Uzinduzi wa Mchezo wa namba ujilikanao kwa jina la Supa 5 ukiwa tayari kuzinduliwa rasmi na wananchi kuanda kuucheza mchezo huo kwa njia ya simu zao za Kiganjani.
|
Huu unakuwa ni mchezo pekee kwa sasa nchini Tanzania ambapo mshindi anaweza kupata kiasi kikubwa ndani ya dakika kumi tu. Mchezo wa Supa Tano pia unakuwa ni mchezo pekee wenye kutoa fursa nyingi zaidi za ushindi hapa nchini.
Meneja wa Fedha wa The Network, Bwana Jacob Millinga, amesema ‘Supa Tano ni mchezo mpya wa namba ambao wachezaji wanaweza kucheza viwango mbalimbali kati ya shilingi 1000 mpaka 20,000. Mchezo unatoa nafasi ya kushinda hadi mara 10,000 ya dau uliloweka, ambacho ni kiasi kikubwa kuliko mchezo wowote Tanzania’ anasema Kupitia Supa Tano mchezaji anapata nafasi nyingi zaidi za ushindi, kwani kila namba anayolinganisha analipwa kuanzia namba 2, 3, 4 au namba 5 kwenye droo za kila dakika 10, na wakati huo huo kila shilingi 1000 yake inampa nafasi ya kuingia kwenye SupaMzuka Jackpot siku za Jumapili na Jumatano.
‘Mchezaji anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu namba ambazo zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa.
Mchezo wa Supa 5 unaendeshwa kwa uwazi na usimamizi wa serikali kupitia Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Matokeo yote ya washindi na zawadi walizoshinda yatawekwa kwenye tovuti ya: www.supatano.co.tz.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwakilishi wa Bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), amesema mchezo wa Supa 5 unaongeza fursa nyingine za ushindi kwa watanzania lakini ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa ustaraabu bila kutumia pesa ya matumizi muhimu kwenye mchezo huu.
No comments:
Post a Comment