Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 30 June 2021

DAVIS & SHIRTLIFF YAPATA CHETI CHA UBORA CHA ISO

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Davis & Shirtliff Tanzania, Benjamin Munyao (Kushoto) akipokea cheti cha Ubora kutoka Shirika la Kimataifa la ISO kutoka kwa Ofisa wa kampuni ya Bureau Veritas, Charles Vunugulu (kulia) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni wasimamizi na wakaguzi, Fausta Kusibago na Lizy Washuka. Cheti cha ISO ni uthibitisho kuwa kampuni imekidhi viwango vya ubora vya kimataifa.

Dar es Salaam. Juni 29,2021 - Kampuni ya Davis & Shirtliff Tanzania, imekabidhiwa cheti cha ISO kutoka Shirika la Kimataifa la Usimamizi wa Viwango (ISO), hatua ambayo ni kubwa kwa kampuni ya kitanzania ambayo imekuwa mstari wa mbele kuboresha maisha ya watu kupitia huduma za maji.

Cheti cha ISO 9001 ni uthibitisho kwamba kampuni imekidhi vigezo vya usimamizi wa ubora kwa mujibu wa mfumo wa usimamizi unaokubalika kimataifa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Davis & Shirtliff Tanzania, Benjamin Munyao alisema “Katika moja ya misingi yetu ‘Core Values’ ni ubora, kwahiyo cheti hiki ni msisitizo wa ubora wa wafanyakazi wetu, vifaa vyetu na utendaji kazi kwamba upo katika viwango vya juu sana.”

CLYDE & CO UPDATER - BANKING IN TANZANIA: POST-LICENSING COMPLIANCE FOR BANKS, FINANCIAL INSTITUTIONS AND MICROFINANCE SERVICE PROVIDERS


In this article, we highlight some of the basic compliance requirements that banks and financial institutions (BFIs) and microfinance service providers (MSPs) in Tanzania must strictly adhere to after receiving their licence to provide banking and financial services.

The Bank of Tanzania (BOT) is the regulatory authority responsible for the licensing of BFIs and MSPs. The BOT’s regulation extends to the conduct of business and operations of BFIs and MSPs.

Governing laws

BFIs are governed by the Banking and Financial Institutions Act No. 5 of 2006 (BAFIA) and subsidiary legislation thereof.

On the other hand, MSPs are governed by the Microfinance Act No. 10 of 2018 (the Microfinance Act) and subsidiary legislation thereof. There are four categories of MSPs:
  • tier 1 – deposit taking microfinance service institutions (DTs);
  • tier 2 – non-deposit taking microfinance service providers (NDTs);
  • tier 3 - savings and credit cooperative societies (SACCOS); and
  • tier 4 - community microfinance groups (CMGs).
According to the Microfinance Act, DTs are regulated by the BAFIA even though they are a category of MSP.

Continue Reading > > >

BENKI YA LETSHEGO YADHAMINI KONGAMANO LA BIASHARA NA UCHUMI JIJINI DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti cha shukrani Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Letshego, Simon Jengo (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Andrew Tarimo (wa pili kulia) kwa udhamini wa Kongamano la Biashara na Uchumi lililofanyika jijini Dodoma hivi karibuni. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mayoda Economic Development Group, Sophia Simbu (kushoto) na Mwenyekiti Mtendaji wa Mayoda, Agustino Matefu.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Letshego, Andrew Tarimo akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Biashara na Uchumi lililofanyika jijini Dodoma hivi karibuni. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Mayoda Economic Development Group kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Meneja wa Uendelezaji Biashara Benki ya Letshego, Ruth Mpangalala (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi (kulia) mara baada ya kufungua Kongamano la Biashara na Uchumi lililofanyika jijini Dodoma hivi karibuni. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Andrew Tarimo.

EMPLOYMENT OPPORTUNITY AT DCB COMMERCIAL BANK

DStv INAKULETEA KATUNI KALI KUPITIA CHANELI ZA WATOTO

 


Si watoto, hata wakubwa wanafurahi na katuni kali kupitia chaneli zetu za watoto.

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako ili wewe na mtoto wako kuweza kufurahia burudani hii.

Na kama hujajiunga na DStv jiunge sasa kwa kupiga 0659 07 07 07.

