Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 15 June 2016

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAZINDUA KITOVU CHA MJI WA KISASA WA SAFARICITY JIJINI ARUSHA

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa #SafariCity Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Felix Daudi Ntibenda akipanda mti pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa mji wa #SafariCity
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limezindua rasmi mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa SafariCity, jijini Arusha, 11 Juni, 2016. SafariCity, mradi wenye ukubwa wa ekari 559.4 ni sehemu ya mji iliyopangiliwa kitaalamu na kuzingatia sheria za mipango miji. Mji huu upo katika kitongoji cha Mateves, km 3 kutoka uwanja wa ndege wa Arusha, km 15 kutoka Arusha mjini na km 50 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.

Mradi wa SafariCity unatoa fursa kwa makundi mbalimbali ya wawekezaji wanunuzi wenye mahitaji tofauti ya uendelezaji wa nyumba za makazi kwa vipato tofauti (Chini, kati na juu), majengo ya ofisi na biashara, maduka makubwa (Shoping Mmall), pamoja na madogo, maeneo ya biashara, maendeleo ya viwanda vidogo vidogo burudani na utalii, hospitali, uwanda wa elimu, huduma za jamii kama vile Kituo cha Polisi na Zimamoto pamoja na uhifadhi wa maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo mbalimbali na mapumziko. Mazingira bora ya mji huu yanaufanya kuwa mojawapo ya miji yenye mvuto wa asili.

Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa SafariCity, Shirika la Nyumba la Taifa linatoa fursa kwa wawekezaji (watu binafsi, taasisi, pamoja au waendelezaji) kuwasiliana nasi ili waweze kupata maelezo ya jinsi ya kuweza kushiriki katika uwekezajinunua viwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi za gharama nafuu na gharama za kati.

Wawekezaji wanapewa fursa ya kuwekeza nunua kwenye mji viwanja vilivyuliopangwa uvikiwa na huduma muhimu kama vile miundo mbinu ya maji, barabara na umeme ili kuboresha upatikanaji wa makazi bora nchini. Uzinduzi wa utekelezaji wa mradi huu unaenda sambamba na utekelezaji wa mradi wa nyumba za mfano zitakazojengwa na Shirika ilikuleta chachu katika mji mzuri wa SafariCity.

Viwanja vinavyopatika kwenye awamu hii ni takribani viwanja 600 vinavyouzwa kuanzia Shilingi million 7 na kuendelea. Ili kupata fursa hii, jaza fomu ya maombi inayopatikana katika ofisi za makao makuu ya Shirika la Nyumba ama ofisi yoyote ya mkoa ya Shirika la Nyumba.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0687 444 333 au 022 216 2800 au tembelea tovuti ya www.thesafaricity.com

No comments:

Post a Comment