Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 17 September 2020

AKIBA COMMERCIAL BANK YAZINDUA HUDUMA ZA MALIPO YA SERIKALI NA MAKUSANYO YA KODI ZOTE ZINAZOLIPWA TRA KUPITIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI GePG

Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara wa Benki ya Biashara ya Akiba Commercial Benki (ACB), David Karosso (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za malipo ya Serikali na makusanyo ya kodi zote zinazolipwa TRA kupitia mfumo wa Kieletroniki GePG. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kuhamisha Fedha wa Benki hiyo Fredy Chaji, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa akiba Commercial Benki Dora Saria. 
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki, Dora Saria (katikati) akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za malipo ya Serikali na makusanyo ya kodi zote zinazolipwa TRA kupitia mfumo wa Kieletroniki GePG. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara wa Benki ya Biashara ya Akiba Commercial Benki (ACB), David Karosso pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Kuhamisha Fedha wa Benki hiyo Fredy Chaji (kushoto).

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA HUDUMA ZA MALIPO YA SERIKALI NA MAKUSANYO YA KODI ZOTE ZINAZOLIPWA TRA KUPITIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI GePG

Mabibi na Mabwana

Wawakilishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari

Menejimenti na Wafanyakzai wa Akiba Commercial Bank

Itifaki ikizingatiwa

Habarini za Asubuhi

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa ajili ya siku njema ya leo. Pia kwa namna ya pekee napenda kutoa shukarani zangu kwa vyombo vyote vya habari vilivyojumuika nasi siku ya leo. Karibuni sana.

Akiba Commercial Bank ni benki ambayo inatoa huduma zake kwa wateja wa chini na wakati yaani MSME toka kuanzishwa kwake miaka ishirini na mitatu iliyopita. Benki inatoa huduma zinazolenga na kukidhi mahitaji ya soko lake. Aidha Benki imekuwa ikifanya tafiti na tathimini za huduma zake mara kwa mara kwa lengo la kuboresha huduma zake ikiwemo kuanzishwa kwa huduma mpya pale inapohitajika.

Aidha Benki, imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 5 ya azima ya ‘Tanzania ya Viwanda’ kwa kutoa mikopo inayosaidia wajasiriamali mbali mbali wakiwemo wale wa viwanda vidogo vidogo.

Kama mdau mmojawapo Benki inaunga mkono jitihada za Serikali za ukusanyaji wa mapato yake na malipo mbali mbali kwa kuunganisha mifumo ya Benki na Mfumo wa Serikali wa malipo ya Kielektroniki wa GePG – Government Electronic Payment Gateway.

Matawi yote ya Benki ya Akiba yanatoa huduma za kukusanya Kodi zote za TRA bila gharama yeyote. Naomba nisiisitize kuwa huduma hii ya kufanya malipo ya Serikali inapatikana kwa watu wote, yaani wateja wa Akiba na wasiokuwa wateja. Hivyo Walipa kodi wanaweza kujipatia huduma hii katika matawi yetu yote bila changamoto yeyote, cha msingi ni kuwa na ile control number ya malipo.

Pia wateja wetu wote wanaotumia huduma yetu ya Akiba Mobile waweza kufanya miamala ya Malipo mbali mbali ya Serikali kama kulipia kodi, Dawasco, Faini za Traffic, Bima za Afya n.k .

Huduma hizi zinapatika kwa urahisi kabisa na zinaokoa muda na gharama.

Hivyo basi lengo kuu la kuwaita hapa siku ya leo ni kutoa taarifa rasmi kwa umma wa Tanzania kwa kuwatangazia kuwa wanaweza kutumia Benki ya Akiba kulipa malipo ya Serikali zikiwemo kodi zote za TRA na huduma nyinginezo. Aidha, natoa rai pia kwa taasisi mbali mbali za Serikali kufungua akaunti katika Benki ya Akiba kusudi wananchi waweze kupata wigo mpana na unafuu zaidi wa kufanya malipo mbalimbali ya serikali. Hii pia itarahisha na itaboresha mfumo mzima wa ukusanyaji wa mapato ya

Serikali ambayo yanasaidia katika shughuli mbali mbali za maendeleo ya wananchi.

Mwisho kabisa, tunawashukuru wote mlioitikia wito wetu wa kufika na tunaamini kupitia nyie mtafikisha ujumbe wetu kwa umma na tunategemea mwitikio mkubwa kwa wananchi kutumia Benki yetu kufanya malipo ya Kodi zote pamoja na malipo mengine ya serikali. Nia yetu ni kutoa mchango wetu kwa Serikali katika mchakato mzima wa kuboresha mfumo wa makusanyo wa mapato.

Kwa kumalizia tunapenda kuipongeza Serikali kwa jitihada zake nzuri za kuboresha mfumo wa kukusanya mapato kidigitali kwa kuanzisha GePG.

Vile vile tunaipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za Uchumi wa Kati

Tunatoa rai kwa taasisi zingine za fedha kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukusanya mapato kwani tunashuhudia mafaniko na maendeleo ya nchi yetu kupitia nguvu zetu wenyewe.

Asanteni kwa kunisikiliza

Ni David Koroso – Meneja Mwandamizi kitengo cha Biashara

No comments:

Post a Comment