WASHINDI WA CRDB BANK MARATHON KUZAWADIWA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 45.4

Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB akionyesha bango linaloonyesha zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa washindi wa CRDB Bank Marathon 2021. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EFM, Denis Busulwa (kushoto), Meneja Masoko wa Strategis, Lilian Malakasuka (wapili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha BancAssurance Alliance General, Osward Tellis.

Dar es Salaam 29 Juni, 2021 – Benki ya CRDB imetangaza zawadi za washindi wa msimu wa pili wa CRDB Bank Marathon 2021 ambapo jumla ya shilingi milioni 45.4 zitatolewa kwa washindi 32. Akitangaza zawadi hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa alisema kwa mwaka huu zawadi zimeongezwa ili kuendana na hadhi ya kimataifa ambayo CRDB Bank Marathon ilipewa mwaka huu baada ya kusajiliwa na Chama cha Usajili na Upimaji wa Mbio za Kimataifa (AMIS) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Riadha (World Athletics).

“Mwaka huu sio marathon tu ni ya kimataifa, hata zawadi pia ni za kimataifa zaidi. Tumejipanga kutoa zawadi nono kwa washindi, kwa mbio kubwa za kilometa 42 mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 5, mshindi wa pili shilingi milioni 3, mshindi wa tatu shilingi mili 2 na mshindi wa nne shilingi milioni 1. Hizi ni zawadi kubwa zaidi kupata kutokea katika mbio zote nchini,” alisema Tully huku akibainisha kuwa wingi wa zawadi unatokana na kuongezeka kwa namba ya washiriki ambapo ambapo matarajio ni kupata washiriki 5,000 kutoka ndani nan je ya nchi.


Tully aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujisajili katika mbio hizo za CRDB Bank Marathon kwani pamoja na kuwa mbio hizo sasa hivi ni za kimataifa lengo kubwa ni kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania kwa kuwaleta pamoja kutatua changamoto katika jamii. “Wakimbiaji wengi wa kimataifa wanajisajili ma mia kwa mamia kuja kushiriki kusambaza tabasamu nchini kwetu, lakini tungependa zaidi kuona Watanzania wakishiriki kwa wingi kwani hii ni marathon yetu na tungependa pia kuona zawadi hizi zikibaki nyumbani,” aliongezea.

Akizungumzia fursa zitokanazo na mbio hizo ambazo sasa hivi zimesajiliwa kimataifa, Tully alisema mbio hizo zitakwenda kuchochea uchumi wa Jiji la Dar es Salaam na kulitangaza jiji hilo pamoja na Tanzania kwa ujumla duniani kote. Alisema mbio hizo zitatumika kutangaza vivutio na historia ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo utamaduni wa pwani (swahili culture). “ Pamoja na hivyo mbio hizi pia zitasaidia kuonyesha vipaji vya wakimbiaji duniani kwani mbio hizi zitaonyeshwa live na TVE ambayo ipo DSTV. Tunakwenda kufunguka zaidi kwenye anga za dunia,” alisisitiza Tully.


Akikumbushia lengo la kuandaa marathon hiyo, Tully alisema mbio hizo zinalenga kuwaleta pamoja Watanzania kuchangia watu wenye uhitaji katika jamii pamoja na kutatua changamoto nyengine zinazoikabili jamii. Alisema mwaka huu lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 ambazo zitaelekezwa katika kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ujenzi wa kituo cha mawasiliano “Call Center” katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na kampeni ya utunzaji mazingira ya “Pendezesha Tanzania” ambapo miti milioni 1 inatarajiwa kupandwa ndani ya miaka 3.


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EFM na TVE, Denis Busulwa (Ssebo) alisema kampuni yao inajivunia kuwa washirika wa CRDB Bank Marathon kutokana na mbio hizo kujikita zaidi katika kuhamasisha watu kusaidia jamii. “Tunaishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa mbio hizi zinazowaleta Watanzania kushiriki katika kutatua changamoto katika jamii. EFM na TVE ni vyombo vya habari vya jamii hivyo tunakila sababu ya sisi kushiriki katika mbio hizi ikiwa ni sehemu yetu ya kusaidia jamii,” alisema Ssebo huku akihamasisha Watanzania kujisajili kwa wingi.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikikisho Riadha Tanzania, Jackson Ndaweka aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa mbio hizo kwa viwango vya kimataifa huku akimhakikishia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa kuwa zawadi zote zitabaki nchini kwani wanariadha sasa hivi wanajifua kuelekea tarehe 15 Agosti 2021 siku ya marathon. “Wanariadha wetu wana kiu kubwa ya kushindana baada ya mbio nyingi za kimataifa kuahirishwa kutokana na changamoto ya COVID-19. Zawadi hizi zimekuja wakati muafaka na wanariadha wetu wapo wanajifua kuchuana na wanariadha wa kimataifa,” alisema Ndaweka.


