Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Monday, 20 April 2026

BENKI YA EQUITY TANZANIA YAZINDUA TAWI JIPYA UBUNGO, NDANI YA EACLC MALL DAR ES SALAAM

Benki ya Equity Tanzania imezindua rasmi tawi jipya la Ubungo lililopo ndani ya East African Commercial Logistics Centre (EACLC Mall), ghorofa ya kwanza, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma za kifedha karibu na wateja na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa Ubungo na maeneo jirani.

Tawi hili jipya linatoa huduma kamili za kibenki, ikiwemo kufungua akaunti, utoaji wa mikopo, kuweka na kutoa fedha, huduma za fedha za kimataifa (money transfer), huduma za biashara, pamoja na usaidizi kwa wateja. Kupitia hatua hii, Equity Tanzania inaendelea kuimarisha mtandao wake wa matawi nchini ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Bi. Isabela Maganga, alisema kuwa kufunguliwa kwa tawi la Ubungo—ambalo ni tawi la kibiashara—ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa benki hiyo wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kifedha karibu na maeneo wanayoishi na kufanyia shughuli zao za kiuchumi.

Tunendelea kuwekeza katika miundombinu ya matawi pamoja na teknolojia ili kuhakikisha huduma zetu zinawafikia Watanzania wengi zaidi, hasa waliopo katika maeneo yenye shughuli nyingi za kiuchumi. Ubungo ni kitovu muhimu cha biashara na usafiri, hivyo tawi hili litachochea ukuaji wa shughuli za kifedha kwa wafanyabiashara na wakazi wa eneo hili,” alisema Bi. Maganga.

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kuwekeza katika sekta za kimkakati zikiwemo biashara, kilimo, elimu na afya, kwa kutoa mikopo nafuu na huduma bunifu zitakazochochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kwa sasa, tawi hili linakuwa sehemu ya mtandao wa matawi 19 ya Benki ya Equity Tanzania yaliyopo nchini, yanayoendelea kutoa huduma kwa wateja katika mikoa mbalimbali.

Uzinduzi wa tawi hili unaashiria dhamira ya benki hiyo ya kuimarisha ujumuishaji wa kifedha (financial inclusion) na kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.







No comments:

Post a Comment