Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 28 February 2020

CRDB BANK PLC BOARD MEMBER VACANCIES

KUONGEZA TIJA KWENYE SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO KWA MAENDELEO YA VIWANDA

Mkuu wa Kitendo cha Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mikakati ya benki hiyo katika kuendelea kuwasaidia wakulima katika uzalishaji bora. Hayo ameyasema wakati wa Mkutano wa wadau katika kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Afisa Masoko Tawi la NBC Samora, Dustane Lipawaga (mwenye tisheti Nyekundu), akizungumza na baadhi ya washiriki wa walipotembelea banda la NBC Tanzania wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC. 
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) akikata utepe kuashiria kuzindua kitabu chenye muongozo wa sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akichangia mada wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC. wapili kulia ni Waziri Ufugaji na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina (Mb) wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa pamoja na Viongozi wa Maendeleo ya kilimo.
27 Februari 2020 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema kuwa itaendelea kushirikiana na kuwasaidia wakulima hasa katika kuwapatia ujuzi na mbinu mbalimbali za kuboresha mazao yao kwa lengo la kuhimarisha sekta hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda, Mkuu wa Kitendo cha Wafanyabiashara wadogo na wa kati benki ya NBC, Evance Luhimbo alisema benki hiyo imekuwa mbele kuwasaidia wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.

Alisema mikakati yao ya mbeleni kwenye kilimo ni kuhakikisha wanaisaidia sekta hiyo kwa asilimia kubwa na kwa kuanzia wameaandaa nyaraka inayoelezea ni kwa jinsi gani mtu anaweza kumsaidia mkulima katika mazao yake na mtaji wake.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL) YATOA DARASA LA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA BODA BODA SINGIDA

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Singida, Edson Mwakihaba (kushoto) na Meneja Uhusiano na Serikali wa SBL, Neema Temba (kulia) wakikabidhi makoti ya usalama barabarani kwa Mwenyekiti wa bodaboda Singida Mjini, Abdul Misigo kwenye hafla ya kampeni ya SBL ‘Usinywe na kuendesha chombo cha moto’ iliyofanyika leo stendi ya mabasi mjini Singida.
Picha ya pamoja kutoka kushoto ni Mkuu wa Mauzo SBL Singida, Godwin Urassa , RTO Singida, Edson Mwakihaba, Meneja Uhusiano na Serikali wa SBL, Neema Temba, na Mkaguzi wa Magari mkoa Singida, Hassan Hamis Hassan mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya SBL ‘Usinywe na kuendesha chombo cha moto’ iliyofanyika leo stendi ya mabasi mjini Singida.
Picha ya pamoja kutoka kushoto Anorld Kisukuli Mkurugenzi wa kanda ya kati Dodoma wa chama cha kutetea Abiria Tanzania, RTO mkoa wa Singida Edson Mwakihaba na Neema Temba.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Singida, Edson Mwakihaba akigawa makoti ya usalama barabarani kwa madereva wa boda boda mjini Singida kwenye kampeni ya ‘Usinywe na kuendesha (Don’t Drink and Drive) kutoka kampuni ya Serengeti Breweries SBL.
RTO Mkoa wa Singida Edson Mwakihaba, Meneja Uhusiano na Serikali wa SBL, Neema Temba wakiwa na madereva wa Bodaboda mkoa wa Singida katika mafunzo ya ‘Usinywe na kuendesha (Don’t Drink and Drive) kutoka kampuni ya Serengeti Breweries SBL.

Singida, Februari 28, 2020 – Ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono Serikali katika kupambana na ajali za barabarani, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetoa darasa juu ya masuala ya usalama barabarani kwa waendesha boda boda mkoani Singida chini ya kampeni yake ya ‘Usinywe na kuendesha chombo cha moto’

Kampeni hiyo ya nchi nzima, inalenga kuwaelimisha watumiaji wa barabara na haswa madereva juu ya unywaji wa kistaarabu ikiwa ni hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kutokomeza ajali zinazosababishwa na unywaji usio wa kistaarabu.

Katika kipindi cha mwaka mmoja kampeni hii imefanyika katika mikoa nane ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Dodoma, Tanga, Arusha, Moshi na Iringa ikiwafikia zaidi ya watu 100,000.


UNLOCKING THE POWER OF GEOSPATIAL DATA IN MARKET GROWTH: FINANCIAL SECTOR REGULATORS LAUNCH THE FINANCIAL SERVICES REGISTRY

Bank of Tanzania (BOT) Governor, Prof. Florens Luoga (third left) presses a button to launch the Financial Services Registry (FSR) in Dar es Salaam yesterday. Others are BOT Deputy Governor, Dr. Bernard Kibesse (second left), DCB Commercial Bank CEO, Godfrey Ndalahwa (extreme left), Vodacom Tanzania Director of M-Commerce, Epimack Mbeteni (third right) and Tanzania Co-operative Development Commission (TCDC) Deputy Registrar, Collins Benedict (second right). 
Bank of Tanzania Governor Prof. Florens Luoga (centre) in group photo with from left, BOT Director of National Payment Systems, Bernard Dadi, DCB Commercial Bank CEO, Godfrey Ndalahwa, Financial Sector Deepening Trust (FSDT) CEO, Sosthenes Kewe, BOT Deputy Governor, Dr. Bernard Kibesse, Vodacom Tanzania Director of M-Commerce, Epimack Mbeteni and Tanzania Co-operative Development Commission (TCDC) Deputy Registrar, Collins Benedict. 
A cross section of stakeholders follow proceedings during the launch event.
Regulators of the financial sector in Tanzania supported by the Financial Sector Deepening Trust (FSDT) on February 27, 2020 launched the Financial Services Registry (FSR) which aims at mapping all financial services access points in the country.

FSR is a sustainable registry, that will map all financial services access points countrywide by capturing their geo-locations and type of services offered with the objective to unlock the power of geo-spatial data as a tool for business intelligence, decision making and strategic planning.

The regulators led by the Bank of Tanzania include the Tanzania Co-operative Development Commission (TCDC), Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) and the Capital Markets and Securities Authority (CMSA).

Bank of Tanzania and Chairperson of the National Council for Financial Inclusion, Prof. Florens Luoga, officially launched the FSR system by amplifying that: “Data is the new oil” and that “those who can use it effectively and for their benefit will reap its fruits and flourish.”

He said the financial services registry will provide the engine to consolidate and unlock the power of data to encourage growth, innovation and collaboration within the financial sector of Tanzania, which is ready for this new decade of digitization, industrialization and connectivity.

KANZIDATA YA KUDUMU YA WATOA HUDUMA ZA FEDHA YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga, (wa tatu kushoto), akibofya kitufe maalum wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dk. Bernard Kibesse, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa. Wengine kutoka kulia ni Meneja Usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Bima (TIRA), Paul Abdiel, Naibu Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Collins Benedict na mwakilishi wa Chama Cha Wamiliki wa Makampuni ya Simu nchini, Epimack Mbeteni ambaye ni Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa. 
Meza Kuu ikifurahia jambo mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha uliofanyika jijini Dar Es Salaam jana.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga, (kushoto), akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa,  Bernard Dadi, Mkurugenzi Mkuu wa FSDT, Sosthenes Kewe (wa tatu kushoto) na Mwakilishi wa Chama Cha Wamiliki wa Makampuni ya Simu nchini, Epimack Mbeteni.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga, (kulia), akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha. Katikati ni Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dk. Bernard Kibesse na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (katikati), akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha. Kulia ni Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bernard Dadi na kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dk. Bernard Kibesse.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya huduma jumuishi za kifedha Profesa Florens Luoga amesema kuwa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha litaleta mashine ambayo itakusanya na kufungulia nguvu ya takwimu ili kuhimiza ukuaji, ubunifu na ushirikiano ndani ya sekta ya fedha nchini ambayo ipo tayari kwa ajili ya muongo huu uliotawaliwa na digitali, viwanda na muunganisho.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha iliyobeba kauli mbiu ya "Takwimu ni Mafuta Mapya" na kuwataka watoa huduma kuitumia kauli hiyo ipasavyo na kwa manufaa yenye kuleta tija.

Prof. Luoga amesema kuwa ufunguzi huo wa daftari la nguvu ya kitakwimu za kijiografia kwenye ukuaji wa soko uliowakutanisha wasimamizi wa sekta ya fedha wa watoa huduma za kifedha (FSR) ni endelevu huku mlengo mkuu ukiwa ni kuonesha mahali ambapo vituo vinavyotoa huduma za kifedha nchini.


Thursday 27 February 2020

KIVUMBI CHA LIGI KUU YA UINGEREZA KINARUDI TENA WIKIENDI HII!

Kivumbi cha Ligi kuu ya Uingereza kinarudi tena wikiendi hii! Je nani kupanda nani kushuka?

Na @dstvtanzania inazidi kukusogezea soka hili mpaka nyumbani kwako, huku wakinogesha kwa ofa ya Tia Kitu Pata Vituuz (Ofa hii ni mpaka 29 Februari 2020) ambapo mteja wa kifurushi cha Family sasa, ukilipia sh. 29,000 tu, utapandishwa kwenda kifurushi cha Compact kwa mwezi mzima ambapo utafaidi michuano hii bila gharama za ziada.

Vigezo na masharti kuzingatiwa

#DStvStepUp

BENKI YA NBC YAZINDUA KLABU YA BIASHARA TANGA, YATOA MAFUNZO YA KIBIASHARA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanga, Daudi Mahej (wa pili kulia), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru kuashiria uzinduzi rasmi wa Club ya Biashara katika Mkoa wa Tanga. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Wadogo na Wa Kati wa NBC, Evance Luhimbo (kulia), pamoja na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Tanga Asia Chambega. Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru akizungumza wakati wa Mafunzo ya Biashara kwa wafanya Biashara wadogo na wa kati wa Mkoa wa Tanga wakati wa Uzinduzi wa Club ya Biashara Mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru (kulia), akishikana mikono na Afisa Mkuu Msimamizi wa kodi TRA Makao Makuu, Julius Mjenga baada ya kumaliza mafunzo ya biashara yalioandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanya Biashara wa Mkoa wa Tanga. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe.
Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakifurahi baada ya kufanyika uzinduzi wa Club ya biashara Mkoa wa Tanga.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua klabu ya biashara Katika mkoa wa Tanga yenye lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati pamoja ili kupeana fursa, mbinu na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusi biashara zao.

Aidha benki hiyo imeendesha mafunzo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati kwa lengo pia la kuwaongezea uwezo, uelewa na ubunifu katika ufanyaji wa biashara zao.

BENKI YA NMB YAJITOSA KWENYE UDHAMINI WA BIMA MARATHON 2020

Meneja Mwandamizi wa Bima NMB, Martine Massawe (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Sh milioni 35 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa African Digital Banking Summit Limited, Baraka Mtavangu kwa ajili ya NMB Bima Marathon itakayofanyika tarehe 28 Machi 2020 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa NMB Jogging Club, Elifadhili Mramba.
Benki ya NMB, imetangazwa kuwa Mdhamini Mkuu wa Mbio za Bima Marathon 2020, zinazotarajiwa kufanyika Machi 28 jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Kampuni ya African Digital Banking Summit.

Kwa udhamini huo, mbio hizo zinazoenda kufanyika kwa mara ya pili mfululizo, zitatambulika kwa jina la NMB Bima Marathon 2020, ambazo zitahusisha mbio za kilomita 21, kilomita 10 na kilomita 5.

NMB imedhamini mbio hizo kwa kitita cha Sh. Milioni 35, ambako hafla ya NMB kutangaza udhamini wake huo katika mashindano hayo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya udhamini, Meneja Mwandamizi wa Bima wa NMB, Martine Massawe, alisema wamevutiwa kudhamini Bima Marathon kutokana na mlengo wake.

TELECOMS ARE REVOLUTIONIZING TANZANIA’S HEALTH SECTOR

Last week, Dar es Salaam’s Muhimbili hospital and the University of Oxford announced a project to help improve healthcare provision in Tanzania.

The project will include a TZS13.5 billion study to help Tanzania develop the next generation of health technologies, including artificial intelligence and digital pathology. Investments such as this are helping to ensure that Tanzanian hospitals can continue to deliver high quality care by using innovative health technology.

In recent years, however, the application of mobile internet and communication technology has also emerged as one of the major trends which is serving to transform the care provision in Tanzania.

One example is the use of mobile enabled services applications, in what is known as m-health. These services are helping patients to research information online, share their symptoms and identify potential treatment options.

Wednesday 26 February 2020

BENKI YA NBC YAFANIKIWA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU BILA MALIPO KWA WATU MILIONI 3.3

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndungulile akisalimiana na Afisa Masoko Tawi la NBC Samora, Dustane Lipawaga akiwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya Kibiashara ya NBC, William Kallaghe (kulia) na Meneja Huduma za Jamii, Irene Peter wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yaliyofanyika hivi karibuni yakihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndungulile (wa watu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Benki ya Biashara ya NBC, William Kallaghe (kulia), wengine ni Afisa Masoko Tawi la NBC Samora, Dustane Lipawaga (kushoto), na Meneja Huduma za Jamii, Irene Peter wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la Mennonite, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Askofu Nelson Kisare akielezea jambo kwa kwa Meneja Uhusiano wa Benki ya Kibiashara ya NBC, William Kallaghe (wa pili kulia), wengine ni Afisa Masoko Tawi la NBC Samora, Dustane Lipawaga (kulia) na Meneja Huduma za Jamii Irene Peter (kushoto) wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yaliyofanyika hivi karibuni. 

JOB VACANCIES AT CRDB BANK PLC - SENIOR INTERNAL AUDITORS

JOB VACANCIES

CRDB Bank Plc is inviting applications from qualified and experienced candidates to fill the vacant positions existing in the Department of Internal Audit.

The Bank seeks to recruit highly competent, self-motivated and professional individuals to fill the following positions:
  1. Senior Internal Auditors- ICT Audits (2 Positions)
  2. Senior Internal Auditors (2 Positions)
Mode of Application & Closing Date

Interested candidates who meet the above criteria should submit an Application Letter accompanied with a detailed up to date CV with three work-related referees addressed to the below email with a ​clear subject of the position applied for not later than 3r​d March 2020. Hard copies will not be accepted.

Email: career.career@crdbbank.com

APPOINTMENT OF RESPIGE KIMATI AS MANAGING DIRECTOR, MKOMBOZI COMMERCIAL BANK PLC


JOB VACANCY AT NMB BANK PLC - SENIOR SPECIALIST; CARD GOVERNANCE & COMPLIANCE

Job Purpose
To provide the overall Card governance, controls, fraud prevention and compliance process; Derive as much value from Card Business by preventing Fraud and creating frictionless payment experiences.

Main Responsibilities
  • Provide leadership in collaboration with other senior managers and business partners to develop and implement strategies that effectively manage financial crime risk across the Cards lines of business
  • Oversee the fraud risk management function across the card lines of business, ensuring regulatory compliance and compliance with other relevant internal and external standards and requirements
  • Ensure teams understand regulatory and compliance requirements as prescribed for the function, and provide recommendations and implement actions to ensure adherence as required 
  • Identify Card business control risks and gaps 
  • Be an active player in fraud management forums 
  • Manage Card fraud risk and minimize losses through monitoring, reporting and taking appropriate action
  • Meet regularly with senior internal business partners and lines of business executives to track and address operational risks related to card business 

