Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 18 November 2019

WANAFUNZI WAFAIDIKA NA ELIMU YA KUWEKA AKIBA KUPITIA BENKI YA NMB

Katika kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kibenki kwa vitendo.

Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili kufahamu shughuli zao lakini pia walitembelea Tawi la NMB Ohio.

Pamoja na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao kuwekeza nguvu zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti zitakazowawezesha kutunza fedha na kujijengea tabia ya kuweka akiba na kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na Mwanachuo Akaunti.
Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.

Wanafunzi wakifurahi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna na Mwalimu wao, Jennifer Dominick.

Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa ofisa wa benki ya NMB, Monica Job.
Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa ofisa wa benki ya NMB, Subira Kapita.

#NMBKaribuYako

No comments:

Post a Comment