Hafla hiyo ya kutangaza zawadi ilihudhuriwa washirika mbalimbali wa CRDB Bank Marathon ikiwamo kampuni za bima za Sanlam, Alliance (Life na General), Heritage, Mayfair na Britam, pamoja na viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) na klabu za riadha Dar es Salaam. Viongozi hao walipongeza juhudi zinazofanywa na Benki ya CRDB kupitia CRDB Bank Marathon na kuahidi kuendelea kushirikiki katika mbio hizo.

Kujisali na kuchangia katika CRDB Bank Marathon washiriki wanatakiwa kutembelea katika tovuti rasmi yam bio hizo www.crdbbankmarathon.co.tz ambapo mtu binafsi anatakiwa kuchangia shilingi 30,000 na washiriki kupitia vikundi ni shilingi 25,000. Malipo yanaweza kufanyika kupitia matawi ya Benki ya CRDB, CRDB Wakala, SimBanking App, mitandao ya simu na kupitia kadi ambazo zinawawezesha hadi watu wa nje ya nchi kufanya malipo.



 


Tuesday 29 June 2021

WAZIRI DOTTO BITEKO AZINDUA ‘NMB MINING CLUB’

Waziri wa Madini - Dotto Biteko (kushoto) na Afisa Mkuu wa Mikopo Benki ya NMB – Daniel Mbotto wakizindua rasmi jukwaa la ‘NMB Mining Club’ katika hafla ya uzinduzi iliofanyika katika hoteli ya Morena - Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB – Alex Mgeni akiwaelimisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini Kanda ya Kati waliohudhuria uzinduzi wa NMB Mining Club kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki ya NMB.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya Madini kutoka Kanda ya Kati katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa NMB Mining Club uliofanyika Jijini Dodoma.

Benki ya NMB imeendelea kuweka historia nyingine tena kwa kuzindua jukwaa la kwanza nchini mahsusi la kuwahudumia wadau wa Sekta ya Madini liitwalo ‘NMB Mining Club’.

Klabu hiyo mpya imejumuisha zaidi ya wadau wa madini 200 wa Kanda ya Kati na imelenga kutoa mafunzo kuhusu maarifa ya biashara (elimu juu ya mipangilio ya biashara na elimu ya mwendelezo wa kitaalamu wa madini) na fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.

Wadau hao ni pamoja na wamiliki wa migodi, maduka makubwa ya vifaa vya uchimbaji, viongozi kutoka kampuni za madini, Kampuni ya Taifa ya Madini (Stamico), vyama vya wachimbaji wa kada zote na madalali.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jukwaa hilo uliofanyikakatika hoteli ya Morena- Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko aliwapongeza NMB kwa ubunifu huo wa kuwafikia na kuwaunganisha wadau wa Sekta hiyo huku wakiwapa fursa ya mafunzo ya biashara na kubadilishana mawazo kwa ajili ya ufanisi wao binafsi na kisekta kwa ujumla.

Monday 28 June 2021

DStv INAKULETEA BIRIANI ULAYA JUMATATU HII - CROATIA VS SPAIN NA FRANCE VS SWITZERLAND


@geoff_lea anakwambia tofauti ya biriani la Dar es Salaam linaloliwa kila Ijumaa tu #BirianiUlaya ndani ya @dstvtanzania pekee linapatikana kila siku na Jumatatu hii;

⚽️Croatia vs Spain
⚽France vs Switzerland
📺 SS EURO2020, 224

Nani kuibuka Kidedea?

Hakikisha unapiga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema kutazama mtanange huu.

BENKI YA NMB YAZIDI KUWA KARIBU NA WATEJA WAKE - DODOMA, SINGIDA NA MANYARA

Meneja wa NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi akizungumza na wafanyabiashara kutoka Singida, Itigi, Ikungi na Manyoni katika mkutano NMB Business Club uliofanyika Mkoani Singida.
Sehemu ya wafanyabiashara walio hudhuria mkutano wa NMB Business Club uliofanyika Mkoani Singida.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB - Alex Mgeni akizungumza na wafanyabiashara wakubwa wa Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) waliohudhuria jukwaa la NMB Business Executive Network katika hafla iliofanyika katika hoteli ya Morena - Jijini Dodoma.

Benki ya NMB imeendelea kuwa karibu na wateja wake zaidi ya 700 wa mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kupitia jukwaa la ‘NMB Business Club na ‘NMB Executive network’ kwa nyakati tofauti.

NMB imetumia majukwaa hayo kuwakutanisha wateja wao wadogo na wakubwa ili kuwapa elimu ya kuwa wabunifu katika shughuli zao za kujiongezea kipato ili kukuza biashara zao, lakini pia, wametumia fursa hiyo kuweza kupata maoni kutoka kwa wateja wao kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo ikiwa ni moja wapo ya njia ya kuwahusisha wateja wao kuwa sehemu ya ubunifu wa bidhaa zao.

Akizungumza katika NMB Business Club mkoani Singida, Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi aliwahakikishia wafabiashara hao kuwa wapo sehemu salama, kwani NMB iko tayari kukuwa nao katika kila hatua ya shughuli zao. Lakini sio hivyo tu, alibainisha kuwa NMB imeendelea kuwa kinara wa ubunifu wa huduma na bidhaa ili kukidhi matakwa ya wateja wao.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB – Alex Mgeni alisema kuwa, kutokana na kukuwa kwa mtaji, NMB imeendelea kuwa benki inayoongoza kwa faida kwa kupata TZS bilioni 206 baada ya kodi ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 45 (YoY), mwaka 2020. Lakini pia wameruhusiwa na TIRA pamoja na BoT kufanya shughuli za Bima ‘bancassurance’ kwa kushirikiana na makampuni 10 ya bima ambapo huduma inapatikana kupitia matawi yote ya NMB nchi nzima.

Friday 25 June 2021

BOLT - TRANSFORMING LIVES THROUGH RIDE HAILING


“I thank God for enabling me to complete a motorcycle ownership agreement through Bolt. Now I am a proud owner of a motorcycle. Ride hailing has completely transformed my life. In the 4 years I have been working with Bolt, I was able to marry and look after my wife and daughter. I am also blessed to know different parts of Dar es Salaam city and I feel respected.

Ride hailing service is everywhere. Riders have easy access to urban transportation at any time.

I have saved enough money to buy a plot of land and plan to begin building our house. Ride hailing is a fantastic opportunity for youth to get good income and be in control of your working times. I managed to recruit many of my friends who are now benefitting from working with Bolt. I have a lot to thank for and owe it all to Bolt”. – Bolt Driver, Dar es Salaam, Tegeta resident (24) Dizaya Damiano Bugeraha.

BENKI YA CRDB YAZINDUA AKAUNTI YA ‘HODARI’ KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI WAKATI WA UZINDUZI WA MSIMU WA PILI WA KAMPENI YA TUPO MTAANI KWAKO

Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki hiyo, Boma Raballa, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Mashariki, Badru Idd na Maafisa Waandamizi wa Benki ya CRDB wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kampeni ya TUPO MTAANI KWAKO awamu ya pili iliyo boreshwa zaidi ikienda sambamba na Uzinduzi wa Huduma mpya ya HODARI AKAUNTI ambayo ni mahususi kwaajili ya wajisiriamali na wafanya biashara wadogo nchini, ambao wataunganishwa moja kwa moja na huduma ya LIPA HAPA. Uzinduzi huu umefanyika jana kwenye viwanja vya Mbagala Zakiem, Dar es salaam ikiwa ni jitihada za makusudi kabisa za Benki ya CRDB kuhakikisha inalifikia kila kundi kwa kadiri ya mahitaji yake na kuwapa usalama na urahisi katika ufanyaji wa biashara zao.


Benki ya CRDB leo imezindua akaunti ya wajasiriamali iliyopewa jina la “Hodari,” ikiwa na lengo la kuwasaidia wajasiriamali katika sekta mbalimbali nchini kuboresha biashara zao. Uzinduzi wa akaunti hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” inayolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za benki pamoja na kuwapa Watanzania elimu ya fedha na uwekezaji.

Akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile alisema akaunti hiyo ya “Hodari” itakwenda kusaidia kurahisisha biashara za wajasiriamali kwa kuwawezesha kuweka akiba kwa urahisi, kupokea malipo kidijitali kupitia CRDB Lipa Namba na kuunganisha na fursa za uwezeshaji kupitia mikopo ya wajasiriamali.


Bruce alisema pamoja na kuboresha biashara za wajasiriamali, akaunti hiyo pia inakwenda kuleta unafuu mkubwa kwao kwani wateja hawata tozwa makato yoyote kwa miamala ambayo itafanyika ndani ya mtandao wa Benki ya CRDB kuanzia kwenye matawi, CRDB Wakala, ATMs na SimBanking. Alisema akaunti hiyo pia itakuwa ikifunguliwa bure ili kuweza kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi hususani wale wenye mitaji midogo.

Uzinduzi wa akaunti ya “Hodari” unakuja wiki chache baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhimiza taaasisi za fedha kuja na mikakati ya uwezeshaji kwa wajasiriamali ambao wengi wao ni vijana. Bruce anasema uzinduzi wa huduma hiyo ya “Hodari” ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais, huku akibainisha kuwa malengo ya Benki hiyo nikuwafikia wajasiriamali kote nchini.


“Nichukue fursa hii kuwaalika wajasiriamali wote kufungua Akaunti ya Hodari na kuanza kufurahi faida hizi nilizozitaja hapa. Huduma hii ni kwa wajasiriamali wote iwe bodaboda, mama/ baba lishe, wauza genge, wenye maduka ya reja reja, wamachinga na wengineo, wote hawa kwetu ni Hodari na ujumbe wetu leo ni tunawaalika kuwa mahodari,” alisema Bruce.

Uzinduzi wa akaunti hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maoni ambayo benki hiyo ilipokea kutoka kwa wateja wake katika msimu wa kwanza wa kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako,” mwaka jana. Akitaja maboresho mengine ambayo yamefanyika kutokana na maoni ya wateja katika kampeni hiyo, Bruce alisema mapema mwaka huu benki hiyo ilizindua huduma ya SimBanking iliyoboreshwa zaidi ambayo inawawezesha wateja kujifungulia akaunti wenyewe, na kupata huduma za bima na mikopo kidijitali.


“Katika kampeni ya mwaka jana vilevile tulipata mrejesho kuhusu bima, ambapo hivi karibuni Benki yetu ilizindua kampeni maalumu ya elimu ya bima kwa umma yenye kauli mbiu ya “Furahia Maisha.. Bima Unachokithamini, jitihada zote ni matokeo ya kufanyia kazi maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla,” alisisitiza Bruce huku akibainisha kuwa kampeni ya mwaka ilifanikiwa kufika katika mikoa 20 na kufikia zaidi ya watu laki 1.

Akizungumzia dhumuni la kuifanya kampeni hiyo ya “Tupo Mtaani Kwako” kwa msimu wa pili, Bruce alisema wananchi wengi walipendekeza elimu ya huduma za benki kuendelea kutolewa kutokana na watu wengi kuwa na uelewa mdogo unaopelekea kuwa nje ya mfumo rasmi wa kibenki. “Tukiwa Benki ya kizalendo tunajukumu la kuhakikisha wananchi wote wananufaika na huduma za kibenki, hivyo tukaona ni vyema tukaifanya kampeni hii kuwa endelevu ili kusaidia lengo la Serikali la kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini ,” alisema Bruce.

 


Katika kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” ya mwaka huu Benki ya CRDB imejipanga kutumia timu ya wafanyakazi wake wabobevu katika masuala ya kibenki kuwatembelea wateja popote pale walipo, iwe ni ofisini, sokoni, dukani, stendi na kuwapatia huduma.

“Tutakuwa tukitumia magari yetu haya ambayo mnayaona hapa kuwafikia wateja mtaani, lakini pia tutakuwa na MaGazebo ambayo yatakuwepo mtaani kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wateja,” aliongezea Bruce huku akiwataka wateja kutumia fursa hiyo ya kusogezwa kawa huduma karibu kufungua akaunti na kuweka akiba.

Bruce amesema amesema kampeni hiyo pia inalenga katika kuhamasisha matumizi ya njia mbadala za utoaji huduma ikiwamo CRDB Wakala, SimBanking, Internet Banking na TemboCard. Kupitia njia hizi mteja anaweza kufanya miamala yake ya benki popote pale alipo kwa urahisi, usalama na unafuu.

