Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 28 July 2021

WASANII WA ZANZIBAR WANOLEWA

Meneja wa Chapa wa Zantel, David Maisori akizungumza wakati wa semina kwa wasanii wa muziki visiwani Zanzibar. Tukio hilo ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel litakalofanyika siku ya Agosti 21 katika Viwanja vya Amani Zanzibar.
Wasanii mbalimbali wa muziki kutoka Zanzibar, wakifuatilia kwa umakini semina maalumu juu ya namna bora ya kukuza vipaji vya muziki visiwani humo. Semina hiyo ni sehemu ya Tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel litakalofanyika Agosti 21, katika Viwanja vya Amani Zanzibar.
Msaanii wa muziki kutoka kundi la Wasafi, Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa semina kwa wasanii wa muziki visiwani Zanzibar. Semina hiyo ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel litakalofanyika Agosti 21, katika viwanja vya Amani Zanzibar.

EQUITY BANK (T) INTRODUCES INTERBANK MONEY TRANSFERS AND SADC (SIRESS) SERVICES TO BOOST CROSS BOARDERS' AND REGIONAL REMITTANCE SERVICES.


  • Customers with Equity Bank accounts can now transact seamlessly in any of the Equity Bank branches across Africa.
  • SIRESS services to boast and facilitate monetary transactions to and from the SADC block at the cost of USD 10 only regardless of the amount 
Dar es Salaam, Tuesday 27th July 2021 - Equity Bank Tanzania has introduced to the market two new remittance services aiming to boast inter-country and regional remittance transactions. The new platforms, namely, Equity Bank Interbank transfers, allow real-time transactions for Equity Bank customers in any Equity Bank group branches and SADC Integrated Regional Electronic Settlement System (SIRESS) Services that opens up remittance transactions within the 16 SADC countries.

Speaking at an event in Dar es Salaam yesterday, Equity Bank Managing Director Robert Kiboti said: "We are proud to provide a reliable financial link between Equity Bank Tanzanians customers with the rest of Equity bank network through our One Equity Inter-Country services that allow seamless real-time transactions at a minimal cost. Simply, Equity Bank Customers will be able to make deposits, receive deposits, and make withdrawals at any Equity Bank branch online in Kenya, Uganda, Rwanda, South Sudan, and Congo DRC as a domicile country. Also, Equity customers can now transfer to an Equity customer in any country of operation. Through our world-class digitization of the product, Equity Bank customers will enjoy the freedom of accessing all these services at their convenience of Eazzy Banking App-, and Eazzy Net& Eazzy Biz- Intercountry Funds transfer on our online banking platforms.

"The primary purpose of the product is to provide solutions for Equity customers and non-customers (deposit only) across the Group to access their accounts and transact from any of the Equity Bank group subsidiaries, in any of the local currencies. "We believe this will be an important solution to facilitate cross-border payments between Tanzania, Kenya, Congo DRC, Rwanda, and the rest of Equity network. I call upon all cross-border traders, including SMEs, Transporters, and the likes to capitalize on these new services from Equity Bank," said Mr. Kiboti.

NMB YAKABIDHI HUNDI YA SH. MILIONI 438.4 KWA WAHANGA WA MOTO KARIAKOO

Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya NMB, Martine Massawe akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa wafanyabiashara waliokuwa na Bima waliounguliwa katika Soko Kuu la Kariakoo. Kushoto ni Meneja Madai wa Kampuni ya Bima ya Reliance, Joel Mwakalebela na kulia ni Meneja wa Bima Benki ya NMB, Adam Nsenga.
Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB, Martine Massawe (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 438 kwa wafanyabiashara 12 waliokuwa na Bima waliounguliwa katika Soko Kuu la Kariakoo, Sajida Kagasheki na Emmanuel Kabadi (kushoto) wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Tawi la NMB Kariakoo Business Center. Kutoka kulia ni Meneja wa Bima wa Benki ya NMB, Adam Nsenga na Meneja wa Kampuni ya Reliance, Joel Mwakalebela.
Meneja wa Madai wa Kampuni ya Bima ya Reliance, Joel Mwakalebela akipongezana na mmoja wa wafanyabiashara waliounguliwa na Moto katika Soko Kuu la Kariakoo, Emmanuel Kabadi (kushoto) baada ya Benki ya NMB kukabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya Shilingi Milioni 438 kwa wafanyabiashara 12 waliokuwa na Bima. Kushuto ni Sajida Kagasheki mmoja wa wafanyabiashara na Kulia ni Meneja wa Bima wa Benki ya NMB, Adam Nsenga.

