Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 28 February 2020

KUONGEZA TIJA KWENYE SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO KWA MAENDELEO YA VIWANDA

Mkuu wa Kitendo cha Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mikakati ya benki hiyo katika kuendelea kuwasaidia wakulima katika uzalishaji bora. Hayo ameyasema wakati wa Mkutano wa wadau katika kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Afisa Masoko Tawi la NBC Samora, Dustane Lipawaga (mwenye tisheti Nyekundu), akizungumza na baadhi ya washiriki wa walipotembelea banda la NBC Tanzania wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC. 
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) akikata utepe kuashiria kuzindua kitabu chenye muongozo wa sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akichangia mada wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Februari 27-28 unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC. wapili kulia ni Waziri Ufugaji na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina (Mb) wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa pamoja na Viongozi wa Maendeleo ya kilimo.
27 Februari 2020 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema kuwa itaendelea kushirikiana na kuwasaidia wakulima hasa katika kuwapatia ujuzi na mbinu mbalimbali za kuboresha mazao yao kwa lengo la kuhimarisha sekta hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda, Mkuu wa Kitendo cha Wafanyabiashara wadogo na wa kati benki ya NBC, Evance Luhimbo alisema benki hiyo imekuwa mbele kuwasaidia wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.

Alisema mikakati yao ya mbeleni kwenye kilimo ni kuhakikisha wanaisaidia sekta hiyo kwa asilimia kubwa na kwa kuanzia wameaandaa nyaraka inayoelezea ni kwa jinsi gani mtu anaweza kumsaidia mkulima katika mazao yake na mtaji wake.

"Nyaraka hii imejikita katika kilimo tu ambapo tunaangalia kwa njia gani tunaweza kumpatia huduma nzuri mkulima na pia kuangalia tunaweza kumsapoti mkulima na kumpatia ujuzi na utaalamu pamoja na kushirikana na Wizara katika mambo mbalimbali.

Alisema mkakati huo wa kuwasaidia wakulima ni endelevu hasa ukizingatia benki hiyo imekuwepo nchini kwa miaka 52 sasa na wamekuwa wakiwasapoti wakulima hasa katika kuwapatia mbinu mbalimbali za kilimo bora na chenye tija, kuwapatia ushauri juu ya kuendesha shughuli zao za kifedha."Tunaowataalamu wengi ambao tunaendelea kuwatumia kuwasaidia wakulima lakini NBC tunashirikiana na PASS ambao kazi yao kubwa kuwawekea ulinzi na usalama wa mazao kwa wakulima," alisema

Evance Luhimbo alimalizia kwa kusema mtu akimsapoti mkulima atakuwa ameweza pia kusapoti masuala ya viwanda ambayo ndio ajenda kubwa nchini.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema ili kufikia uchumi wa kati katika sekta ya Viwanda, mahitaji ya wakulima, wavuvi na wafugaji hayawezi kutekelezwa kwa bajeti ya serikali pekee bali wadau wakubwa wajitokeze kuwekeza.

Bashe aliseema katika sekta ya Kilimo kumekuwa na changamoto kubwa ya bajeti, kwani haiwezi kutosheleza kwenye kuleta maendeleo ya kilimo na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Kuhusu National Bank of Commerce (NBC)
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.

Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa ka;ka tanzu tatu tofau;: NBC Holding Corpora;on, Na;onal Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.

Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopa;kana ka;ka maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima.

Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us NBC_Marke8ngDepartment@nbc.co.tz

No comments:

Post a Comment