“… hadi kufikia sasa tuna CRDB Wakala zaidi 20,000 nchi nzima ambao wanatoa huduma mtaani, kwahiyo tunaposema Tupo Mtaani Wako, pia tunamaanisha huduma za kibenki karibu zaidi na mteja kupitia CRDB Wakala,” alisisitiza Bruce huku akibainisha kuwa katika kampeni hiyo wateja watakuwa wakiunganishwa na huduma za SimBanking, Intenert banking na TemboCrad Visa, MasterCard na UnionPay.


--

JUMAPILI HII BELGIUM KUKIPIGA NA PORTUGAL NDANI YA DStv

 

Mwaga Biriani Urudi kwenu!

Jumapili hii hatua ya mtoano inaendelea kubamba na Belgium kukipiga dhidi ya Portugal ndani ya SS Euro2020, 224 saa 4:00 usiku

Nani kumwaga biriani?

Hakikisha unapiga *150*53# kulipia kifurushi chako cha Family sh 29,900 mapema kutazama mtanange huu.

#BirianiUlaya

Thursday 24 June 2021

BANCABC LAUNCHES A DEPOSIT CAMPAIGN

BancABC Tanzania Chief Commercial Officer, Joyce Malai speaks in Dar es Salaam after the bank launched a special deposit campaign of up to 14% interest upfront on structured fixed accounts. The upfront interest is aimed at enabling BancABC Tanzania customers to still run their businesses and daily activities without having to wait till the end of the tenure to earn. Left is the banks Acting Head of Treasury and global Markets Luiza Paschal.
BancABC Tanzania Chief Commercial Officer, Joyce Malai (right) and the banks Acting Head of Treasury and global Markets Luiza Paschal (left) display a placard after launching a special deposit campaign of up to 14% interest upfront on structured fixed accounts. 

Upto 14% upfront interest for one year.

June 23rd, 2021 - BancABC, which is part of Atlas Mara has made another milestone, launched a special deposit campaign of up to 14% interest upfront, on structured fixed deposit accounts.

Speaking in Dar es Salaam, the BancABC Chief Commercial Officer Mrs. Joyce Malai said they are introducing an annual interest rate of up to 14% for customers who will open fixed deposit accounts from today to end September this year and will be paid upfront interest instantly while their principal amounts remain secure until maturity.

“This is a good offer in the market so far and we want to encourage our customers and even those who do not bank with us to take advantage of this offer as it lasts,” she said.

RC DAR: NMB MKOMBOZI WA MAISHA YA WAFANYAKAZI, WASTAAFU TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akikaribishwa na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati) na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard wakati wa Siku ya walimu na NMB (Teachers Day) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiongea kwenye kongamano la siku ya walimu na NMB lililofanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB iliandaa siku ya walimu Dar es Salaam ambapo iliwapa mafunzo na elimu juu ya bidhaa za NMB zitakavyoweza kuwasaidia kwa Maisha ya baadae.
Baadhi ya Walimu kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam waliohudhuria kwenye kongamano la siku ya walimu na NMB lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. NMB Iliandaa siku ya walimu Dar es Salaam ambapo iliwapa mafunzo na elimu juu ya bidhaa za NMB zitakavyoweza kuwasaidia kwa Maisha ya baadae.

Watumishi wa umma nchini, hususani walimu, wamekumbushwa umuhimu wa kukopa kwa malengo, sambamba na kuepuka mikopo kandamizi, huku wakielezwa kuwa Benki ya NMB ni mkombozi, mshirika na rafiki sahihi wa maisha ya wafanyakazi kabla na baada ya kustaafu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dar es Salaam, Amos Makalla, wakati akizindua kongamano la siku moja la Walimu na NMB kwa mkoa wa Dar es Salaam 'Hatua kwa Hatua,' lililofanyika Jumatano, likiandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha walimu zaidi ya 300 toka wilaya za mkoa huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo, RC Makalla alibainisha kuwa, walimu na watumishi wengine wa umma wanapaswa kutambua umuhimu wa uwekezaji mdogo mdogo kwa ustawi wa maisha yao wawapo kazini na baada ya kustaafu na kutumia vema fursa za mikopo rafiki ya NMB.