Benki ya NMB kupitia Kampuni ya Reliance Insurance, imewalipa bima ya Sh. Milioni 438.4 wafanyabiashara 12, kati ya waliounguliwa moto maduka yao katika Soko la Kariakoo, Julai 10 mwaka huu. Wafanyabiashara hawa ni waliokuwa wamekatia bima mikopo na biashara zao kupitia NMB.

Hafla ya kuwakabidhi wafanyabiashara hao hundi hiyo, imefanyika katika Tawi la NMB Kariakoo Business Center, ambako wahanga hao walikiri kuwa hasara na maumivu yao ya kuunguliwa yamepozwa na malipo hayo ya haraka ya bima.

Akizungumza kabla ya kuwakabidhi hundi ya mfano, Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya NMB, Martine Massawe, alitoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni chanya wa kuzilinda kwa bima mali na pesa wanazotafuta kwa jasho, ili kuepuka maumivu yasiyo na mfariji wakati wa majanga.

“Tuko hapa kwa ajili ya kuwafuta machozi wafanyabiashara waliokata bima nasi kupitia mikopo yao ama waliokuwa na bima za mali bila mikopo, ambao walikuwa sehemu ya wahanga wa moto sokoni Kariakoo.

“Wito kwa Watanzania, moto wa Soko la Kariakoo uwe fundisho kwao juu ya umuhimu wa bima. Moto ama majanga huja bila kuyatarajia, unapokata bima unakuwa umejiwekea kinga kuilinda pesa ama mali uliyotafuta kwa jasho lako.

Tuesday 27 July 2021

BANK OF TANZANIA NOTICE TO THE PUBLIC - POLICY MEASURES TO PROMOTE CREDIT TO PRIVATE SECTOR AND LOWER INTEREST RATES

HATUA NNE ZA KUTOA RISITI KIDIGITALI KWENYE SIMU YAKO



Web Technologies (T) Limited

Tel: +255 22 218 2912

Mobile: +255 716 888 333 / 685 888 333

JOB VACANCIES AT WEB TECHNOLOGIES (T) LIMITED

AMANA BANK YAZINDUA PROGRAMU YA KIDIGITALI INAYOWEZESHA HUDUMA ZA KIISLAMU

Wafanyakazi wa Benki ya Amana wakijaribu matumuzi ya App hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam.
Wateja wa Amana Bank wakipatiwa maelezo ya matumizi ya teknolojia hii mpya ya kidigitali wakati wa hafla ya uzindzi.

Wakati taasisi za kifedha zinaendelea kubadilika na kurahisisha huduma na njia ya kufanya biashara, Amana Bank imetangaza kuzindua programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama Amana Bank App ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni.

Amana Bank Limited, inayoongoza kwa kutoa huduma za Kibenki za Kiisilamu nchini Tanzania, leo imetangaza kuwa imefanya mapinduzi ya huduma zake za kibenki kupitia simu za mkononi kwa kuanzisha programu mpya kupitia simu za mkononi, inayomwezesha mteja kufanya malipo na huduma za kibenki kwa wateja wake iitwayo Amana Bank App; Programu inawezesha kupata huduma za kibenki kidigitali kama vile kufanya malipo, kuhamisha fedha, kulipa bili na kufanya malipo mtandaoni, kupokea taarifa za benki na kupokea habari juu ya huduma zinazotolewa na benki kama mikopo, viwango vya ubadilishaji wa kigeni na hata kulipia huduma mbalimbali kama malipo ya serikali na huduma za bima.

INTERNSHIP OPPORTUNITIES / JOB VACANCY AT AIR TANZANIA

JOB VACANCIES AT AZANIA BANK LIMITED

DC NYAMAGANA: WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOLETWA NA NMB

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Alex Mgeni akipokea bidhaa zilizosindikwa na Mjasiriamali, Doroth Kimati anayewezeshwa na NMB katika uzinduzi wa Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza. Katikati ni Mjasiriamali, Hellen Bugoye.
Baadhi ya akina mama wajasiriamali wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye uzinduzi wa Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, akizungumza wakati akizindua Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri"  jijini Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Bi. Amina Makilagi amewaasa wanawake wilayani humo kuchangamkia fursa zinazoletwa kwao na benki ya NMB kwa maendeleo yao ya kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na umati wa wanawake na wakazi wengine wa mkoa huo waliohudhuria uzinduzi wa klabu ya ‘mwanamke jasiri’ mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.

Bi. Makilagi alisema kuwa wakazi wa Mwanza wasiache kuchangamikia fursa zinazoletwa na benki ya NMB kwani benki hiyo ina malengo mazuri ya kutaka kuleta maendeleo kwa wateja wake.

Monday 26 July 2021

DStv INAKULETEA CHANELI MPYA YA BURUDANI

 

DStv wakali wa burudani wanakuletea Chaneli mpya itakayokuwa ikirusha filamu kali za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Uganda).

Pata kuburudika na filamu hizi kupitia Chaneli ya Maisha Magic Movies 141, itakayoanza kuruka kuanzia leo tarehe 26 July 2021, saa 10 jioni.

Kulipia kifurushi chako piga *150*53# ili usikose burudani hii.

BANK OF TANZANIA INDICATIVE EXCHANGE RATES 26-07-2021

 

JOB VACANCIES AT DCB COMMERCIAL BANK


BENKI YA NMB KUWAKOPESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO ZAIDI YA SH. 120 BILIONI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Alex Mgeni wakifurahia jambo baada ya kuzungumza rasmi na Klabu ya Madini ya ‘NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa. kushoto ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Dickson Richard na Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini, John Bina.
Sehemu ya wageni waalikwa ambao ni miongoni mwa Wachimba Madini wa Kanda ya Ziwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa 'NMB Mining Club' uliofanyika katika Hoteli ya Gold Crest - Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa.

Benki ya NMB imepanga kutumia zaidi ya Sh.120 bilioni kutoa mikopo ya mitaji, vifaa na mitambo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija katika Sekta ya Madini nchini. Akizungumza jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Klabu la Wachimba Madini Kanda ya ziwa, (NMB Mining Club) Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Alex Mgeni alisema hadi sasa, tayari benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh.63 bilioni kwa kundi hilo.

“Wachimbaji wadogo watakopeshwa vifaa na mitambo bila kulazimika kuweka dhamana kwa sababu mitambo na vifaa hivyo ndivyo vutakuwa dhamana yao baada ya kulipa kuanzia asilimia 20 ya thamani ya kifaa au mtambo anaotaka kununua,” alisema Mgeni.

Akizuzugumza wakati wa hafla hiyo iliyoshirikisha wachimbaji zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera, Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania (Femata), John Bina alisema uamuzi wa benki ya NMB kuanzisha dirisha la mikopo kwa Sekta ya Madini siyo tu utaongeza tija, bali pia utakuza uchumi wa wachimbaji na Taifa kwa ujumla.

Friday 23 July 2021

WAKUU WA MIKOA YA SINGIDA NA MOROGORO WAKIRI NMB KUWA CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA WAALIMU

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mwembesongo, Abdula Omary akichangia mada wakati wa kongomano la Benki ya NMB na Walimu lililofanyika Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigela (katikati) akizungumza jambo na Meneja Mwandamizi wa Mikopo kwa Watumishi na Taasisi za Serikali Benki ya NMB, Emmnuel Mahodanga (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma za Kidigitali, Tito Mangesho baada ya Mkuu huyo kufungua kongomano la Benki ya NMB na Walimu lililofanyika Mkoani Morogoro.

Wakuu wa Mikoa ya Singida na Morogoro, Dr. Binilith Mahenge na Martin Shigela kwa nyakati tofauti wamekiri kuwa benki ya NMB imekuwa kinara katika kuimarisha waalimu kiuchumi kupitia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.

Wakizungumza katika warsha za siku ya mwalimu ambazo huandaliwa na Benki ya NMB katika mikoa yao, Wakuu hao wamewasisitiza Waalimu kuzitumia vyema huduma za benki hiyo katika kujiimarisha kiuchumi.

Katika warsha ya mkoani Singida, Mkuu wa Mkoa huo, Dr. Mahenge alisema kuwa NMB imekuwa na huduma nzuri zaidi za mikopo ambayo ni rafiki na haina masharti magumu kwa walimu. Hivyo akawasihi waalimu wachangamkie fursa hiyo na akashauri waweze kutumia mikopo hiyo katika kilimo cha alizeti ambayo inastawi sana mkoani hapo huku zao hilo likiwa chanzo kikubwa cha mapato katika mkoa wa Singida.

NMB YAKABIDHI MADAWATI YA SH. MILIONI 10/- MKURANGA

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ally (katikati) akiangalia Viti na Meza 50 baada ya kukabidhiwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mkugilo pamoja na madawati 62 kwa ajili ya Shule ya Msingi, Chatembo iliyopo Mwandege wakati wa hafla ya makabidhiano .Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mkuranga, Peter Msaki na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ally, akionyeshwa Meza na Viti na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mkuranga, Peter Msaki vilivyolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Sekondari Mkugilo pamoja na madawati 62 kwa Shule ya Msingi, Chatembo iliyopo Mwandege vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 10. Kulia ni Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB wa Biashara za Serikali, Aneth Kwayu.

Benki ya NMB imetoa msaada wa viti 50, meza 50 kwa shule ya Sekondari ya Mkugilo na madawati 62 kwa Shule ya Msingi Chatembo, wilayani Mkuranga, Pwani vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 10.

Msaada huo, ulitolewa katika hafla iliyofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Mkugilo na Meneja Mahusiano, Biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Mashabiki, Aneth Kwayu kwa niaba ya NMB na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasser Ally.

Akizungumza katika hafla hiyo Aneth alisema kuwa NMB inazitazama changamoto za Sekta ya Elimu kama moja ya vipaumbele vyake vikuu, kutokana na ukweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maendeleo sio tu ya mtu mmoja mmoja, bali pia kwa Taifa kwa ujumla- hivyo walivyopata maombi kuzisaidia shule hizi mbili waliona uhitaji na wamezisaidia.

DStv INAKULETEA CHANELI MPYA YA MAISHA MAGIC MOVIES



Kaa mkao wa kula sasa uweze kufurahia filamu za nyumbani na Afrika Mashariki ndani ya chaneli mpya ya #MaishaMagicMovies chaneli 141 inayokujia rasmi kuanzia tarehe 26 Julai 2021.

Hakikisha hupitwi na Utamu wa Chaneli hii kupitia kifurushi cha Compact TShs 49,000 tu kwa kupiga *150*53# kulipia kifurushi chako.

Wednesday 21 July 2021

BENKI YA AZANIA YATOA BIMA KWA WAKULIMA ZAIDI YA 700 WA TUMBAKU

Meneja Mwandamizi wa Biashara kutoka Benki ya Azania, Jackson Lohay (kulia) akikabidhiana nyaraka za mkataba wa mkopo wa bima ya afya na Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha wilaya ya Chunya (CHUTCU), Elieza Fijadh (katikati) na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mbeya, Mbala Shitindi (kushoto).

Mbeya. Julai 20, 2021 - Benki ya Azania kwa kushirikiana na mfuko wa bima ya afya (NHIF) pamoja na chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa tumbaku wilaya ya Chunya, (CHUTCU) wamesaini makubaliano ya kuwawezesha wakulima wa zao hilo kujiunga na bima afya ili waweze kupata matibabu bure.

Makubaliano hayo yamefanyika Julai 19, 2021 kati ya Benki ya Azania Limited,NHIF na CHUTCU katika kata ya Lupatingatinga, halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya hiyo Mayeka Simon Mayeka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mwandamizi wa Biashara wa Azania Bank Limited, Jackson Lohay alisema katika makubaliano hayo benki hiyo itatoa mkopo usiokuwa na riba kwa ajili ya kuwawezesha wakulima zaidi ya 700 kupata bima ya afya.

“Katika mkataba wetu tutawawezesha wanachama ambao wapo chini ya chama kikuu cha ushirika ambao ni zaidi ya 700 lakini watakaonufaika na mpango ni zaidi ya watu 2000 wanaotegemewa na wanachama,’’ alisema

ZANTEL YAZINDUA KIJIJI CHA KIDIGITALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA MTANDAO

Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa akifurahia jambo na mgunduzi wa teknolojia, Said Sugu wakati wa uzinduzi wa Kijiji cha kidigitali ‘Digital Village’ ambacho ni maalum kwa ajili ya watu kujifunza matumizi ya mtandao wa 4G. Kulia ni Soud Hassan, mbunifu wa teknolojia. Wagundunduzi hao wamefanikisha kutengeneza vitu mbalimbali ikiwamo helikopta na magari wakitumia kipaji na intaneti kama nyenzo ya kujifunzia.
  • Watu kujifunza namna ya kujiendeleza kielimu na kuendesha biashara mtandaoni
Zanzibar. Jumatatu, Julai 19, 2021 - Kampuni ya simu ya ZANTEL leo imezindua kijiji cha kidigitali, eneo ambalo limewekwa miundombinu imara ya intaneti kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wakazi wa Zanzibar namna bora ya kutumia mitandao katika kujiendeleza kielimu na kibiashara.

Hatua hii ni miongoni mwa utekelezaji wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ awamu ya pili, ambayo pamoja na mambo mengine ina lenga kutoa elimu kwa wakazi wa Zanzibar juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi.

Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Zantel wa kuchochea mageuzi ya kimtandao na kufanya watu waishi kidigitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema kuwa kituo hicho cha Kiditali kitatoa huduma za kimtandao bure kwa wakazi wa Zanzibar ndani ya miezi miwili.

BENKI YA DCB YAZIDI KUKUA NA KUPATA FAIDA; YAWAAMBIA WANAHISA WAKE KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA ILALA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wa Halmashauri ya Jiji la Ilala ukihudhuriwa na watendaji, wakuu wa idara, madiwani na mbunge wake jijini Dar es Salaam hive karibuni. Wengine kutoka kushoto ni; Mweka Hazina wa Jiji la Dar es Salaam, Tulusubya Kamalamo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Tabu Shaibu, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akizungumza na wanahisa wa Benki ya Biashara ya DCB wa Halmashauri ya Jiji la Ilala ukihudhuriwa na watendaji, wakuu wa idara, madiwani na wabunge wao jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni; Mweka Hazina wa Jiji la Dar es Salaam, Tulusubya Kamalamo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Tabu Shaibu, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa na na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (kushoto), akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wa Halmashauri ya Jiji la Ilala ukihudhuriwa na watendaji, wakuu wa idara, madiwani na mbunge wake jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake nyuma yake ni; Mweka Hazina wa Jiji la Dar es Salaam, Tulusubya Kamalamo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Tabu Shaibu, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Tabu Shaibu akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati Benki ya DCB ikifanya mkutano na wanahisa wake kutoka kkatika Halmashauri ya Jiji la Ilala.
Baadhi ya madiwani, wakurugenzi na wakuu wa idara kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Ilala wakihudhuria mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya madiwani, wakurugenzi na wakuu wa idara kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Ilala wakihudhuria mkutano huo jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Idara ya Mikopo Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki akizungumza wakati DCB ikikutana na madiwani, wakurugenzi na wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Jiji la Ilala kuwaelea maendeleo ya benki mipango na mikakati ya baadae katika kuhakikisha benki yao hiyo inaendelea kukua na kupata faida.
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saad Khimji (kulia), akizungumza katika mkutano huo.

Tuesday 20 July 2021

BAA ZAENDELEA KUCHANGAMKIA FURSA YA SBL ‘RAISE THE BAR’ AU 'TUNYANYUKE PAMOJA’

Faith Mpawa, mmoja kati ya wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti akimwelekeza mmoja wa wafanyakazi wa Baa ya Meridian iliyopo Vijana Kinondoni namna ya kujisajili katika Mpango wa kuzisaidia Baa kunyanyuka maarufu kama "Raise the Bar" unaofadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.


Mwakilishi wa kampuni ya Bia ya Serengeti alimwelekeza mmoja wa wateja namna ambavyo anaweza kujaza fomu kwa ajili ya kuomba kunufaika na mradi wa kunyanyua baa baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa Corona unaojulikana kama "Raise the Bar".
Hassan Matata akimwelekeza mmoja wa wafanyakazi wa MK bar iliyopo jijini Dar es Salaam namna ya kujaza fomu ya maombi kwa ajili ya kuomba misaada mbali mbali inayotolewa na Kampuni ya SBL kupitia mpango wa kusaidia baa kunyanyuka maarufu kama Raise the Bar.

Mmoja kati ya wateja waliofika katika banda lililowekwa kwa ajili ya kuwaelekeza wenye mabaa namna ya kujisajili katika mpango wa kuyasaidia mabaa kunyanyuka unaojulikana kama "Raise the Bar" au Tunyanyuke Pamoja akipata maelekezo kutoka kwa wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.

RAIS WA ZANZIBAR AVUTIA WASHIRIKI ‘NMB 5K RUN 2021’

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi na Mke wake Mama Mariam, Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita (wa kwanza kulia) na Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (kushoto) wakishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB zilizofanyika jumapili visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi na Mke wake Mama Mariam na Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedcto Baragomwa (kushoto) wakishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB. Mbio hizo zilifanyika visiwani Zanzibar juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman (kushoto) na Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedcto Baragomwa (katikati) wakishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB na kufanyika juzi visiwani Zanzibar.
Watoto nao pia walishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB na kufanyika juzi visiwani Zanzibar.
Watu mbali mbali walishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB na kufanyika juzi viziwani Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza mamia ya wakimbiaji walioshiriki mbio za kilomita 5 za 'NMB 5K Run 2021,' zilizodhaminiwa na Benki ya NMB, ambapo ushiriki wake uliwavutia wengi zaidi miongoni mwa waliojitosa katika Zanzibar International Marathon 2021

NMB 5K Run 2021 zilikuwa ni sehemu ya Zanzibar International Marathon - mbio zilizofanyika chini ya kaulimbiu ya 'Tunakuza Uchumi wa Bluu Kupitia Michezo Zanzibar, zilizoanzia Ngome Kongwe na kuishia Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ambako Dk. Mwinyi alikuwa mmoja wa waliokimbia kilomita 5.

NMB ilidhamini kilomita 5 kwa Sh. Milioni 35, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Zanzibar katika kuhamasisha na kukuza utalii, kukuza Uchumi wa Bluu na kuchagiza jamii kudumisha utamaduni chanya wa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa.