Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi (wa kwanza kushoto) akitamtambulisha, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi, Mhe. Angela Kairuki (wa pili kushoto) kwa Balozi wa Finland nchini, Sinikka Antila (wa kwanza kulia) wakati wa kufunga mkutano wa siku mbili wa viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika Mashariki uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050. Wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu “Uongozi Instutite”, Prof. Joseph Semboja. Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam, Februari 22, 2015: Mkutano wa kikanda juu ya ukuaji
na maisha ya baadae ya miji ya Afrika mashariki ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi
wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) umefungwa rasmi na Naibu
waziri wa Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Angela Kairuki katika Hoteli ya Hyatt Regency
jijini Dar es salaam.
Mkutano huo wa siku mbili
uliohudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda
na kimataifa, miji mikubwa, wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia umeweza kujadili
na kuainisha mipango kabambe katika kutatua changamoto mbalimbali za ukuaji wa miji
na jinsi gani tungependa kuishi mwaka 2050.
Aliongeza kuwa matatizo
ya foleni na kubanana kwa makazi ni kutokana na mipangilio mibovu ya nyumba na makazi
jijini Dar es salaam. Hivyo basi kwa kutatua changamoto hizi wakazi wa Dar na wa
miji mbalimbali ya Afrika kwa ujumla wataweza kufurahia mahitaji yao muhimu na kuongeza
kasi ya maendeleo.
Mhe. Kairuki pia aliweza
kutambua mchango mkubwa wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu
(UONGOZI INSTITUTE) kwa kuleta mijadala yenye tija yenye lengo ya kustawisha uongozi
bora na maendeleo kwa nchi za Afrika na dunia kwa ujumla.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu
wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja aliwashukuru watoa mada na washiriki
wote walioweza kufika na kuhakikisha kuwa mkutano huu unafana.
“Lengo kuu la mkutano huu
limekuwa ni kujadili juu ya ukuaji na maisha
ya baadae ya miji ya Afrika na tumekubaliana wote kuwa ili haya yaweze kutimia ni
lazima basi miji iongeze nguvu ya ukuaji wa uchumi ili kuongeza
ajira iliyawezekudumukwamudamrefu, lakini pia kufikia maono na malengo haya
basi ni lazima kuwe na utawala bora na tumeainisha mabadiliko ya kifikra na maridhiano
katika kutekeleza majukumu haya”.
Washiriki wa kongamano hilo
wametoka nchi mbalimbali ikiwemo Burundi, Ethiopia, South Afrika, Sudan, Kenya,
Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na
Uganda.
Kwa maelezo zaidi wasilianana:
Mr. AmaniNkurlu,
AfisaMawasiliano , UONGOZI Institute
Simu: +255 22
2602917, +255 0712 223 839
Baruapepe: ankurlu@uongozi.or.tz
|
Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Tuesday, 24 February 2015
MHESHIMIWA ANGELA KAIRUKI AHITIMISHA RASMI MKUTANO WA KIKANDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment