Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 30 September 2022

UNISURE GROUP, PHOENIX OF TANZANIA (PART OF MUA) AND SMART APPLICATIONS INTERNATIONAL EXTEND THEIR STRATEGIC PARTNERSHIP INTO TANZANIA

From right to left; Robert Kalegeya - Head of Business Development, Underwriting and Reinsurance at Phoenix Assurance, Daniel Van Der Merwe - Head of International Private Medical Insurance at Unisure and Grace Gathuri - Tanzania Country Manager at Smart Applications.

29 September 2022, Dar es Salaam – Today marked another important milestone for the insurance industry as The Unisure Group, Phoenix of Tanzania Assurance Co. Ltd (PTAL), (Part of MUA) and Smart Applications International extended their official strategic partnership into Tanzania at a media launch in Dar es Salaam.

Industry leaders, regulators, key stakeholders and members of the media came together to learn more about how this partnership in East Africa and the Indian Ocean Islands, which was first launched in Nairobi, Kenya, in May, will help transform healthcare in the region.



“We are extremely proud to be adding the Tanzanian market to the existing partnership countries. Tanzania is a key market in terms of growth opportunities in medical insurance in particular,” said The Unisure Group’s Deputy Executive Chairman, Stephen Conway. “This partnership is unique in that three independent organisations – one insurance company, an international administration and assistance provider, and a medical services facilitator – have agreed to partner on projects that will provide access to quality healthcare across multiple African countries in a fully regulated way. We’re incredibly excited for the long-term collaborations and new business opportunities that lie ahead for our Umatter International Private Medical Insurance (IPMI) plans and look forward to adding additional countries to the four existing partnership countries.”

EPL INARUDI KWA KISHINDO WIKIENDI HII NDANI YA DStv


#EPL inarudi kwa kishindo wikiendi hii ndani ya chaneli za michezo SuperSport pekee!

Jumamosi London Derby ya kibabe kati ya Arsenal na Tottenham je Arsenal wataweza kujimilikisha Derby?

Lipia kifurushi chako cha Compact mapema kwa kupiga *150*53#

#msimuwasokalakibabe


 

AZANIA GROUP YAZINDUA UNGA WA NGANO KWA AJILI YA MATUMIZI YA CHAKULA ILI KUONGEZA THAMANI, KULETA SULUHISHO, UTOFAUTI NA KURAHISISHA HUDUMA KWA WATUMIAJI WAKE



29 Septemba 2022 - Azania Group, moja ya chapa kubwa na maarufu ya bidhaa za chakula, imezindua unga mpya wenye thamani na ubora wa hali ya juu na wenye ushawishi kwa watumiaji wake kutumia unga mweupe, laini na wenye kudumu kwa matumizi ya muda mrefu na kukidhi aina mbalimbali za mapishi. Azania Group imezindua chapa yake mpya ya unga iliyopewa jina la AZANIA - PREMIUM HOME FOUR (PHF), Unga wa Ngano ambao sio tu safi lakini pia una ubora wa kimataifa ambao utakidhi mahitaji ya watumiaji. Sherehe ya uzinduzi wa bidhaa hiyo imefanyika Alhamisi 29 Septemba 2022 katika maeneo ya Hellenic Greek Club, Dar es Salaam.


"Unga wetu mpya wa Azania PHF unakuja kama sehemu ya utafiti uliofanywa na kugundua uhitaji wake hivyo ili kuleta suluhu na kuleta utofauti kwenye soko na urahisi kwa watumiaji, Azania tumeonelea vyema kuja na bidhaa hii kwani mara nyingi watu wengi wanabanwa sana na muda na kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kama vile Maandazi, Chapati na vitafunio vingi zaidi na vya aina mbalimbali hivyo bidhaa yetu hii itatoa nafasi ya kuzalisha vitafunio vingi zaidi kuliko vile vilivyozoeleka. ” Alisema Bw Joel Laiser Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group.

Thursday 29 September 2022

BENKI YA NBC YAZINDUA MSIMU WA PILI WA KAMPENI YA "VUNA ZAIDI NA NBC SHAMBANI" MAHUSUSI KWA WAKULIMA WA KOROSHO MIKOA YA MTWARA NA LINDI

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya (katikati) akijaribu ubora wa moja ya matrekta ambayo ni miongoni mwa zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (wa tatu kulia) pamoja na wadau wengine wa zao korosho mkoani Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya (wanne kushoto) akioneshwa moja ya simu janja (smart phone) na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke (wa tatu kulia) ikiwa ni sehemu ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa washindi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wadau wengine wa zao korosho mkoani Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo.
Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo.
Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo.
Meneja wa benki ya NBC Tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya (Katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (wa tatu kushoto walioketi), viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo.
Wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani leo.

