Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Finca, Edward Greenwood akizungumza mara baada ya kufuturu mwishoni mwa wiki baada ya kujua umuhimu wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani na kufuturu na waislamu waliofunga. |
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza mara baada ya kufuturu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Finca, Edward Greenwood akizungumza na Sheikh wa Mkoawa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum wakati wakifuturu mwishoni mwa wiki.
|
Baadhi wa waumini wa dini ya Kiislam wakifuturu katika mwenzi Mtukufu wa Ramadhani jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki. |
Akizungumza baada ya kufuturu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Finca, Edward Greenwood amesema wanatambua umuhimu katika mwezi huu kuwa wanawajibu kufuturu na watu ili waendelee kupata baraka ya kuendelea kukua kwa benki hiyo.
Amesema kama benki itaendelea kutoa huduma kwani imekuwa ikikua kwa kasi tangu kuanza kama taasisi ya mikopo na kuweza kufikia benki ni kutokana na jamii kutambua mchango wake ambapo imetimiza miaka 18 tangu ilipoanzishwa mwaka 1998.
“Mafanikio haya ya Finca ni kutokana na mchango wenu, maoni na ushirikiano wenu bila hivyo tusingeweza kufika hapa tulipo” alisema Greenwood.
Nae Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum alisema benki imetambua umuhimu katika mwezi mtukufu kwa kutoa sehemu ya kufuturisha kwa kile wanachokipata.
Benki ya Finca ya watu inayosikilizana kumdhamini kila mtanzania, tunawaahidi kuendelea kutoa huduma bora.
No comments:
Post a Comment