Alisema mafanikio ya uuzaji wa hisa yaliyoifanya benki kuongeza mtaji wake yatasaidia mpango mkakati wao wa kutanua wigo wa huduma zao wakitarajia ndani ya miaka mitano kuwafikia watanzania wengi huku wakiwekeza zaidi katika huduma za kidigitali.
“DCB ilianza mpango wake wa kujitanua kutoka jijini Dar es Salaam miaka miwili iliyopita, safari ya kujitanua inaendelea, tumeshafika Dodoma na maeneo ya karibu, mfumo wetu unaotusaidia ni kutoa huduma bora kwa bei nafuu tukiwekeza zaidi katika mfumo wa kidigatali hivyo kuwa na matawi machache na kuweka vituo vingi vya huduma sehemu mbalimbali nchini,” alisema.
Zoezi la uuzwaji wa hisa za dcb lilizinduliwa Novemba 12,2018 na kuhitimishwa Januari 31, 2019 ambapo hisa 36,635,435 ziliuzwa ikivuka kiwango cha hisa 33,913,948 zilizopangwa awali.
|
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Dodoma, Joseph Njile wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko. |
No comments:
Post a Comment