Mtwara: Septemba 29, 2022: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua msimu wa pili wa kampeni yake maalum kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi inayofahamika kama 'Vuna zaidi na NBC Shambani' ikilenga kuunga mkono na kufanikisha adhma ya serikali ya kuzalisha tani 700,000 za zao hilo kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameongoza hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani humo leo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika maofisa wa benki wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa NBC Bw Elibariki Masuke.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Bw Kyobya alisema imekuja wakati muafaka kwa kuwa inakwenda sambamba na mpango wa serikali wa kuhakikisha sekta ya kilimo inachangia pato la taifa kwa asilimio 10 ifikapo mwaka 2030.

“Na ndio sababu nawapongeza sana Benki ya NBC kwa mkakati huu ambao hapo tu kimasoko bali pia unaunga mkono jitihada za serikali kukuza sekta hii muhimu na pia inalenga kumkomboa mkulima. Wito wangu kwa wakulima wa korosho mkoa wa Mtwara na Lindi naomba sana tuwaunge mkono NBC kwenye hili,’’ alisisitiza.

STANBIC BANK LAUNCHES NEW PROPOSITION FOR SMEs

Stanbic Bank Head of Business and Commercial Clients, Fredrick Max (right) speaks during the launch of Stanbic Bank's exclusive value proposition for Small and Medium enterprises (SMEs) dubbed ‘Mpambanaji’ which aims at promoting financial inclusion by empowering SMEs to utilise the country's investment opportunities and increase their regional and global competitiveness in Mwanza. Also in the picture is Stanbic Bank's Head of Consumer and High Net Worth Clients, Omari Mtiga (centre) and Head of Incubator, Kai Mollel (left).

Dar es Salaam, 28th September 2022 - Stanbic Bank Tanzania, has launched an exclusive value proposition for Small and Medium enterprises (SMEs) dubbed ‘Mpambanaji’, with the theme: Tunakuwezesha Kukuza Biashara Yako (we empower you to grow your business). The New solution aims at promoting financial inclusion by empowering SMEs to utilise the country's investment opportunities and increase their regional and global competitiveness.

The proposition was unveiled through a campaign that kicked off with a press conference and a workshop for SMEs at the Goldcrest hotel in Mwanza.

The Mpambanaji proposition comprises a full suite of solutions including; SMEs-centred accounts for individuals, groups and SACCOS - Mpamabanaji account, Vikundi and Saccos, an incubator program for capacity-building, Borderless Banking, Vehicle Asset Finance (VAF), Insurance services, Biashara Exchange, Africa China Trade Solution, as well as Agency Banking solution - Stanbic Wakala-with over 500 agents, increasing the bank's footprint in the country.

Speaking about the proposition during a press conference, the bank’s Head of Business and Commercial Clients, Frederick Max, stressed that Mpambanaji aims to solve the challenges that have been hindering business from transitioning from informal to formal businesses.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATOA MAFUNZO MAALUMU YA KUONGEZA KIPATO KWA WATU WENYE ULEMAVU

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde (watatu kulia walioketi) akiwa katika uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili (28-29 Septemba) ya kilimo biashara kwa watu wenye ulemavu ya Foundation of Disabilities Hope (FDH) na yaliyodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti mkoani Dodoma. Wa kwanza kulia ni, Michael Salali (Mwenyekiti wa FDH), akifuatiwa na John Wanyancha (Mkurugenzi Mahusiano ya Umma wa SBL). Wa kwanza kushoto ni Neema Kweka (Muwakilishi ofisi ya Rais, TAMISEMI) na akifuatiwa na Yustina Munishi (Mkuu wa Divisheni ya kilimo mjini Dodoma). Waliosimama nyuma ni wakufunzi wa Kilimo biashara.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde akizungumza na watu wenye ulemavu (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili (28-29 Septemba) ya kilimo biashara kwa watu wenye ulemavu ya Foundation of Disabilities Hope (FDH) na yaliyodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde (watatu kulia walioketi) akiwa katika uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili (28-29 Septemba) ya kilimo biashara kwa watu wenye ulemavu. Wa kwanza kulia ni, Martin Kihumbe (Mkurugenzi wa FDH), akifuatiwa na John Wanyancha (Mkurugenzi Mahusiano ya Umma wa SBL). Wa kwanza kushoto ni Neema Kweka (Muwakilishi ofisi ya Rais, TAMISEMI) na akifuatiwa na Yustina Munishi (Mkuu wa Divisheni ya kilimo mjini Dodoma).