ANNOUNCEMENT OF INTENTION TO PUBLISH LIST OF MEMBERS OF THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS


TTCL AND TPRI AGREE ON INNOVATIVE DIGITAL VERIFICATION OF PESTICIDES

Tanzania Telecommunications Corporation Limited (TTCL), Acting Executive Director, Kezia Kutamboi (right) exchanges a signed contract with Tropical Pesticides Research Institue (TPRI) Director General, Dr. Margaret Mollel during the lauch of farmers’ digital verification for pesticides known as T-Hakiki in Dar es Salaam yesterday.
Tanzania Telecommunications Corporation Limited (TTCL), Acting Executive Director, Kezia Kutamboi (right) displays the signed contract with Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) Director General, Dr. Margaret Mollel during the lauch of farmers’ digital verification for pesticides known as T-Hakiki in Dar es Salaam yesterday. 
Tanzania Telecommunications Corporation Limited (TTCL), Acting Executive Director, Kezia Kutamboi (right), Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) Director General, Dr. Margaret Mollel (left) and Quincewood's Director of Business which oversees the digital electronic pesticide system, Fatma Fernandes (center) during the lauch of farmers’ digital verification for pesticides known as T- Hakiki in Dar es Salaam yesterday.
By Staff Reporter

Tanzania Telecommunications Corporation (TTCL) and Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) have signed an agreement for the launch of an innovative digital verification solution of pesticide known as T-Hakiki.

T-Hakiki platform is using technology to reimagine agriculture in Tanzania by providing accessible, scalable solution for smallholder famers whilst bundling verification with the inputs farmers already use, in this case pesticides.

Speaking to the reporters in Dar es Salaam yesterday on the occasion of signing the agreement, TTCL Acting Executive Director, Kezia Katamboi said that T- Hakiki will significantly impact digitization of agriculture and safeguard the lives of many farmers whilst driving financial inclusion efforts in Tanzania.

Tuesday 25 February 2020

BENKI YA CRDB YAPONGEZWA KUISAIDIA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR UKUSANYAJI WA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 25 SEKTA YA UTALII


Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid akiwasili katika Semina kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyoandaliwa na Benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alipokuwa akimpokea.
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwasilisha mada wakati wa Semina na Baraza la Wawakilishi iliyoandaliwa na Benki hiyo wikiendi hii. Semina hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Idd akimpongeza Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa utayari wa Benki hiyo kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi ya maendeleo wakati wa Semina Maalum iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Hoteli ya Verde, Zanzibar Wikiendi hii.
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid akifuatilia mada katika Semina hiyo. Kushoto ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akielezea ushiriki wa Benki hiyo katika kusaidia jamii Zanzibar kupitia miradi ya CSR.
Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akifafanua jambo wakati wa Semina hiyo.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini mada katika semina hiyo.
Wageni waalikwa wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Wageni waalikwa wakifualtiia kwa makini mada.
Waziri wa Afya SMZ, Hamad Rashid akichangia kuhusu uwekezaji katika huduma za afya kwa kujenga hospitali za kisasa ambapo alisema ni chachu katika kuimarisha nguvu kazi ya taifa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara SMZ, Mhe. Hassan Hafidh Khamis akichangia mada wakati wa Semina hiyo huku akiitaka Benki ya CRDB kuwekeza zaidi katika viwanda kwani vitasaidia kuongeza ajira hususan kwa vijana. 
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tauhida Gallos akitoa mchango wake kuhusu uwezeshaji wa wakinamama wajasiriamali wakati wa Semina hiyo. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa jailli ya Bonanza kati ya Benki hiyo na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi lililofanyika wikiendi hii.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa kinara katika kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kukusanya mapato katika sekta ya Utalii. Mwaka jana Benki ya CRDB kupitia mifumo yake ya kidijitali iliweza kukusanya kodi na tozo kwa watalii na wageni zinazofikia dola za kimarekani milioni 12 kutoka dola laki 4 mwaka 2014 ambapo ni ongezeko la takribani asilimia 3000.

Akizungumza katika Semina maalum iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na viongozi wengine wa taasisi za Serikali Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid, alisema Benki ya CRDB imekuwa kiungo muhimu katika uchumi wa Zanzibar hususani katika kuweka miundo mbinu thabiti ya huduma za kifedha kwa Wazanzibari na wageni.

“Benki ya CRDB ni mshirika muhimu katika uchumi wa Zanzibar, hususan kipindi hiki tukiwa tunakwenda kukamilisha Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020. Serikali inafurahishwa sana na namna ambavyo tumekuwa tukishirikiana na Benki hii katika kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea,” alisema Mhe. Zubeir Maulid.