Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo mapema leo asubuhi katika ofisi za SBL zilizopo Temeke jijini Dar es salaam. |
Huu ni mwaka wa sita mfululizo ambapo SBL inatoa msaada kwa wanafunzi wa ndani wanaochukua kozi za shahada katika vyuo vikuu vya Tanzania chini ya programu ya kampuni ijulikanayo kama “Skills for Life”. Jumla ya wanafunzi 31wa Tanzania tayari wameshanufaika na mpango huu ambao ni sehemu ya Mfuko wa Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL Foundation).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha fomu za maombi kwa ajili ya udhamini zinapatikana katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza au kupitia tovuti ya www.eablfoundation.com.
Wanyancha amesema mpango huo uko wazi kwa wanafunzi kutoka nchi nzima ya Tanzania ambao ambao tayari wamepata usajili wa kujiunga na vyuo vikuu nchini katika fani za Biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Uhandisi na Sayansi ya Chakula katika ngazi ya shahada kutoka vyuo vikuu hapa nchini.
Mfuko wa EABL ulianza kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi kuanzia wanaojiunga na vyuo vikuu mwaka 2005 ambapo hadi sasa zaidi ya wanafunzi 238 wamenufaika kwa mpango huo wakiwemo 31 kutoka Tanzania. Wengi walionufaika tayari walishamaliza masomo yao na wanafanyakazi katika makampuni mbalimbali katika ukanda huo. Mpango huu upo katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mfuko wa EABL umetumia jumla ya zaidi ya Tshs billion 5 kuugharamia tangu mwaka wa 2005.
Udhamini huu hugharamia ada ya masomo, vitabu, malazi, fedha za kujikimu na programu za ushauri kwa waombaji watakaofanikiwa.
“Lengo letu kuu kupitia mpango huu ni kuwawezesha waombaji kutimiza ndoto zao maisha,” alisema Wanyancha na kuongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Septemba 20, 2016.
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini kuchangamkia fursa hiyo ili kwa kutuma maombi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ujao.
MAHITAJI MUHIMU: Fomu za maombi zilizojazwa vizuri zikiwa zimeambatanishwa na barua ya usajili kutoka kwa taasisi ya elimu ya juu, udhibitisho wa hitaji la kifedha na nakala za vyeti vya elimu ya sekondari kidato cha nne na cha sita.
ni mkakati mzuri, kusaidia wanafunzi wenye wazingira magumu kiuchumi kutimiza malengo yao kimasomo, lakini idadi ya wanufaika 31 kwa kipindi cha takribani miaka kumi na hivyo kuwa na wastani wa wanufaika 3 kwa mwaka!nadhani kasi ya mkakati huu hauendani na huitaji katika jamii. Natambua uwepo wa bodi ya mikopo wa elimu ya juu, lakini wastani mkubwa kidogo, mfano wa wanufaika 10-15, ingekua na mvuto Zaidi.
ReplyDelete