Dodoma, Septemba 28, 2022 - Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imedhamini mafunzo ya siku mbili ya mafunzo ya kujiongezea kipato kupitia kilimo kwa watu wenye ulemavu katika jitihada za kuchochea ukuaji uchumi shirikishi nchini. Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano baina ya SBL na shirika liitwalo, Foundation of Disabilities Hope (FDH).



Mafunzo hayo yameanza tarehe 28 Septemba mjini Dodoma yakishirikisha zaidi ya watu 100 wenye ulemavu watakaopata mafunzo ya wa kilimo biashara, ujasiriamali na ujuzi wa masuala ya fedha ili kuwasaidia kuingiza kipato zaidi katika shughuli zao za kila siku za kiuchumi.



Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya dhamira yao ya kukuza kasi ya uchumi nchini Pamoja na kudumisha mpango wao wa miaka kumi ya kujenga jamii shirikishi na endelevu.



MRADI WENYE THAMANI YA DOLA MILIONI 300 UNATARAJIWA KUIPELEKA TANZANIA KWENYE KILELE CHA BIASHARA AFRIKA


Dar es Salaam; Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza, wamealikwa kutumia fursa katika mradi mpya wa kiuchumi wa Mkinga. Mradi huo wa mamilioni ya dola utaipeleka Tanzania katika kilele kipya cha biashara. Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Mkinga unatarajiwa kuleta mabadiliko katika maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano barani Afrika kwani mradi huu ni kama lango la zaidi ya nchi 18.

Mradi huo wenye thamani ya Dola Milioni 300 sawa na Sh.699 Bilioni, utaleta umahiri wa kiuchumi barani Afrika utakaofikia ekari 650 zinazoongoza maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Afrika. Mradi huo una teknolojia za kiwango cha kimataifa kama Akili Bandia yaani Artficial Intelligence (AI), Biashara ya Mtandaoni (E-commerce) na biashara ya kidijitali na kuifanya kuwa ya kipekee katika eneo hilo.


Mradi huu unalenga kujenga miundombinu muhimu kwa Mkinga ili kuimarisha uchumi na kujenga msingi wa maendeleo kwa kuzingatia mikataba kati ya Mataifa ya Afrika kama vile AfCFTA, EAC, SADC, AGOA na mikataba mingine mingi, alisema Shady El Zeki, Mjumbe wa Bodi kutoka Zworld. 

Wawezeshaji hao wamethibitisha kuwa hadi sasa jumla ya wawekezaji watano kutoka mataifa mbalimbali wameonyesha nia ya kuwekeza fedha, ikiwemo Brazil, Misri, Tunisia, Bulgaria, GCC, Ufilipino na India. Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika. 

Tuesday 27 September 2022

NMB YASHINDA TENA TUZO YA BENKI BORA WATEJA BINAFSI

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati), Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya Serikali wa Benki ya NMB, Amanda Feruzi (kulia) na Meneja Mwandamizi wa Mahusianao ya Biashara ya Nje ya Nchi wa Benki ya NMB, Lucy Kimei (kushoto) wakifurahia tuzo ya Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara Tanzania kwa mwaka 2022 kutoka jarida la Global Banking and Finance Mara baada ya Hafla ya Ugawaji Tuzo uliofanyika jijini London nchini Uingereza hivi karibuni.

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Benki ya NMB imeshinda tuzo ya benki kiongozi wa kuwahudumia wateja binafsi nchini kutokana na ubora wa huduma zake kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha za umma wa walio wengi.


NMB ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora ya Wateja Binafsi Tanzania kwa mwaka 2022 kwenye hafla ya tuzo za Global Banking and Finance (GBAF) Awards zilizofanyika huko London, Uingereza.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2011 na jarida la Global Banking & Finance Review lenye wasomaji zaidi ya milioni tatu ulimwenguni kote na ambalo shughuli yake kubwa ni kuangazia matukio na maendeleo ya kifedha duniani.



Akizungumza kwenye hafla ya kuwazawadia washindi wa tuzo za mwaka huu, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw Filbert Mponzi, alisema ushindi wa benki hiyo ni kutambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wateja na kulihudumia kikamilifu taifa kwa ujumla.

“Kwetu sisi NMB, mteja na huduma jumuishi za fedha ndiyo msingi wa shughuli zetu zote. Tunatoa huduma nafuu za kifedha kwa wateja zaidi ya milioni tano Tanzania nzima,” Bw Mponzi alibainisha kwenye hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo.

TANZANIA NA UAE ZATIA SAINI MKATABA WA KUTOTOZA KODI MARA MBILI KATI YA NCHI HIZO

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussaini, wakionesha Mkataba wa makubaliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, Mjini Dubai, Falme ya nchi za Kiarabu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussaini, wakisaini Mkataba wa makubaliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, Mjini Dubai, Falme ya nchi za Kiarabu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussaini (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, Mjini Dubai, Falme ya nchi za Kiarabu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru na kushoto ni Balozi wa Tanzania Katika Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Mohamed Mtonga.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussaini (wa pili kulia), Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha mjini Dubai-UAE, kabla ya kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, Mjini Dubai, Falme ya nchi za Kiarabu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) akiagana na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussaini (wa pili kulia), Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha mjini Dubai-UAE, baada ya kusaini Mkataba wa makubaliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, Mjini Dubai, Falme ya nchi za Kiarabu.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru na Konseli Mkuu wa Konseli ya Tanzania-Dubai (Balozi Mdogo), Bw. Idi Bakari, wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) akipokea taarifa ya utendaji kutoka kwa Balozi wa Tanzania katika Nchi za falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga, katika Jengo la Ubalozi Mdogo wa Tanzania mjini Dubai. Dkt. Nchemba yuko katika ziara ya kikazi Uarabuni ambapo pamoja na mambo mengine amesaini Mkataba wa Makubaliano ya Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, Mjini Dubai, Falme ya nchi za Kiarabu.

Dubai, UAE - Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu zimetia saini mkataba wa makubaliano ya kuondoa utozaji Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi ya Mapato kati ya nchi hizo mbili, yaani 'Agreement on Avoidance of Double Taxation and Prevention of Fiscal Evasion on Income Taxes'.

Mkataba huo umetiwa saini katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Dubai na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mhe. Mohamed Bin Hadi Al Hussain, Waziri wa Nchi wa Mambo ya Fedha wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa kusainiwa kwa Mkataba huo ni jitihada za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizozifanya Mwezi Februari, 2022 katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo aliagiza kuondolewa kwa changamoto hiyo ili kukuza mahusiano ya kiuchumi, kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kodi na kuchochea mazingira wezeshi ya uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

TANZANIA PORTS AUTHORITY, ANTWERP MULL PARTNERSHIP


The Tanzania Ports Authority (TPA) is mulling a partnership with Belgium’s Antwerp Port, which is expected to further improve operations of Tanzania’s ports.

This envisaged partnership, will also enable Tanzania’s principal port of Dar es Salaam adopt best international practices.

Antwerp is Europe’s second-largest port. It is a major lifeline for the Belgian economy: more than 300-line services to over 800 destinations ensure global connectivity.

The Port of Antwerp annually handles around 231 million tonnes of international maritime freight, and is home to Europe’s largest integrated chemical cluster.

Delegation of the port, including its Managing Director Kristof Waterschoot with a company of Belgium Ambassador to Tanzania, Mr Peter Van Acker, is in the country for a familiarization tour at the TPA.

The delegates were yesterday taken through TPA’s functions and its ports, with the main focus on the Dar es Salaam Port.

LENDING HITS RECORD HIGH AS FINANCIAL SECTOR LEAPS


Banks’ lending to the private sector are in record high to provide massive boost to businesses thanks to Central Bank’s accommodative monetary policy implemented in 2020/21 to promote economic activities.

The Central Bank Governor, Prof Florens Luoga said in a Monetary Policy Committee (MPC) meeting statement over the weekend that private sector credit growth improved significantly in July and August, reaching around 20 per cent, compared with the projection of 10.7 per cent for 2022/23.

The Central Bank’s latest monthly economic review said credit to the private sector increased at an annual rate of 22.6 per cent for the year ending July compared with 8.9 per cent in the same period last year.

The report attributes the phenomenal growth to improved business environment in the country, recovery of private sector activities from the effects of COVID-19, and supportive fiscal and monetary policy conditions.

The Central Bank implemented an accommodative monetary policy in 2021/22 to facilitate recovery of economic activities from adverse effects of COVID-19 pandemic.

Among other things implementation of the policy was aimed at boosting growth of credit to the private sector of 10.6 per cent and maintaining sufficient foreign exchange reserves to cover at least four months of projected imports

BANK OF TANZANIA MONETARY POLICY COMMITTEE MEETING

Monday 26 September 2022

BENKI YA CRDB YATEKELEZA KWA VITENDO AHADI YA RAIS SAMIA YA KUFUNGUA UCHUMI


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Proparco, Françoise Lombard, wakati alipotembelea Makao Makuu ya AFD jijini Paris, Ufaransa. Ujumbe wa Benki ya CRDB ulikutana na Kampuni ya Proparco kujadili maeneo ya kimkakati ya ushirikiano na fursa za uwekezaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Kilimo na Teknolojia ya Chakula wa Taasisi ya Business France, Laure Elsaesser wakati wa ziara yake nchini Ufaransa. Ujumbe wa Benki ya CRDB upo nchini Ufaransa kukutana na wadau mbalimbali ili kuendeleza uhusiano na kujadili fursa za uwekezaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa SH Biaugeaud, Emmanuel Vallantin Dulac, wakati wa mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo Tanzania. Ujumbe wa Benki ya CRDB upo nchini Ufaransa kukutana na wadau mbalimbali ili kuendeleza mahusiano na kujadili fursa za uwekezaji nchini.

Ujumbe wa Benki ya CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Societe Generale Group wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa Kibenki Afrika, Cathia Lawson (wa tatu kushoto). Ujumbe wa Benki ya CRDB upo nchini Ufaransa kukutana na wadau mbalimbali ili kuendeleza mahusiano na kujadili fursa za uwekezaji nchini.

Katika ziara yake ya kwanza ya kikazi nchini Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa ahadi alipokuwa akizungumza kwenye mkutano maalumu na viongozi wa sekta binafsi.

“Tunakwenda kufungua nchi, Kenya kuna Uhuru ikimaanisha uhuru wa kufanya biashara; Tanzania kuna Suluhu maana yake ni suluhu za vikwazo vya kibiashara, mpira sasa uko kwenye himaya yenu,” Rais Samia alisema huku akipigiwa makofi na jumuiya za wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania.

Ili sekta binafsi iweze kufanya kazi na kuleta ukuaji wa uchumi, sekta ya fedha ni moja ya njia muhimu ya kufikia huko. Miongoni mwa vikwazo vingi vinavyoikabili sekta binafsi katika nchi kama Tanzania ni mahali pa kupata mikopo nafuu ili kuwekeza kama mtaji.

"Mitaji ni moja ya changamoto kubwa inayozuia ukuaji wa biashara na hivyo kuathiri uwezo wetu wa kuzalisha na kuuza kwa ushindani katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile Kenya," alisema Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Angelina Ngalula.

Sekta ya fedha nchini imeitikia vyema mageuzi ya biashara na kiuchumi ya Rais Samia. “Sisi kama sekta ya fedha tuna wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza uchumi kwa kutoa fedha kwa sekta ya umma na binafsi," anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa kukutana na washirika wake na wawekezaji ikiwamo Shirika la Fedha la Proparco.

Nsekela ambaye anaongoza ujumbe wa benki hiyo, ameahidi kuimarisha utoaji wa mikopo kwa kuongeza kiasi cha fedha za mikopo kupitia uanzishwaji wa ushirikiano na taasisi za fedha za kimataifa kama vile Proparco na nyingine.

Benki ya CRDB ambayo kwa mara ya kwanza ilitia saini ya makubaliano ya ushirikiano na Proparco, kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ufaransa (AFD) linalojihusisha na ukopeshaji wa kibiashara, inataka kupanua wigo wa ushirikiano na taasisi hiyo yenye makao yake makuu jijini Paris.

NCBA YAENDELEA KUINUA MAISHA, YATOA ZAWADI ZA PIKIPIKI

Meneja Masoko kutoka Benki ya NCBA, Solomon Kawiche (wa kwanza kushoto), akiwazawadia pikipiki washindi wa awamu ya pili wa kampeni ya Mpawa iliyopewa jina la “Chuzi Limekubali” kwa kushirikiana na Vodacom kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala. Wa pili kushoto ni Fulgence Otaru, mshindi kutoka Dar es Salaam; wa tatu kushoto ni Maria Mabella, Afisa Huduma kwa wateja kutoka Benki ya NCBA; na kulia kabisa ni Richard Mkoba, mshindi kutoka Mkoani Pwani.
Afisa Huduma kwa Wateja kutoka Benki ya NCBA, Maria Mabella (wa kwanza kulia) akimkabidhi pikipiki Richard Mkoba (katikati) kutoka Pwani, mmoja wa washindi wa awamu ya pili wa kampeni ya Mpawa iliyopewa jina la "Chuzi Limekubali" kwa kushirikiana na Vodacom. Upande wa kwanza kushoto ni Fulgence Otaru, mshindi mwingine wa kampeni kutoka Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Zakhem huko Mbagala Septemba 23, 2022.

Dar es Salaam, Septemba 23, 2022 - Benki ya NCBA imewazawadia pikipiki washindi watatu wa kampeni ya Mpawa ijulikanayo kwa jina la Chuzi Limekubali kwa mara ya pili mfululizo katika tukio lililotokea katika viwanja vya Zakhem Mbagala. Kampeni hiyo ilianza Agosti mwaka huu.

Kampeni hiyo inafanyika kwa ushirikiano na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, ambayo inawahimiza wateja kuweka akiba, kukopa na kurejesha mikopo ili kujishindia zawadi kila siku na kila wiki.

Washindi wa raundi ya kwanza droo ya Mpawa "Chuzi Limekubali" wakiwa na zawadi zao za pikipiki.

Fulgence Otaru, mfanyabiashara kutoka Dar es Salaam, alielezea furaha yake baada ya kushinda pikipiki. "Ilikuwa vigumu kwangu kuamini mwanzoni, lakini baada ya simu kadhaa kutoka kwa kitengo chao cha huduma kwa wateja, mashaka yangu yaliondolewa. Nataka kuhimiza kila mtu aanze kuweka akiba na Mpawa mara moja kwa sababu mikopo ni ya haraka na rahisi.' Alisema.

MITANANGE YA UEFA NATIONS LEAGUE NDANI TA DStv

 

WAZIRI MKUU ATAMBUA MCHANGO WA MAREHEMU BALOZI PAUL RUPIA NA UTUMISHI ULIOTUKUKA SIKU ZA UHAI WAKE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam kabla ya maziko yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini humo. Balozi Rupia alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Benki ya DCB na kuiongoza kwa kipindi cha miaka 15 na alifariki Dunia Septemba 16 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (kushoto), akitoa salamu za pole kwa niaba ya Bodi na Menejimenti ya DCB katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, kabla ya maziko yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini humo. Balozi Rupia alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Benki ya DCB na kuingoza kwa kipindi cha miaka 15. Alifariki Dunia Septemba 16 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango mkubwa alioutoa Mwenyekiti wa kwanza wa Benki ya DCB, Marehemu Balozi Paul Rupia katika kufanikisha uanzishwaji na maendeleo ya benki hiyo na utumishi wake uliotukuka katika maeneo mbalimbali wakati wa uhai wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), akizungumza katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam kabla ya mazishi yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Zawadia Nanyaro.

Waziri Mkuu aliyasema hayo katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na baadae kufuatiwa na maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini humo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa, na Mwenyekiti wa Bodi Mstaafu wa DCB, Prof. Msambichaka wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam kabla ya maziko yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini humo. 

Waziri Mkuu alisema moja ya jambo ambalo halitasahaulika kwa Marehemu Balozi Paul Rupia ni mchango wake mkubwa kwa benki hiyo kwani hadi anaondoka katika Uongozi aliiacha benki hiyo ikiwa na matawi nane.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya Biashara ya DCB, Regina Mduma (kulia) na Ofisa Masoko, Agnes Ntabaye (kushoto) wakiweka shada la maua kwenye kaburi alimozikwa Marehemu Balozi Paul Rupia wakati wa maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Balozi Rupia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Benki ya DCB na kuingoza kwa kipindi cha miaka 15.

“Mheshimiwa Rais Samia amenituma kuja kumuwakilisha katika msiba huu, amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo za Balozi Rupia, hakuweza kuhudhuria kwa sababu yupo nchini Msumbiji kwa ziara ya kikazi, pia ametoa pole kwa familia na waombolezaji wote”, alisema Waziri Mkuu.