Akizungumza kituoni hapo Meneja wa benki hiyo wa tawi la Nyerere, Nuru Mwangulangu, ambaye aliongoza wafanyakazi wenzake waliofika kituoni hapo alisema wamefanya hivyo kama sehemu ya utaratibu wao wa kuchangia makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii hususani watoto ambao ndio tunaamini wanapaswa kuandaliwa vizuri na kupata mahitaji muhimu na haki wanazostahili kwa kuwa ndio taifa la kesho.
“CBA leo tumekuja kuwaona vijana, kufurahi nao, na kuwapatia zawadi ili kuwawezesha kufurahia sikukuu ya Pasaka kama watoto wengine waliopo majumbani. Watoto kama hawa wanahitaji upendo, faraja na kupatiwa misaada mbalimbali ya kuwawezesha kujisikia kuwa nao ni sehemu ya jamii na kusaidia jamii ni sehemu ya sera yetu ndio maana tumekuwa tukisaidia jamii katika Nyanja mbalimbali hususani elimu na afya”, alisema Mwangulangu.
Pia alisema kufika kwao wameweza kuangalia mazingira, kufahamu changamoto zinazowakabili walezi wa kituo hicho na kuona wapi benki inaweza kusaidia katika siku za usoni na aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia kutoa msaada na kutumia muda wao kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo hicho, Sista Ana Marandu, aliwashukuru wafanyanyakazi wa benki hiyo kwa kutoa msaada wa chakula , nguo,kuwafungia watoto michezo ya burudani na kutumia muda wao kucheza nao. “Tunatoa shukrani kwa upendo mkubwa mlioonyesha siku hii ya leo na tunawaomba siku zote mtupe ushirikiano kama huu”, alisema Sista Marandu.
Global Publishers
No comments:
Post a Comment