Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Thursday, 28 March 2019

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu katika fani mbalimbali kutoka Serikali ya Thailand. 

Kozi hizo zitakazotolewa kwenye Vyuo mbalimbali nchini humo, zitajikita katika fani za Filosofia ya Uchumi Timilifu; Mabadaliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula; Afya ya Jamii na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Wizara inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hizo za mafunzo zilizotangazwa na Serikali ya Thailand kwa mwaka 2019.

Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 31 Machi 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti  ifuatayo: http://www.tica.thaigov.net


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
27 Machi 2019

No comments:

Post a Comment