Picha ya pamoja.
- Wateja kujishindia ofa na punguzo la bei wanapolipa kwa M-Pesa kwenye maduka yaliyolengwa katika msimu huu wa Wapendanao.
10 Februari 2021, Dar es salaam - Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali Vodacom Tanzania Plc leo imezindua kampeni ya 'Lipa Kwa Simu katika mwezi wa Wapendanao’ – itakayowazawadia wateja pindi wanapofanya malipo kwa kutumia simu zao za mkononi katika maduka ya Hope Holding.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd, Epimack Mbeteni alisema kampeni hiyo mpya ni sehemu ya juhudi za Vodacom kuhamasisha wateja kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali.
"Wateja sasa wanaweza kufurahia usalama na urahisi wa kufanya malipo ya kidijitali ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vitu katika maduka ya Hope Holding, ambapo watapata ofa na punguzo la bei la papo hapo la asilimia 10 pindi wanapofanya malipo kupitia M-Pesa katika kipindi hiki cha msimu wa Wapendanao,” alisema Mbeteni. "Tukiwa ni kampuni inayoamini katika nguvu ya teknolojia, tunatamani kuhakikisha teknolojia bora zinaibuka katika soko na kutoa huduma huku tukibuni bidhaa mbalimbali kwa wateja wetu, ambapo “Lipa Kwa Simu" ni hatua inayohakikisha usalama wa malipo pamoja na kurahisisha maisha,” aliongeza Mbeteni.
Kampeni ya Lipa kwa Simu ya msimu huu wa Wapendanao inajumuisha maduka yaliyo chini ya Hope Holding ambayo ni Red Tag, Sketchers, Bottega verde, Flormar, mgahawa wa PapaRotti na mazulia ya Amal ambapo wateja watapata ofa mbalimbali kama vile punguzo la asilimia 50 ya bei kutoka Bottega Verde, kupata zawadi ya wapendanao kutoka maduka ya Vipodozi vya Flormar ikiwa watanunua bidhaa mbili, na watapata viatu vya bure kutoka duka Skechers ikiwa watanunua jozi mbili na kisha kufanya malipo kupitia simu zao za mkononi.
"Ninawahimiza wateja wote kutumia fursa hii na kufanya malipo kupitia M-Pesa ili kufurahia usalama, utulivu na urahisi wa malipo ya kidijitali kupitia simu zao za mkononi huku wakipata thamani zaidi wakati huu wa mwezi wa Wapendanao. Kampeni hii inaanza leo tarehe 10 Februari mpaka tarehe 10 Machi 2021," alisema Mbeteni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Hope Holding, Jamal Omar alitoa wito kwa wateja kujitokeza kwa wingi kwenye maduka yanayomilikiwa na Hope Holding ili wapate bidhaa mpya kemkem zilizoletwa kwa ajili ya kampeni ya Lipa Kwa Simu katika msimu huu wa Wapendanao.
Kupitia mkakati wake wa kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali Vodacom Tanzania PLC imebuni bidhaa na huduma nyingi kama Lipa Kwa Simu, M-Pesa MasterCard, M-Pawa, M-Koba na nyingine nyingi ikiwa ni kutekeleza mkakati huo na hivyo kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia.
“Tukiwa na wateja zaidi ya milioni 11 pamoja na mfumo bora wa malipo wa M-Pesa, Vodacom iko katika sehemu nzuri ya kuhakikisha wananchi wanahamia katika jamii isiyotumia pesa taslimu kwa kujikita katika malipo kupitia simu za mkononi. Bidhaa yetu ya 'Lipa Kwa Simu' inaruhusu malipo ya uhakika kwenye mitandao na hivyo ni hatua inayorahisisha maisha zaidi”, Epimack alihitimisha.
Kuhusu Vodacom M-Pesa Tanzania
Vodacom M-Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu inayoongoza nchini iliyoanzishwa na Vodacom Tanzania PLC mwaka 2008. Kwa sasa ni moja ya huduma chache duniani zilizopewa tuzo ya ubora ya GSMA na ina wateja zaidi ya milioni 10.1. Kwa kiasi kikubwa M-Pesa imechangia katika kukua kwa huduma za kifedha na shughuli za uchumi nchini. Wateja wanatuma na kuweka pesa kupitia huduma ya M-Pesa kupitia kwa mawakala zaidi ya 106,000 nchini kote. Mfumo wa M-Pesa unaunganisha mabenki, makampuni na mashirika ya Serikali katika kufanya malipo ya kidigitali.
Kwa sasa, M-Pesa inaendelea kuwa kinara katika soko la huduma za kifedha nchini kupitia huduma zake za kibunifu kama vile Akiba na Mikopo, malipo ya kieletroniki, huduma za vikundi na nyingine nyingi ambazo zinakidhi mahitaji ya watanzania na kuwezesha ufikaji na utumiaji Zaidi wa huduma rasmi za kifedha.
|
No comments:
Post a Comment