Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 15 October 2025

AIRTEL MONEY YAUNGANA NA COPRA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFEDHA KIDIJITALI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Dar es Salaam, Tanzania – Airtel Money Tanzania imefanya mazungumzo ya kimkakati na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), yenye lengo la kuimarisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali katika sekta ya kilimo.

Mazungumzo hayo yanalenga kuchochea fursa za ushirikiano zitakazowezesha kuimarisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali nchini, hususan katika sekta ya kilimo biashara.

Kupitia mpango huu, wadau wa sekta ya kilimo — wakiwemo wakulima, wauzaji na wasindikaji — watawezeshwa kufanya malipo, kuweka akiba, na kupata huduma muhimu za kifedha kupitia majukwaa ya kidijitali kama Airtel Money.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi endelevu za kukuza ujumuishi wa kifedha, kuongeza ufanisi katika minyororo ya thamani, na kuimarisha ushiriki wa wakulima katika mifumo rasmi ya uchumi.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Bw. Andrew Rugambo, alisema:

Airtel Money inaamini kuwa teknolojia ya kifedha ni chachu ya mabadiliko katika sekta ya kilimo. Kupitia ushirikiano huu na COPRA, tunalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma bora za kifedha kwa urahisi zaidi, kuongeza uwazi katika malipo, na kukuza uchumi wa wakulima kupitia mifumo ya kidijitali,” alisema Bw. Rugambo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene Madeje Mlola, alisema kuwa ushirikiano huo utarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wakulima na wadau wa sekta hiyo.

Ushirikiano huu utasaidia kuongeza ufanisi katika minyororo ya thamani ya mazao, kurahisisha malipo, kuhakikisha usalama wa fedha za wakulima, na kuimarisha ushiriki wao katika mifumo rasmi ya kifedha,” alisema Bi. Mlola.

 



No comments:

Post a Comment