Wafanyakazi wa benki ya CBA Tanzania wakiwa katika picha ya moja. |
tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi Kaimu Mkurugenzi, Julius Konyani amesema kuwa benki hiyo ndani ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania, imeweza kupata mafanikio kupitia wateja wao.
Aliendelea kudai kuwa ndani ya miaka hiyo kumi benki hiyo imeweza kuwa na wateja wengi wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo na kudai kuwa benki hiyo inatoa mikopo kwa wateja wao.
"Benki yetu ndani ya miaka 10 imeweza kutoa mikopo kwenye makampuni na wafanya bishara ambao ni wateja wao" alisema Kaimu Mkurugenzi.
Mteja wa benki hiyo ambaye ni mfanyabiashara, Isack Lazaro alisema kuwa kupitia benki ya CBA ameweza kupata mafanikio makubwa hasa katika biashara zake.
"Nilijiunga na benki hii muda mrefu sana, nadhani mimi ni mmoja wa wateja wa mwanzoni kujiunga na benki ya CBA tangu ilipoanzishwa Tanzania" alisema Isack Lazaro.
Mteja huyo aliendelea kudai kuwa kupitia biashara zake ameweza kupata mikopo katika benki hiyo kwaajili ya kuweza kuendesha biashara zake kwa kuongezea mtaji.
Mteja mwingine wa benki hiyo, Enock Mwakipesile alidai kuwa tangu ajiunge na benki ya CBA, ameweza kunufaika nayo katika mambo mengi hasa katika biashara zake.
"Tangu nijiunge na CBA nimeweza kunufaika nayo katika mambo mengi hasa kibiashara. Nimeweza kuendesha vizuri biashara zangu na ninapohitaji mkopo wamekuwa wakinipa pamoja na kunishauli mambo ya kibiashara" alisema mteja
wa benki hiyo Enock Mwakipesile.
Hata ivyo benki iyo imekuwa ikitoa semina mbalimbali kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa katika sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment