Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 17 November 2014

MAONYESHO YA WADAU WA GESI NA OIL YAFANA MKOANI MTWARA

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Stanbic, Ijumaa, wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya wadau wa Gesi na Oil yaliyofanyika mkoani Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Wilman Ndile akizungumza na Ofisa wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, Francis Kihinga wakati walipokutana kwenye mkutano wa wadau wa gesi uliofanyika mkoani Mtwara, TSN ni moja kati ya wadhamini wa mkutano huo.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya bidhaa za wadau mbalimbali wa madini yaliyofanyika sambamba na mkutano huo. Maonesho hayo yalifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Veta Mtwara wakati Mkutano wa wadau ulifanyika katika hoteli ya Naf. 

Afisa Matekelezi wa NSSF mkoani Mtwara, Jamila Mfanga, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile vipeperushi vya bidhaa zake.

Picha na wadau.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiangalia bango la mafunzo ya Chuo Kikuu Huria ambao walifungua chuo chao mkoani humo, nao walikuwa ni baadhi ya waliojitokeza kwenye maonyesho hayo pia pembeni yake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Tolly Mbwete.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiwaonyesha baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano wa kujadilia masuala ya gesi na Mafuta uliofanyika mkoani Mtwara, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye, pembeni Mwenyekito wa Bodi ya Ushauri wa Madini, Richard Kasesela.

Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment