Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 14 March 2020

NBC YAZINDUA KLABU YA BIASHARA MASASI, YATOA MAFUNZO YA KIBIASHARA

Mkuu wa Wilaya ya Masasi Selemani Mzee akipiga makofi wakati wa uizinduzi wa NBC Business Club kwa wilaya hiyo NBC Businee Club kwasasa imeenea katika mikoa mbalimbali ikiwepo Tanga, Arusha, Moshi, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Singida pamoja na Lindi ikia ni dhumumuni la kuwakutanisha na kuwaongezea ujuzi pamojha na kuwakuzia mtandao wafanya biashara, wengine pichani ni Meneja wa Tawi la NBC Masasi, Erick Mbeyela, Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha wa NBC Jonathan Wilson, pamoja na maofisa wengine wa NBC.
Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha wa NBC Jonathan Wilson, akizungumza na wafanya biashara wa wa Wilaya ya Lindi wakati wa uzinduzi wa Biashara club iliozinduliwa na Benki ya katika wilaya ya Masasi hafla ya uzinduzi huo imefanyika hivi karibuni.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea na mpango wao wa kuanzisha NBC Biashara Club katika wilaya mbali mbali ikiwemo Masasi kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwapa nafasi ya kujadiliana changamoto zao na kupeana fursa mbalimbali. NBC Biashara club inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao wa njia ya Mikopo ya muda, Huduma za ziada za kibenki, Ufundi wa kigheni, POS, Benki ya mtandao, Akaunti za sasa, Dhamana za Benki, Wakala wa Benki na Bidhaa za Bima.

Klabu ya Biashara ya NBC hutumiwa kama sehemu ya utunzaji wa biashara na mkakati wa uaminifu wa wateja. Kusudi kuu ni utoaji wa huduma za msaada zisizo za kifedha kupitia mafunzo ya ustadi wa biashara na kuwajengea uwezo kwa wateja wa biashara wa NBC, kama sehemu ya safari yetu katika kuwaunga mkono.

Akiongea katika hafla ya NBC Business Club iliyofanyika katika Hotel ya Rock City Wilaya ya Masasi, Meneja wa bidhaa na huduma za kifedha NBC Makao makuu Dar es salaam, Bw. Jonathan Wilson Bitababaje alisema, wamezindua NBC Business Club zaidi ya maeneo kumi na moja na Mtwara ikiwa eneo la kumi na mbili ivyo wameandaa fomu maalumu ambazo wafanyabiashara watajisajili kua mwanachama wa klabu iyo na watapata faida mbali mbali ambazo zitawasaidia kuendesha biashara zao.


Faida alizotaja Bw Jonathan Bitababaje ni, Mafunzo ya kukuza na kuendeleza biashara zao, Namna ya kupata mitaji, Namna ya kujua soko, Kuwakutanisha na wanachama wa Biashara Club kutoka mikoa mbali mbali, Jinsi ya kuendesha biashara zao kwa faida, Punguzo la bei kwa bidhaa za NBC na Safari za nje ya nchi amabzo wamekua wakitoa toka mwaka 2017.

Aidha alisisitiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbuka za ulipaji wa kodi kwani itawasaida kuendesha biashara zao kwa faida. Pia alisema Klabu iyo itawasaida kuwapa taarifa mbali mbali kuhusu fursa zilipo ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na kuwapa elimu ya mafunzo stahiki kwa ajili ya kuendana na ukuaji wa teknolojia.

Jonathan alimalizia kwa kusema Serikali imekua mdau mkubwa wa benki iyo na ni mmliki wa benki iyo kwa asilimia 30, ivyo ni muhimu kufwata taratibu zilizowekwa na serikali kwa ajali ya wateja wao. ‘’ Serikali imeweka fursa mbali mbali kwa ajali ya wateja wetu na wateja wanazijua na kuzitumia kwa upana zaidi. Changamoto wanazozipata zitashughulikiwa na benki na serikali yetu.’’

Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bw Selemani Mzee aliunga mkono NBC kwa kusema Klabu iyo ya biashara iwe ni zoezi endelevu ili liweze kuleta tija katika mkoa wa Masasi.Aliongeza kusema kua, kadri watakavyo hudumia wafanyabiashara ndivyo watakavyozidi kuleta fedha kwenye benki.

Alisisitiza wafanyabiashara wa Masasi kua makini na kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili waweza kujiendeleza ki Maisha. Pia walipendekeza utolewaji wa vyeti kwa wafanyabiashara ikiwa ni ishara wa kuwatia moyo.

Kuhusu National Bank of Commerce (NBC)


Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.

Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa ka;ka tanzu tatu tofau;: NBC Holding Corpora;on, Na;onal Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.

Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopa;kana ka;ka maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima.

Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us NBC_Marke8ngDepartment@nbc.co.tz

No comments:

Post a Comment