Pichani ni Meneja wa NMB kanda ya ziwa, Abraham Augustino akiongea katika mkutano wa klabu ya biashara uliofanyika jijini Mwanza wiki iliyopita. Zaidi ya wateja 300 walihudhuria mkutano huo ambapo pamija na mambo mengine walipata mafunzo ya jinisi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Katika kuhakikisha kuwa NMB inahudumia makundi mbalimbali ya wateja wake kulingana na mahitaji yao ya kifedha, wiki iliyopita, benki iliendesha mkutano wa Klabu ya Biashara uliowakutanisha pamoja zaidi ya wateja 300 wanaohudumiwa na matawi ya NMB ya jijini Mwanza. Baadhi ya faida zilizopatikana katika mkutano huo ni pamoja na mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kutunza daftari la biashara na njia mbalimbali za kuboresha biashara. |
No comments:
Post a Comment