Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 10 August 2016

TIGO, KUPATANA.COM KUSHIRIKIANA KUWEZESHA BISHARA KWA MTANDAO

Meneja Miradi ya Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Anthony Njau (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa biashara kati ya Tigo na Kupatana.com. Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao ya Kupatana.com, Philip Ebbersten na Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha.
Mkurugenzi wa Kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao ya Kupatana.com, Philip Ebbersten akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa biashara kati ya Tigo na Kupatana.com. Wengine ni Meneja Miradi ya Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Anthony Njau na mwisho ni Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha.
Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha akifafanua jambo wakati wa mkutano huo mapema leo jijini Dar es salaam.

Wafanyakazi wa tigo wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo na waandishi wa habari katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, Agosti 9, 2016 - Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania na kampuni ya Kupatana.com, moja ya kampuni zinazoongoza Tanzania katika huduma za masoko katika mtandao zimeingia katika ubia wa kibiashara ambapo kila kampuni itauza bidhaa na huduma za kila mmoja katika majukwaa yao ya kidijitali.

Katika hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua maduka matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo kuuza simu zao zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano baina ya pande hizo mbili jijini Dar es Salaam, Meneja miradi ya biashara wa Tigo, Anthony Njau alisema, “tukiwa ni kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba hivi sasa Watanzania wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia njia ya mtandao.”

Njau aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo linabadilisha namna ambavyo watu wanaishi kwa kuwezesha kupatikana kwa huduma na bidhaa katika njia sahihi na rahisi.”

“Lengo la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu jukwaa ambalo wanaweza kupakua vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha na kwa upande wa Tigo kuuza vifaa vipya, kuongeza usambazaji na kuwa na mafanikio katika jaribio hili la msingi, Tigo na Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na kuhakikisha inapatikana kwa urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo ambayo yamesambaa kote nchini,” alisema Njau.

Mkurugenzi wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema kwamba kupitia matumizi ya jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu binafsi) wataweza kuwafikia maelfu ya wanunuzi muhimu kila siku bila kujali maeneo yao ya kijiografia.

Alifafanua kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo ni bure na kuwashauru wateja umuhimu wa kufuata kanuni na miongozo salama kwa bidhaa zote zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa kwa usalama na uelewa zaidi.

No comments:

Post a Comment