Picha ya pamoja ya baadhi ya wateja wakubwa wa Benki ya NMB. |
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa wa NMB, Aziz Chacha, wakati akifungua Jukwaa la Wateja Wakubwa (NMB Executive Network), lililofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma.
Chacha alibainisha ya kwamba, uwezo wa kipesa unaotokana na ukubwa wa mtaji katika benki ya NMB ni mkubwa, unaowawezesha kuhudumia wateja wa kada zote, wakiwemo wateja wakubwa na kumudu kwa asilimia zote mahitaji yao ya kifedha.
Aliongeza ya kwamba wateja wakubwa wana mahitaji makubwa ya kihuduma, lakini wao wana nguvu ya kutosha kuyatimiza na ndio maana wakawaalika katika jukwaa hilo, ili kujadiliana kwa pamoja kujua namna ya kushughulika na changamoto zao na kuzitatua.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NMB, Amour Muro, alisema ‘NMB Executive Network’ ni jukwaa linalotumika kukutana na wateja wakubwa, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
“Hili ni moja ya majukumu yetu katika wiki hii na hii inatusaidia kuzungumza nao kujua namna ya kuongeza thamani ya huduma tunazowapatia. Kupitia Jukwaa kama hili, tunatanua uelewa na kuongeza thamani ya kupitia majadiliano tutakayofanya,” alisema Muro.
Alisema NMB kama taasisi inaamini katika huduma walizonazo, lakini njia bora na sahihi ya kuzifanyia maboresho mbalimbali ni kukutana na makundi tofauti ya wateja, kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi, ili kuwezesha upigaji hatua za maendeleo yao.
Magdalena Magali, ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Saruji ya Tanzania Potland, kwa upande wake aliishukuru NMB kwa kuwaandalia jukwaa maluum wateja wakubwa na kupokea mawazo yao chanya kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wateja na taasisi hiyo kwa ujumla.
Aliipongeza NMB kwa mabadiliko chanya ya kimfumo kutoka analogi kwenda dijitali, uliojikita katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka, wepesi na usalama na kuwataka Watanzania kuchangamkia huduma hizo ili kuokoa muda na kwenda na wakati.
Naye Steven Gideon, ambaye ni Ofisa Mipango na Bajeti wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), alisema kampuni yake inapongeza uamuzi wa NMB kukutana na kujadiliana nao, kwani njia rahisi ya kufikia malengo ni kufanyia kazi changamoto zilizopo ilikusonga mbele.
Gideon aliwataka Watanzania kujali muda na kuendana na kasi za maendeleo kwa kuchagua kuifanya NMB kuwa mshirika sahihi wa ukuaji kiuchumi na kwamba siri ya mafanikio iko katika mapinduzi ya kiteknolojia yaliyofanywa na benki hiyo, yanayoongeza ufanisi kwa wateja.
No comments:
Post a Comment