Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 30 October 2018

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA MSAADA WA VIFAA VYA AFYA KWA VITUO VYA AFYA KISARAWE VYENYE THAMANI YA MILIONI 15

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan, ameishukuru Benki ya NMB kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 108, mashine za kupumulia wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 vikilenga kusaidia kituo cha Maneromango, Kurui na Chole vyote vikiwa wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Akipokea vifaa hivyo Makamu wa raisi aliushukuru uongozi wa Benki ya NMB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la afya kwa wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine hapa nchini.

Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Vicky Bishubo alimkabidhi Makamu wa rais Samia Suluhu msaada huo wa vifaa kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokea msada huo mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia mashine ya Oxygen iliyokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo kwaajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe. NMB ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Wa pili kutoka (kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya kitanda cha kujifungulia kilichokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NMB, Joseline Kamuhanda.

No comments:

Post a Comment