Ofisa waandamizi wa Benki ya NBC, James Ndimbo akichangia mada kwenye kongamano hilo. |
Ofisa waandamizi wa Benki ya NBC, Godhard Hunja akichangia mada kwenye kongamano hilo. |
Mteja wa benki ya NBC akichangia mada wakati wa kongamano hilo. |
Mteja wa benki ya NBC akichangia mada wakati wa kongamano hilo. |
Muwakilishi kutoka Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Bi Nyakao Mturi akiwasilisha mada wakati wa Kongamano hilo. |
Akizungumza wakati wa kongamano hilo lililofanyika hivi karibuni jijini humo, Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje alisema kufuatia uboreshwaji mkubwa wa huduma za benki hiyo ambazo zinaendana na kasi ya kiteknolojia na fursa za kiuchumi kumekuwa na hitaji kubwa kwa wateja hao kujengewa uelewa ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko hayo.
“NBC kwasasa tumefanya mabadiliko makubwa ya kihuduma yanayoendana na kasi ya kiteknolojia na ukuaji wa uchumi na tumeona kuwa mabadiliko haya yatakuwa na tija zaidi kwa wateja wetu hasa wadogo na wakati ikiwa tu tutawajengea uelewa wa kutosha ili waweze kwenda sambamba mabadiliko haya badala ya kuwa changamoto,’’ alibainisha.
Alisema mbali na kuwajengea uelewa kuhusu huduma za benki hiyo,kupitia kongamano hilo washiriki waliweza kutoa maoni yao ikiwa ni mrejesho wa huduma wanazopata kutoka benki hiyo, hatua aliyosema itasaidia taasisi hiyo kuboresha zaidi huduma hizo sambamba na kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja hao.
Aidha katika kongamano hilo la siku moja, mbali na masuala ya kibenki washiriki walipata fursa ya kusikiliza na kuchangia mada kutoka kwa wawakilishi wa taasisi nyingine ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA) na Baraza la Uwezeshaji (NEEC) ambao walielezea fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi ikiwemo nafasi ya taasisi hizo katika kuwaunganisha wafanyabiashara na wenzao kutoka nje ya nchi.
“Kwa kushirikiana na benki ya NBC tumekuwa tukishirikiana mambo mengi yanayolenga kuwasaidia wafanyabiashara wetu na hivi karibuni tunatarajia kuwasafirisha wafanyabiashara kwenda nchini China kwa ajili ya safari ya kibiashara ya siku kumi ambapo wahusika watalipa gharama ya kiasi cha Dola za Kimarekani 2500 tu ambayo itagharamia mahitaji yao yote ya msingi ikiwemo nauli ya kwenda na kurudi, gharama za chakula na huduma nyingine ikiwemo ya wakalimani,’’ alisema Bw Patrick Magai, Meneja Maendeleo Viwanda kutoka TCCIA.
Wakizungumza wakati wa kongamano hilo lililofutiwa na Uzinduzi wa Klabu wa Wafanyabiashara ya Benki hiyo mkoani humo, baadhi ya washiriki walisema pamoja na huduma za kifedha ipo haja ya taasisi za kifedha hapa nchini kuongeza ushirikiano zaidi na wafanyabiashara hao pindi wanapotafuta zabuni kubwa zenye kuhitaji dhamana kutoka taasisi hizo.
“Pia ipo haja kwa taasisi za fedha nchini kutambua baadhi ya changamoto zinazotukabili wateja wao kwenye biashara zetu kwa kubuni huduma zinazotambua changamoto zetu ikiwemo kuangalia namna ya kushirikiana nasi pindi tunapokabiliwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa malipo yetu kutoka kwa wateja wetu,’’ alisema mmoja wa wafanyabiashara hao ambae ni Mkandarasi, Dr Steven Masangia.
No comments:
Post a Comment