BENKI YA DCB YASHIRIKI UZINDUZI WA MPANGO WA KUWAANDAA WANACHUO KATIKA SOKO LA KIBENKI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa UDBS, Dk. Evelyn Richard, Mkuu wa UDBS, Prof. Ulingeta Mbamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania (TBA), Tusekelege Joune.
Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), Prof. Ulingeta Mbamba, akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Kituo Huduma za Kibenki na Fedha wa UDBS, Dk. Tobias Swai, Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa UDBS, Dk. Evelyn Richard, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania (TBA), Tusekelege Joune.
Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Fedha wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), Dk. Evelyn Richard, akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mabenki Tanzania (TBA), Tusekelege Joune (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), chuoni hapo Dar es Salaam. 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakihudhuria uzinduzi huo chuoni hapo, Mlimani.
Kaimu Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya DCB, Meshack Kayila (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), waliohudhuria uzinduzi huo chuoni hapo, Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi na waalikwa wengine wakipiga picha ya kumbukumbuku muda mfupi baada ya uzinduzi wa program inayowaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa soko la ajira za kibenki uliondaliwa na shule hiyo, Dar es Salaam.

EMIRATES POSTS FIRST ANNUAL LOSS IN OVER 30 YEARS

An Emirates Airlines Boing 777 plane unloads a coronavirus vaccine shipment at Dubai International Airport in this picture taken on February 1, 2021

Dubai-based Emirates airline on Tuesday posted a $5.5 billion annual loss, its first in more than three decades, after the coronavirus pandemic devastated the aviation industry.

The carrier said it received a capital injection of $3.1 billion from its owner, the government of Dubai, to help it survive the crisis.

The Emirates group was "hit hard by the drop in demand for international air travel as countries closed their borders and imposed stringent travel restrictions", said chairman and chief executive, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum.

"No one knows when the pandemic will be over, but we know recovery will be patchy," he said in a statement.

The Middle East's largest carrier said that the fallout triggered a loss of 20.3 billion dirhams ($5.5 billion) over the financial year to March, after last year's 1.1 billion dirhams ($288 million) profit.

The airline, which was forced to temporarily suspend operations last year, saw revenue fall 66 percent to $8.4 billion.

Over the fiscal year Emirates carried 6.6 million passengers, down 88 percent from the same period in the previous year.

"The Covid-19 pandemic continues to take a tremendous toll on human lives, communities, economies, and on the aviation and travel industry," Sheikh Ahmed said.

"Economies and companies that entered pandemic times in a strong position, will be better placed to bounce back."

Wednesday 23 June 2021

BENKI YA EQUITY YAZINDUA KADI YA MALIPO YA EAZZY CARD

Mkuu wa Biashara wa Equity Group, Polycap Igathe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Bank Tanzania, Esther Kitoka (kulia) wakionyesha mfano wa kadi mpya ya "Eazzy Card" iliyozinduliwa na benki hiyo Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Biashara wa Equity Group, Polycap Igathe (kushoto) akishika kadi mpya "Eazzy Card" pamoja na viongozi wa Equity Bank Tanzania katika uzinduzi wa kadi hiyo mpya ya malipo uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.
  • Kadi za malipo ya awali zinazowezesha malipo ya kidijitali
  • Huweza kufunguliwa kwa mteja na asiyemteja wa Benki ya Equity
  • Huwezesha malipo Masaa 24 kupitia POS, ATM, Wakala na njia ya mtandao
  • Haina makato
  • Ni rahisi kuijaza fedha kupitia Eazzy Banking, Wakala, Matawini na Huduma Fedha za Simu za mikononi.
  • Inaruhusa pia malipo ya haraka kwa njia ya kugusa “tap and go”
Dar es Salaam Tanzania, 22 June, 2021 – Benki ya Equity (T) leo wamezindua rasmi kadi ya malipo ya awali ijulikanayo kama “Eazzy card” ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya kiditali na nchini kupitia huduma za fedha jumuishi.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank (T) Robert Kiboti alisema, kuwa kadi hiyo ni ya malipo ya kabla, ambapo mmiliki anaweza kutumia kiasi cha fedha ambacho tayari amekiingiza na kukitunza katika kadi yake husika. “Kadi hii ni ya malipo ya awali hivyo inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo kulipia ankara au bili, kununua bidhaa, kutoa pesa kwenye mashine za ATM na pia kufanya malipo ya mtandaoni.”