Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 19 June 2025

PUMA ENERGY YASHIRIKI KONGAMANO KUKUZA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA SEKTA YA MADINI

Mwanza, Juni 18, 2025 – Kampuni ya Puma Energy Tanzania imedhihirisha dhamira yake thabiti ya kuiunga mkono sekta ya madini nchini kwa kushiriki kikamilifu katika kongamano la kitaifa la siku tatu lililoandaliwa na Wizara ya Madini. Tukio hilo muhimu limefanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort, jijini Mwanza, likiwa na lengo kuu la kuongeza ushiriki wa Watanzania katika mnyororo wa thamani wa madini.

Kongamano hili limewakutanisha wadau kutoka serikalini, sekta binafsi, na mashirika ya kiraia kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuongeza ushirikishwaji wa Watanzania katika shughuli za madini. Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, aliyeambatana na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo.

Katika ziara yao ya kutembelea mabanda ya washiriki, viongozi hao walifika kwenye banda la Puma Energy Tanzania na kupokelewa na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. Prosper Kasengela, ambaye alitoa maelezo ya kina kuhusu mchango wa Puma Energy katika kuiwezesha sekta ya madini kupitia huduma bora za nishati.

Dhamira ya Kuendeleza Ushirikiano wa Kimkakati

Kupitia ushiriki wake katika kongamano hilo, Puma Energy Tanzania imesisitiza kwamba itaendelea kushirikiana na wachimbaji wakubwa na wadogo nchini kwa kuwapatia suluhisho endelevu za nishati, ili kuongeza tija, usalama na ufanisi katika shughuli za uchimbaji madini.

Mbali na sekta ya madini, kampuni hiyo ina mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya sekta nyingine ikiwemo usafirishaji, ujenzi na usafiri wa anga, kwa kuhakikisha upatikanaji wa nishati salama, bora na ya uhakika.

Kutambuliwa kwa Mchango Wake

Katika kilele cha kongamano hilo, Puma Energy Tanzania ilitunukiwa tuzo maalum kama ishara ya kutambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika kuunga mkono mafanikio ya kongamano pamoja na maendeleo ya sekta ya madini kwa ujumla.

Kwa ujumla, ushiriki wa Puma Energy Tanzania katika kongamano hili umeonesha kwa vitendo dhamira ya kampuni hiyo ya kuwa mdau hai wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment