Mratibu wa Mauzo mkoa DKT International Tanzania, Emma Saronga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa kondomu mpya ya kiume Kiss jijini Dar es Salaam. |
Watanzania sasa wanaweza kujikinga vizuri zaidi na athari zitokanazo na magonjwa ya kujamiiana (STI's) baada ya kuzinduliwa kwa kondomu mpya ya kiume ya Kiss Condom.
Kondomu ambayo imezinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika maonesho ya ubora wake, Condom ya Kiss ni bidhaa ya kiwango cha juu inayopatikana kwa bei nafuu, hii inamsaidia mwanaume na mwanamke wenye kipato cha kati kushiriki katika ngono salama.
"Kondomu mpya iliyozinduliwa ya KISS Condom ina harufu nzuri ya Vanilla na ni condom bora kwa watu wazima walioridhiana. Inadhihirisha kazi kubwa iliyoanzishwa na Wizara ya Afya na Mamlaka ya Dawa Tanzania (Tanzanian Medicines and Drugs Authority) katika kukabiliana na kusambaa kwa maambukizi yatokanayo na kujamiiana na mimba zisizotarajiwa,"Alisema Bw. Kevin Hudson, Mkurugenzi Mkazi wa DKT International nchini Tanzania.
Kiss Condom ni nembo ya kimataifa inayozalishwa katika viwanda vilivyothibitishwa na WHO. Kitu ambacho kinampa mtumiaji ubora wa juu. Kiss Condom zitakuwa zinapatikana madukani katika baadhi ya maduka ya reja reja yaliyochaguliwa kuanzia tarehe 12 September.
Kondomu ni mbinu ya uzazi wa mpango ya kizuizi kwaajili ya kujikinga na kupambana na HIV/Ukimwi na STI's vile vile ni kizuizi cha mimba zisizotarajiwa ambacho hakiathiri homoni za mwili. Kwa sasa, kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS za mwaka 2020, - Watu wapatao milioni 1.7 nchini Tanzania wanaishi na HIV. Takwimu za UNAIDS zinaonyesha kwamba kuna maambukizi mapya 77,000 ya HIV kila mwaka, na takribani vifo 27,000 vinahusiana na maambukizi ya AIDs
Kiss Condom ni bidhaa ya nyongeza iliyokuja katika muda muafaka miongoni mwa bidhaa nyingi za DKT International Tanzania. Bidhaa zingine ni kama Fiesta na Bull condoms, Vidonge vya uzazi wa mpango vya dharura vya Trust Daisy. (Trust Daisy emergency contraceptive pills) na Dawa ya uzazi wa Mpango ya Trust Lily. (Trust Lily oral contraceptive pills).
Kazi za taasisi ya DKT ina lengo la kuhakikisha kwamba mtumiaji wa mwisho bidhaa zake ana aina mbalimbali za machaguo kukidhi mahitaji yao ya kupanga uzazi. Bidhaa zote zimefanyiwa majaribio kabla ya kusafirishwa kuja Tanzania na kwa mara nyingine tena hufanyiwa majaribio zinapowasili nchini kuthibitisha viwango," Aliongeza Hudson Mkurugenzi wa DKT nchini Tanzania.
DKT International ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) la mauzo kwa jamii linalofanya shughuli zake katika zaidi ya nchi 24 duniani kote. Kama taasisi, DKT ni moja kati ya wasambazaji wakubwa wa bidhaa na huduma zenye ubora za afya ya uzazi katika nchi zinazoendela. Mwaka jana DKT International ambayo ni moja kati ya wasambazaji wakubwa wa bidhaa na huduma za afya ya uzazi duniani walisambaza zaidi ya condom milioni 721 kwa watu wenye uhitaji duniani kote.
DKT International Tanzania ilianza kutoa huduma zake nchini Tanzania mwaka 2015 na imepata usajili wa TMDA wa zidhaa zaidi ya 29 za afya uzazi katika malengo yake ya kuwapatia fursa ya kupatikana kwa huduma endelevu ya afya ya uzazi kwa wale wenye uhitaji Tanzania.
No comments:
Post a Comment