Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 13 February 2020

MAENDELEO BANK PLC, AIRTEL MONEY NA FSDT WAUNGANA KUZINDUA TIMIZA BIASHARA


Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki Plc Dkt Ibrahim Mwangalaba akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya Timiza Biashara kupitia Timiza vicoba inayowezeshwa na mtandao wa Airtel Money. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano. Maendeleo banki, Airtel na FSDT wameungana kuzindua Huduma hiyo ya Timiza biashra ili kusaidia vikundi vidogo vidogo vya wajasiliamali maarufu kama vicoba kuweza kuweka akibapamoja na kukopa kwa njia ya kidigitali (mtandao) zaidi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano (kati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya Timiza Biashara kupitia Timiza vicoba inayowezeshwa na mtandao wa Airtel Money akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki Plc Dkt Ibrahim Mwangalaba (kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uwezeshaji wa FSDT Dkt. Peter Kingu. Maendeleo banki, Airtel na FSDT wameungana kuzindua Huduma hiyo ya Timiza biashra ili kusaidia vikundi vidogo vidogo vya wajasiliamali maarufu kama vicoba kuweza kuweka akibapamoja na kukopa kwa njia ya kidigitali (mtandao) zaidi.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uwezeshaji wa FSDT Dkt. Peter Kingu akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya Timiza Biashara kupitia Timiza vicoba inayowezeshwa na mtandao wa Airtel Money.
Dar es Salaam, Alhamisi Februari 13, 2020; Maendeleo Bank Plc leo imetangaza kuungana na Airtel Money pamoja na FSDT kwa kuzindua kampeni ya Timiza Biashara ambayo inalenga kusaidia vikundi vidogo vidogo vya wajasiriamali maarufu kama Vicoba ili kuweza kuweka akiba pamoja na kukopa kwa njia ya kidigitali (Kimtandao) zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki Plc Dkt Ibrahim Mwangalaba alisema “kwa kuungana na Airtel Money, Benki yetu inayo Furaha kuzindua suluhisho hili la Timiza Biashara inayowalenga wajasiriamali na wafanya biashara wadogo na wakati hapa nchini. ‘Huduma hii imelenga kutimiza biashara yako na kuleta suluhu ya changamoto ambazo zimekuwa zikivipata vikundi wakati wa kuweka na kukopa katika maeneo mbalimbali wakati inapokuja suala la kuweka akiba na kukopa”.

“TIMIZA BIASHARA kwa kupitia huduma ya TIMIZA VICOBA

inayowezeshwa na mtandao wa Airtel pekee kwa sasa inawawezesha wateja kuunda kikundi cha watu kuanzia 5 mpaka 50, kikundi kinaweza kuundwa na na watu kutoka sehemu yoyote Tanzania na sio lazima wanakikundi kuwa eneo moja ili kuweza kupata huduma hii. Wanakikundi wanaweza kuamua siku gani wataweka akiba zao, mikopo itakuwa ya muda gani na wakati gani watakuwa wanafanya marejesho ya mikopo yao’, alisema Dkt. Mwangalaba huku akiongeza kuwa Timiza Vicoba ni huduma inayotumia mfumo wa kidigitali kukuwezesha kuweka akiba na kukopa kidigitali, mfumo huu unalenga Zaidi kuwawezesha wanakikundi kuweza kuendelea na shughuli zao huku wakiweka akiba na kukopa wakiwa kwenye biashara zao.

Tunawashukuru FSDT ambao wamedhamini kampeni hii kwa nia ya kutoa suluhisho la changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara na wajasiliamali. Kampeni ya TIMIZA BIASHARA inayobeba huduma ya TIMIZA VICOBA inawezesha upatinakaji wa mitaji kwa njia ya kidigitali hapa nchini. Airtel Money ni washirika wetu wa muda mrefu na ni mtandao mpana nchini kwa kuwa unawafikia watu wengi hivyo kufanya huduma ya kifedha kwa mtandao kupatikana kwa urahisi bila hata kutembelea tawi la benki, aliongeza Dkt. Mwangalaba.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurungenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda alisema “Kampeni ya TIMIZA BIASHARA inalenga wajasiriamali na wanavikundi ambao wataunda kikundi cha watu kati ya 5 na 50 na baada ya hapo wanaweza kuanza kuweka akiba na kukopa kwa kupitia TIMIZA VICOBA inayopatikana Airtel Money.

“Lengo la kuzindua kampeni hii ya TIMIZA BIASHARA inayotangaza huduma ya TIMIZA VICOBA ni kuwajengea Watanzania tabia ya kujiwekea akiba na sana sana kwa wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wadogo, tunalenga kufikisha huduma za kifedha kwa alisimia 80 ya Watanzania ambao hawatumii huduma za kifedha kupitia benki. ‘Tutakuwa tukitoa elimu kwa wafanya biashara wadogo na wa kati juu ya umuhimu wa kutumia mtandao kidigitali kwa kuweka akiba na kukopa”, Nchunda aliongeza.

Kwa upande wake, Dkt. Peter Kingu Mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wa wajasiliamali kutoka taasisi ya FSTD alisema kuwa, FSDT imekuwa na agenda kubwa ya kutoa suluhisho ya changamoto za huduma za kifedha hapa nchini na zaidi kwa Watanzania ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa maeneo ya vijijini.

Tunaelewa ni kwa jinsi gani Watanzania wanavyopitia hatua ndefu ili kupata mkopo kwenye taasisi za fedha hapa nchini. Hata hivyo, ukiwa na Timiza Vikoba,

unatakiwa kuanza kujiwekea akiba kidogo kidogo kulingana na uwezo wako, halafu unaanza kukopa kidigitali pasipokutembelea tawi la benki.

Kingu aliongeza kuwa “TIMIZA BIASHARA inalenga kutoa suluhisho ya changamoto ambazo wajasiriamali na vikundi vidogo vidogo wanazopitia wakati wakihitaji mikopo na pia kupanua wigo wa huduma za kifedha hapa nchini kwa mfumo wa kidigtali. Kwa sababu hizo, naomba kutoa rai kwa Watanzania wajasiriamali, wafanyabiashara wadogo pamoja na vikundi vya vikoba kutumia fursa hii ya TIMIZA VICOBA ili kukuza biashara zao”.

No comments:

Post a Comment