Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert

DSTV Advert

Stanbic Bank Adverts

Zantel Advert

NMB Bank Advert - NMB Mkononi

Advertise Here

Advertise Here

Wednesday, 31 October 2018

BUILDING OF ISAKA-KIGALI RAILWAY TO START IN DECEMBER


Tanzania and Rwanda have announced that the construction of the 571km-long standard gauge railway line linking Isaka township in Tanzania with the Rwandan capital, Kigali will begin this December once a contractor has been identified.

The announcement was made through a joint statement by the Tanzania Minister for Works, Transport and Communication, Isaack Kamwelwe, and his Rwandan counterpart Claver Getete when the two met recently in Dar es Salaam to finalise plans of the $2.5 billion project.

The ministers were accompanied by members of the Joint Technical Monitoring Committee.

The two countries also agreed on the financing modalities, with Tanzania seeking a loan to fund the Isaka-Rusumo stretch and Rwanda opting for a public-private partnership model for its stretch of the line.

When completed, the railway line is expected to improve trade between the two countries by making it easy and cheaper for people and cargo to move across the common border.

On a state visit to Tanzania in January, President Paul Kagame and his host President John Magufuli, jointly asked for the fast-tracking of the project.


BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WODI YA WANAWAKE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA AMANA

Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mkutano wa makabidhiano ya misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10, magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 katika wodi ya wananwake Hospitali ya Amana Ilala Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dr. Amim Kilomoni.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dr. Amim Kilomoni (kulis) akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya misaada mbalimbali toka Benki ya KCB ikiwemo vitanda 10, magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali hiyo leo jijini Dar Es Salaam. 
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni moja kati ya Vitanda na Vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 kwa wodi ya wanawake Hospitali ya Amana, Dar Es Salaam.
Wafanyakazi wa KCB na wauguzi wa Hospitali ya Amana wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Benki ya KCB kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 6,017,000 kwa wodi ya wanawake leo kwenye Hospitali ya Amana Ilala, Dar Es Salaam.
Dar es Salaam, 31 Octoba, 2018 – Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada wenye thamani ya milioni 6 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa benki hiyo, Christine Manyenye alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu, Mazingira, Ujasiriamali na masuala ya ubinadamu”, Bi. Manyenye alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofungua milango yake hapa Tanzania mwaka 1997, imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

Benki ya KCB ilikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilling 6,017,000 katika Hospitali hiyo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa upungufu wa vitanda, magodoro na masuka katika hospitali nyingi nchini ni changamoto hasa katika wodi za akina mama na watoto Benki ya KCB iliamua kutoa msaada huo ilikupunguza changamoto hizo.

DKT. ABDULLAH MAKAME AHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA MASUALA YA UHAMIAJI JIJINI RABAT, MOROCCO


Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Africa Mashariki (EALA), Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, akiwa katika mkutano malum unaohusu masuala ya Uhamiaji jijini Rabat, Morocco, tarehe 30 - 31 Oktoba 2018.  Mkutano huo umedhaminiwa na Mfalme Mohammed VI wa Morocco.

LION AIR: WHY DID A BRAND-NEW BOEING JET CRASH 13 MINUTES AFTER TAKEOFF?


(CNN) - The plane behind Lion Air's crash off Indonesia was one of Boeing's newest and most advanced jets. It was just two months old and with 800 hours under its belt, so experts are baffled as to what exactly caused the 737 MAX 8 to crash.

While no information has been released yet as to why the brand-new plane crashed into the sea 13 minutes after takeoff, FlightRadar24 has published data that shows the plane behaving erratically during takeoff. When a plane would normally be ascending in the first few minutes of flight, the Lion Air jet experienced a 726-foot drop over 21 seconds.

Aviation expert Philip Butterworth-Hayes told CNN that the data was unusual -- especially since takeoffs like this are typically controlled by the plane's automatic systems.

"This doesn't fit an automatic flight profile," Butterworth-Hayes said while studying the data. "Unless, the aircraft was trying to correct itself at the time for a number of reasons."

2018 AFRICAN ECONOMIC CONFERENCE TO OFFER PRACTICAL SOLUTIONS - AFRICAN DEVELOPMENT BANK

“The 2018 African Economic Conference (AEC) will feature practical solutions from regional integration experts and the private sector,” a senior African Development Bank staff has said, as preparations for the event move into top gear.

The 13th conference of the EAC, will take place in Kigali, Rwanda from December 3–5, 2018, under the theme “Regional and Continental Integration for Africa’s Development.” The United Nations Development Programme (UNDP) will host the meeting. The EAC is the leading forum for discussing African issues of the day.

“Expectations for the 2018 AEC are high,” organizers – African Development Bank, UNDP and United Nations Economic Commission for Africa – said as they held a teleconference on Thursday 25 October 2018 in Abidjan, for preparatory talks on the upcoming meeting.

“The conference will be less academic, geared towards bringing together regional integration practitioners to provide us with practical solutions especially in the implementation of the African Continental Free Trade Area (AfCFTA). Private sector representatives will be sharing their experiences as they do business on the continent,” Bank Director for Integration, Moono Mupotola, said.

Tuesday, 30 October 2018

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO MAONYESHO YA VIWANDA MKOANI PWANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, kwa kuwa wadhamini wakuu wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, akitoa hotuba yake wakati wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, baada ya kutoa hotuba yake wakati wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani. Benki ya CRDB ni wadhamini wakuu wa Maonyesho hayo. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, wakati wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (wa tatu kulia) alipokuwa akimueleza machache juu ya huduma wanazotoa, wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB, kwenye Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela.


MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA MSAADA WA VIFAA VYA AFYA KWA VITUO VYA AFYA KISARAWE VYENYE THAMANI YA MILIONI 15

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan, ameishukuru Benki ya NMB kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 108, mashine za kupumulia wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 vikilenga kusaidia kituo cha Maneromango, Kurui na Chole vyote vikiwa wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Akipokea vifaa hivyo Makamu wa raisi aliushukuru uongozi wa Benki ya NMB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la afya kwa wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine hapa nchini.

Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Vicky Bishubo alimkabidhi Makamu wa rais Samia Suluhu msaada huo wa vifaa kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokea msada huo mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia mashine ya Oxygen iliyokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo kwaajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe. NMB ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Wa pili kutoka (kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya kitanda cha kujifungulia kilichokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NMB, Joseline Kamuhanda.

AIRTEL EXTENDS SUPPORT TO MOROGORO ORPHANAGE CENTER

Airtel Tanzania Director of Customer Care Service Adriana Lyamba (right) hands over humanitarian assistance to Mgolole Orphanage Center Assistance Manager Sister Valeria Mnyanzaga (left) in Morogoro. Airtel Tanzania through Airtel Tunakujali programme visited the centre and donated various humanitarian assistance worth TZS 18 million to the Orphanage center over the weekend.
Airtel Tanzania Director of Customer Care Service Adriana Lyamba (right) hands over mosquito nets to Mgolole Orphanage Center Assistance Manager Sister Valeria Mnyanzaga (left) in Morogoro. Airtel Tanzania through Airtel Tunakujali programme visited the centre and donated various humanitarian assistance worth TZS 18 million to the Orphanage center over the weekend.
Airtel Tanzania Director of Customer Care Service Adriana Lyamba (right) hands over a mattress to Mgolole Orphanage Center Assistance Manager Sister Valeria Mnyanzaga (left) in Morogoro. Airtel Tanzania through Airtel Tunakujali programme visited the centre and donated various humanitarian assistance worth TZS 18 million to the Orphanage center over the weekend. Center is Airtel Tanzania Experience Manager Deogratius Hugo.
Airtel Tanzania Director of Customer Care Service Adriana Lyamba (right) hands over a bed to Mgolole Orphanage Center Assistance Manager Sister Valeria Mnyanzaga (left) in Morogoro. Airtel Tanzania through Airtel Tunakujali programme visited the centre and donated various humanitarian assistance worth TZS 18 million to the Orphanage center over the weekend. Center is Airtel Tanzania Experience Manager Deogratius Hugo.
Airtel Tanzania through its Customer Care Department has donated various humanitarian assistance to Mgolole Orphanage Center in Morogoro. The donation included foodstuffs, utensils, beds, Mattresses and a refrigerator all worth TZS 18 million.

