Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 17 April 2015

BAYPORT FINANCIAL SERVICES YAZIDI KUCHANJA MBUGA, YAZINDUA TAWI LA 80 WILAYANI ILEJE, MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Rosemary Senyamule (kulia), akionyeshwa nyaraka za ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, inayojihusisha na mambo ya mikopo katika uzinduzi wa taasisi hiyo katika wilaya hiyo ya Ileje, mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Alpha Akim. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wilayani humo.
Wageni mbalimbali wakiangalia shughuli za uzinduzi wa tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Senyamule.
Baadhi ya wageni waalikwa wakisoma vipeperushi vya taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Bayport Financial Services, Alpha Akim, akizungumza jambo katika uzinduzi wa tawi lao la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo kwa watumishi wa wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, mwishoni mwa wiki ilizindua tawi lake jipya la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, huku Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Staki Senyamule, akiwataka wananchi wake kukopa kwa sababu maalum.

Kufunguliwa kwa tawi hilo kutainua uchumi wa wananchi wa Ileje watakaotumia fursa ya uwapo wa ofisi hiyo, bali pia kutarahisisha utoaji wa huduma wa taasisi hiyo ya Bayport nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo jipya, Mkuu huyo wa wilaya Ileje, Rosemary alisema kuwa wananchi wakiitumia fursa ya tawi hilo kutainua pia kiwango cha uchumi cha watu wake.

Alisema suala la mikopo ni jambo jema kutokana na uwezo mzuri unaoweza kuwaendeleza wananchi, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zote zilizoidhinishwa, ambao kimsingi ni watu wanaotakiwa kuendelezwa kwa mambo mengi.

No comments:

Post a Comment