Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 26 August 2015

WANAWAKE WAKIAFRIKA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA

Rubani Anne-Marie Lewis ni mwanamke wa kwanza kuongoza ndege aina ya Airbus A380 inayomilikiwa na kampuni la fastjet Tanzania.
Pamoja na kwamba uwepo wa wanawake katika sekta ya usafiri wa anga bado ni mdogo, uwezo wa kuwa viongozi katika usafiri wa anga hauna mwiko. Wanawake barani Afrika hawapaswi kuogopa kuwa sehemu ya sekta hii inayokua barani kote. Hayo ni maneno kutoka kwa rubani mwanamke wa kwanza kuongoza ndege aina ya Airbus A380 inayomilikiwa na kampuni la fastjet Tanzania, rubani Anne-Marie Lewis, ambaye huongoza ndege hii ya Airbus katika mikoa ya Tanzania na nchi nyingine za jirani.

Wanawake wanapaswa kuelewa kwamba hakuna aina ya kazi ambayo ipo kwa ajili ya wanaume peke yao, bali wanawake wataleta kwenye sekta ya usafiri wa anga uwezo wao wa kufanya kazi kwa bidii, kulea na ujuzi wao wa usimamizi bora. Alisema hayo wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wetu.

Kwa mujibu wa Bi Lewis, wanawake wa Afrika wanahitaji kuelewa kwamba nia na uamuzi wao utaondoa hofu au hasara ya kiuchumi. Uwezo wao wa kufanya kitu chochote, ambapo wataweka mawazo yao juu ya kile wanachotaka kukifanya utakuwa ndio msukumo wa malengo yao.

Alibainisha kuwa kwa upande wake, yeye alianzia chini kabisa lakini nia yake ya kuingia, kwenye hii fani iliyokuwa imetawaliwa na wanaume na kwa msaada wa mara kwa mara kutoka kwa baba yake ulikuwa ndio msingi wa mafanikio anayoyapata mpaka sasa.

Wakati vijana wengi barani Afrika, wanaweza kufikiri kwamba wao ni kundi lisilokuwa na faida, lakini wanapaswa kufurahi kwasababu wako katika maisha ya kisasa ya kompyuta na intaneti, ambayo wanaweza kutumia kujifunza juu ya kitu chochote wanachotaka. aligusia.

Rubani Lewis aliongeza kwa kusema kwamba Watu kutoka kwenye hali ya uchumi wa chini na wanawake, siku zote wanakumbwa na changamoto nyingi wakati wa kusoma au kazini, kwani mara nyingi imekuwa ikidhaniwa kwamba msingi wa sababu hizo, ni kwamba kwa namna fulani hawataweza kushindana, ingawa muda na wakati tena imethibitika kuwa ni hadithi tu.

Wanawake wanatakiwa wawe wao kama wao ili kufanikiwa, wanaleta sifa za kipekee katika nafasi yoyote, kwani wao ni wasikivu wazuri, Walezi na wana ujuzi mkubwa wa kupangilia mambo, alisema huku akiongezea kwamba nia, msukumo na shauku daima hutoa kilicho bora, na ni msingi wa mafanikio yake.

Kwa upande mwingine, Bi Lewis anatoa pongezi kwa baba yake, kama baba wa mabinti watano, baba yangu alijua alipaswa kuongoza kwa mfano, kutuonyesha sisi kwamba ili kufanikiwa itahitaji kufanya kazi kwa bidii na nia, alibainisha.

Aliongeza kuwa Baba yao alisisitiza kwa wasichana wote juu ya umuhimu wa elimu na kwamba itakuwa si, tu kuwa sababu ya kuamka kitandani kila siku, lakini pia ni njia ya kuwa huru kiuchumi, huku pia akipandikiza kwao kwamba jinsia haina maana yoyote katika uchaguzi wa taaluma.

Wanawake wa Afrika wanao uwezo wa kufanya kazi katika eneo lolote la sekta ya anga. Kama mimi nilivyo rubani, napenda kuona marubani wanawake zaidi barani Afrika, ambapo itasababisha wao kuwa marubani wanaotoa mafunzo kwa marubani wanaowasimamia. Wataleta mabadiliko katika sekta za anga katika bara la Afrika sawa na wale wanawake wa magharibi walioleta mabadiliko katika sekta za anga katika bara lao, alihitimisha.

No comments:

Post a Comment