Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na wawekezaji kutoka Jimbo la Zhejiang la China lililofanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019. Katika hotuba yake Mhe. Kairuki alisisitiz akuwa Tanzania ni eneo salama zaidi kuwekeza barani Afrika kutokana na sababu za msingi kama amani, mazingira na sheria rafiki za uwekezaji pamoja na maeneo lukuki ya kuwekeza kama kilimo, madini, usindikaji, viwanda na utalii. Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta binafsi liliwahusisha sehemu ya watalii 300 waliowasili nchini kwa ziara ya kitalii ya siku nne. |
No comments:
Post a Comment