The donation of the humanitarian assistance is part of the company’s programme of Airtel Tunakujali where the company’s policy where employees contribute their own funds to support the less privileged and the needy in the society.

VODACOM YASHEREHEKEA ‘UBORA WA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA’

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare.
Katika kuadhimisha miaka 18 ya utoaji huduma kwa wateja wao Vodacom Tanzania (PLC) yafanya mwezi mzima wa October kuwa mwezi wa huduma kwa wateja. Vodacom, imeendeleza sherehe za wiki ya huduma kwa wateja, ambazo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, na mwaka huu kauli mbiu ikiwa ni ‘Kusherehekea ubora wa utoaji huduma’.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare, amebainisha kuwa, lengo kuu la kuendeleza maadhimisho hayo ni kuwashukuru wateja wao, watoa huduma na kuonyesha huduma mbalimbali wanazozindua kwa dhumuni la kuwasaidia wateja.

“Tunafurahia kuona Vodacom inaongoza katika kubadilisha maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 12 na kuwaunganisha popote duniani. Huduma zetu zimekuwa za kwanza nchini, zimepokelewa vizuri na kuendelea kutufanya Mtandao bora wa simu nchini.”

Akiongelea mchango wa huduma zao kwa watanzania na uchumi kwa ujumla, Harriet alisema kuwa “M-Pesa imekuwa msaada mkubwa kwa huduma za kifedha kama kutuma na kupokea fedha ndani na nje ya nchi, kufanya manunuzi, na kulipa bidhaa na ankara”. Huduma nyongeza kama M-Pawa imesaidia kuboresha maisha ya watu daraja la chini na hata wa kati kwa kutoa mikopo isiyo na usumbufu kwa riba nafuu.

ECOBANK INTRODUCES RAPIDTRANSFER MOBILE APP AND SLASHES COST OF INTERNATIONAL REMITTANCES

VODACOM YAHIMIZA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE - SPORTS BONANZA

KAMPUNI ya mawasiliano Vodacom Tanzania imehimiza wafanyakazi wake pamoja na jamii kuzingatia michezo ili kuweza kuimarisha utendaji kazi pamoja na ubora wa afya kwa manufaa binafsi na manufaa ya taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa kazi Vodacom Bi. Karen Lwakatare wakati wa siku ya Vodacom Sport Bonanza day iliyofanyika Jumamosi katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.

"Tunafanya bonanza kwa ajili ya wafanyakazi wote wa Vodacom kuhamasisha mazoezi kwa afya ya wafanyakazi na jamii kiujumla. Mshindi atakayepatikana atapata fursa ya kwenda kushiriki mashindano ya Vodacom Wellbeing Challenge ya mwaka ambayo hufanyika nje ya nchi yanayowakutanisha wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone duniani” Lwakatare aliongeza.

Bonaza hilo limehusisha michezo ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kukimbia, kuogelea, gofu, tenesi, Volley ball, kuruka kamba, draft, rede kutembea kwa miguu na kuendesha baisikeli kutoka ofisi za makao makuu ya Vodacom hadi Gymkhana.


Kundi la waendesha baiskeli wakishangilia baada ya kuwasili viwanja vya Gymkhana kutokea makao makuu ya kampuni ya Vodacom, Jumamosi wakati wa siku ya Vodacom Bonanza iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana.
Glory Mtui akiongoza mbio za baiskeli kutoka makao makuu ya ofisi za Vodacom kuelekea viwanja vya Gymkhana jana wakati wa Sports Bonanza ya kampuni ya Vodacom.
Sandra Oswald akiongoza mbio za baiskeli kutoka makao makuu ya ofisi za Vodacom kuelekea viwanja vya Gymkhana jana wakati wa Sports Bonanza ya kampuni ya Vodacom. 
Mwanandada Naaja akiwaongoza wafanya kazi wa Vodacom Tanzania kwenye mazoezi ya viungo jana katika viwanja vya Gymkhana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakifanya mazoezi ya viungo jana katika viwanja vya Gymkhana kuadhimisha siku ya Vodacom Sports Bonanza.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishindana mchezo wa kuogelea katika viwanja vya Gymkhana wakati wa maadhimisho ya Vodacom Sports Bonanaza.

