Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 18 February 2016

WATEJA WA TIGO, AZAMTV NA LIGABBVA KWENDA KUANGALIA MECHI YA BARCELONA BURE

Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya kujishindia safari ya kwenda kushuhudiamechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu . Katikati yake ni Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta.Kulia kwake Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam TV, Mgope Kiwanga .Promosheni hiyo ya ushirikiano wa Tigo Pesa na Azam TV, inaanza rasmi leo hadi Machi 13 na washindi wawili watakwenda Hispania.

Dar es Salaam, Februari 17 2016: Tigo, Azam Media na LigaBBVA leo wametangaza ushirikiano baina yao ambao utawapa fursa watumiaji wa huduma Tigo Pesa wanaonunua vifurushi vya michezo vya AzamTV kupata nafasi ya kusafiri bure bila malipo kwenda kutazama mechi ya ligi kuu kati ya miamba wawili wa Hispania – Barcelon na Deportivo la Coruna – itakayofanyika Aprili mwaka huu.

Akiongea katika uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema, “Kwa kufahamu mapenzi makubwa waliyonayo watanzania kwa mpira wa miguu hasa ligi kuu ya Hispania, Tigo imeungana na Azamtv na LigaBBVA ili kuwapa watanzania, hususan wateja wa Tigo Pesa fursa hii adimu na bure ya kusafiri na kwenda kutazama mechi kati ya Barcelona and Deportivo la Coruna itakayochezwa Aprili 17.”

Rutta alisema: “Mtumiaji wa Tigo Pesa anachohitaji kufanya kushinda fursa hii ni kuhakikisha kimoja kati ya vifurishi vikuu vya AzamTV kipo hewani (Pure, Plus, Play) na hapo atakuwa ameingia katika droo ya kumpata mshindi wa kwenda kushuhudia mechi hii ya kusisimua. Tunapenda kuwahimiza wateja wa Tigo watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kuchangamkia fursa hii ya kusafiri bila malipo kwenda Hispania.”

Tigo, kwa mujibu wa Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa huyo, ina zaidi ya wateja milioni tano waliojisali katika huduma ya Tigo Pesa waliopo kila kona nchini Tanzania.

Akiongea katika uzinduzi huo. Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Rhys Torrington alisema, “Kama kawaida yetu, malengo yetu daima ni kuwapa kilicho bora zaidi wateja. Nchini Tanzania tunafahamu ni jinsi gani watu wanavyopumua, kula na kuishi mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. Hii ni sababu iliyotupa msukumo wa kuleta LigaBBVA ambayo ni mojawapo katika ligi bora duniani kwa mashabiki wengi Tanzania ili kukata kiu yao ya mpira wa miguu. Alisema “nafasi kama hizi hazijitokezi kila mara kushuhudia maajabu ya Messi, Neymar na Suarez yakitokea”.

Tunapenda kuwahimiza mashabiki wote wa mpira wa miguu nchini Tanzania kutumia fursa ya kipekee kutimiza kutumiza ndoto zao katika maisha.” Mbali na washinfi wawili watakaosafiri kwenda nchini Hispania katika kipindi cha promosheni hii, aidha zitatolewa zawadi mbalimbali kwa washindi zikiwemo jezi asili za timu ya Barcelona, mipira ya miguu, mipira, tisheti, kalamu, miwani ya jua na zawadi nyinginezo. Ili kushinda zawadi. watazamaji wa mechi za LigaBBVA kupitia AzamTV watahitajika kupiga simu kabla ya mechi kuanza na wakati wa mapumziko na kujibu maswali yatakaokuwa yanaulizwa.

Torrington alisisitiza “ LigaBBVA ambao tunashirikiana nao, wamefurahishwa na mapokezi mazuri ya watanzania kwa ligi ya ligi ya Uhispania kuanzia siku ya kwanza, na katika kuunga mkono promosheni hii wametukabidhi vifaa vyenye nembo ya LigaBBVA vitakavyotolewa kwa kwa washindi wa kila wiki na tunaamini huu ni mwanzo wa mambo makubwa yajayo.”

No comments:

Post a Comment