Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 18 April 2024

KAMPUNI YA SUKARI YA KILOMBERO YATOA MSAADA WILAYA YA KILOMBERO


Morogoro-Kilombero, 17 Aprili 2024; Kampuni ya sukari ya kilombero imetangaza ushiriki wake katika kutoa msaada wa kibinadamu kwa jamii inayoishi wilaya ya Kilombero, ambayo imeathiriwa vibaya na matukio ya mafuriko yanayoendelea nchini kote yaliyo sababishwa na mvua kubwa.


Hafla hii ya utoaji msaada imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, ambapo kampuni imetoa mchango wa tani sita za mahitaji muhimu ya chakula, ikiwa ni pamoja na maharage, unga wa mahindi, na mchele. Mchango huu unatarajiwa kusaidia zaidi ya kaya 500 zilizoathiriwa na mafuriko.


Wakati wa kukabidhi mchango huo, wenye thamani ya Shilingi za Tanzania milioni 15, Bwana Victor Byemelwa, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano na Wadau wa Kampuni ya Kilombero Sugar, Amesema msaada huo ni sehemu ya Programu ya Misaada ya Maafa ya kampuni. "Kilombero Sugar inaahidi kujali ustawi wa jamii yetu. Mchango wa leo unadhihirisha utayari na uadilifu wetu kwa jamii tunayoihudumia. Tumetoa msaada kwa zaidi ya familia 500, Kwa kulenga mahitaji yanayohitajika kwa haraka zaidi.


Zaidi ya hayo, Bwana Byemelwa amewahimiza wadau wengine kuunga juhudi za serikali za kusaidia jamii zilizoathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni,Pia amesisitiza umuhimu wa hatua za pamoja dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ikithibitisha tena dhamira ya Kampuni ya Kilombero Sugar kwa uhifadhi wa mazingira.

Mheshimiwa Bwn. Dunstan Kyobya, Ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, amekiri umuhimu wa kupata msaada huo kwa wakati: Amesema "Jamii yetu imeathirika sana na mvua inayoendelea, hivyo michango iliyotolewa na hawa ndugu zetu Kilombero sugar tunaithamini sana." Ameongeza kuwa msaada huu unatokana na ushirikiano thabiti kati ya serikali na sekta binafsi katika kushughulikia masuala muhimu.

Bwn. Kyobya amefichua kuwa idadi ya kaya zilizoathiriwa na mafuriko inafikia 1,500, ambapo ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imeathirika hasa maeneo ya Utengule na Masagati. Amesisitiza dharura ya msaada wakati juhudi zinaendelea kurejesha miundombinu katika hali yake kabla ya maafa.

Bwana Hassan Abdallah, ambaye ni mkazi wa eneo la Msagati pia muathirika wa tukio hilo amesema kuwa. "Mafuriko yaliharibu kila kitu, yakiiacha familia yangu na mimi bila makazi. Tumepokea msaada kutoka kwa serikali na mashirika kama vile Kilombero Sugar, Kwakweli msaada huu umetusaidia kupunguza mateso tuyayopitia katika kipindi kigumu.

Kilombero Sugar Company Ltd imeendeleza ahadi yake kwa jamii kwa kutenga rasilimali kwa Programu yake ya Misaada ya Maafa, ili kupunguza athari za maafa ambayo yanaweza kuathiri maeneo inayohudumia.

Kwa Mawasiliano:

Bwn. Victor Byemelwa
Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano na Wadau
Kilombero Sugar Company Limited
Barua pepe: Vbyemelwa@illovo.co.tz

No comments:

Post a Comment