DKT. MAHIGA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI ITALIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Taasisi ya kidini ya Mt. Egidio Padri Angelo Romano. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi ya Taasisi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2018 jijini Roma. Dkt. Mahiga yupo Italia kwa ajili ya kuhudhuria mikutano mbalimbali ikiwemo Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Afrika na Italia ambao utafanyika tarehe 25 Oktoba,2018 pamoja na kukutana na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendedelo ya Kilimo (IFAD) tarehe 26 Oktoba,2018.
Dkt. Mahiga akiagana na Padri Angelo Romano mara baada ya kumaliza mazungumzo.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. George Madafa tarehe 25 Oktoba, 2018 akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Dkt. Augustine Mahiga(Mb), kwenye kikao na Watanzania waishio nchini Italia. Kikao hicho kilifanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Italia Bw. Andrew Mohele akitoa salamu za wanadiaspora kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga. Mkutano huo ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2018 kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Rome, Italia.
Baadhi ya Watanzania waishio Italia wakiwa kwenye mkutano huo.

BALOZI DKT. SLAA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA FINLAND

Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic, na Baltic Mhe. Wilbrod Slaa awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Finland, Mheshimiwa Sauli Niinistö jijini Helsinki.
Balozi Dkt. Slaa akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sauli Niinistö.

CURRENT VACANCIES AT THE AFRICAN DEVELOPMENT BANK
UBELGIJI YAAMBIWA IONGEZE UWEKEZAJI NCHINI, MHANDISI MANYANYA

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye kongamano la biashara kati ya Tanzania na Ubelgiji. kongamano hilo lilifanyika katika Hoteli ya Serena jini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bw. John Mathew Mnali akiongea katika kongamano hilo.
Wafanyabiashara kutoka Ubelgiji na Tanzania na wageni waalikwa wakimsikiliza Naibu Waziri wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la biashara katika Hoteli ya Serena. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na wafanyabiashara kutoka Ubelgiji wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Manyanya.
Ubelgiji imetakiwa kuongeza kiwango cha uwekezaji nchini ili kuchochea zaidi kasi ya azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Ubelgiji na Tanzania linalofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam.

“Kuna miradi 32 yenye thamanai ya Euro milioni 902 ambayo imeajiri wafanyakazi 1814 inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Ubelgiji nchini Tanzania. Hivyo, kuna umuhimu wa kuongeza uwekezaji huo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni mazuri na yanavutia”, Mhandisi Manyanya alisema.

Mhe. Naibu Waziri aliwahamiza wawekezaji hao ambao ni wafanyabiashara wakubwa nchini Ubelgiji kuwekeza katika sekta za kilimo, hususan kwenye maeneo ya viwanda vya nguo, sukari, mafuta ya kupikia, maziwa, ngozi, nyama, mbegu, matunda na maua,

Sekta nyingine aliyoitaja ni ya nishati hasa katika miundombinu ya kuzalisha na kusambaza gesi asilia na nishati jadilifu.
Maeneo mengine yaliyosisitizwa na Mhe. Naibu Waziri ni pamoja na sekta ya utalii, madini, uvuvi katika bahari kuu, miundombinu, maeneo maalum ya viwanda (industrial parks) na ujenzi wa majengo hususan katika mji mkuu wa Dodoma ambapo mahitaji ni makubwa.

Uzalishaji wa dawa za binadamu na wanyama, vifaa tiba na uzalishaji wa samani za kisasa ni maeneo ambayo Mhe. Naibu Waziri aliwasihi wawekezaji hao kuyapa jicho la pekee.