabidhi rasmi moja kwa moja Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ambapo alieleza kuwa gharama kubwa za matibabu za ugonjwa wa saratani imekuwa kikwayo kwa jamii hivyo wanafarijika michango na misaada inazotolewa kusaidia matibabu hazo.
Mbio za NMB Bima Marathon zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam zimeshirikisha wakimbiaji mbalimbali wa kuanzia kilomita 5, 10, 20 ambapo zimekuwa na muitikio mkubwa wa washiriki kutoka makampuni anuai, ambapo washindi walikabidhiwa medali na fedha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) akizungumza katika NMB Bima Marathon. |
Kulia mwalimu wa mazoezi za viungo akiongoza mazoezi ya viungo kwa washiriki wa NMB Bima Marathon. |
Mazoezi ya viungo kwa washiriki wa NMB Bima Marathon wakiendelea. |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na maofisa wengine waandamiyi toka NMB na washiriki wengine wa NMB Bima Marathon. |
Baadhi za washiriki wa NMB Bima Marathon wakivishwa medali mara baada za kumaliya mbio zao. |
Picha za pamoja ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa meza kuu pamoja na wadau wa NMB Bima Marathon. |
Picha za pamoja ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa meza kuu pamoja na washindi mbalimbali. |
Picha ya pamoja ya NMB. Courtesy of Michuzi Blog... |
No comments:
Post a Comment