Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 29 August 2023

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI SKULI YA MIL. 600 INAYOJENGWA NA NMB



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, iliyopo Shehia ya Tasani, Makunduchi, inayojengwa na Benki ya NMB, ikitarajia kugharimu Sh. Milioni 600 hadi itakapokamilika Disemba 2023.



Mradi huo umezinduliwa ikiwa sehemu ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023), linaloendelea Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, visiwani Zanzibar.



Tamasha hilo lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Agosti 26 mwaka huu, linafanyika chini ya kauli mbiu 'Tuwalinde Kimaadili Watoto Wetu kwa Maslahi ya Taifa,' na linatumika kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.



Akitoa maelezo ya awali ya mradi huo wa Tasani kwa Rais Samia, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, amesema ujenzi huo ambao ni sehemu ya Programu ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI), ni kati ya jitihada za wazi za benki yake katika kumuunga mkono kufanikisha maendeleo ya elimu nchini.



Bi. Zaipuna alimueleza Dkt. Samia kwamba ujenzi huo utakaojumuisha madarasa matano yatakayochukua wanafunzi 200 kwa mkupuo mmoja, utakamilika Disemba mwaka huu, tayari kabisa kwa Mwaka wa Masomo wa 2024, ambao utaanza Januari mwakani, na kwamba Skuli ya Maandalizi Tasani itakuwa ni shule ya kwanza katika eneo hilo, ikiwa ni ya tatu kwa Makunduchi.



"Ujenzi wa majengo na samani za ndani kama vile viti, meza na madawati, utaigharimu Benki ya NMB Shilingi Milioni 600, ambazo ni sehemu ya faida yetu tunayoitoa kila mwaka kurejesha kwa jamii.



"Mradi huu ulio kwenye eneo la mita za mraba 467, utajumuisha madarasa matano yatakayobeba wanafunzi 40 kila moja, Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Ofisi ya Walimu, jiko, vyoo vya walimu, wafanyakazi na wanafunzi, stoo, Mifumo ya Kisasa ya Maji Safi na Majitaka, pamoja na sehemu ya michezo.



"Mheshimiwa Rais, mradi wa Skuli hii ni uthibitisho wa utayari wa NMB kusapoti Serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kuboresha Elimu nchini.

PRESIDENT MWINYI COMMENDS ABSA FOR MEDICAL SUPPLIES

The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Honorable Dr. Hussein Ali Mwinyi (center), participates in a walk and short run during the Amref Wogging Marathon 2023 in Zanzibar over the weekend, sponsored by Absa Bank Tanzania. Also present, from left, are the First Lady, Mrs. Mariam Mwinyi, Absa Bank Tanzania Managing Director, Obedi Laiser, the Deputy Minister of Health of Zanzibar, Hon. Hassan Khamis Hafidh, and the Country Director of Amref, Dr. Florence Temu. The event aimed to raise funds to support the availability of medical equipment for safe delivery and maternal and child health.
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Honorable Dr. Hussein Ali Mwinyi (second left), is briefed about Absa Bank's banking services from the Absa Bank Manager of Special Client Relations, Salim Khamis Salum, upon arrival at Maisara grounds after participating in the Amref Jogging Marathon 2023 sponsored by Absa Bank in Zanzibar during the week. On his left is the CEO of Absa Bank, Obedi Laiser. 
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Hon. Dr. Hussein Ali Mwinyi (fourth from the left), presents a certificate of appreciation to the CEO of Absa Bank Tanzania, Obedi Laiser, in recognition of the bank's major sponsorship of the Amref wogging Marathon held in Zanzibar over the weeked.

Zanzibar - The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Honorable Dr. Hussein Ali Mwinyi, has commended Absa Bank Tanzania for sponsoring a walkathon and short race aimed at contributing medical supplies for safe maternal and child health.

Speaking after the event named 'Wogging Marathon 2023', organized by Amref in collaboration with the Government of Zanzibar under the sponsorship of Absa, President Dr. Mwinyi expressed his recognition and appreciation for the significant support provided by Absa Bank and the organizers of the marathon.

"On behalf of the government, I extend gratitude to Absa Bank Tanzania and urge them to continue collaborating with us to ensure the success of our goals in reducing maternal and child deaths related to childbirth," said President Dr. Mwinyi.

"I am pleased to hear that this campaign spans three years and started last year, with the aim of raising one billion Tanzanian Shillings. The information I have indicates that total commitments of 792 million Shillings have been made so far, with 557 million Shillings already collected," the President added.

EXIM BANK LAUNCHES WOMEN'S EMPOWERMENT PROGRAM

The Minister for Community Development, Gender, Women and Special Groups Dorothy Gwajima (second right) presses a button to officiate the launch of Exim Bank’s Women Empowerment Program (WEP) that seeks to promote inclusive economic development in countries where the bank operates including Tanzania. Looking on at the center is the Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer, Jaffari Matundu.
The Minister for Community Development, Gender, Women and Special Groups Dorothy Gwajima (second right) in a jovial mood after launching Exim Bank’s Women Empowerment Program (WEP) that seeks to promote inclusive economic development in countries where the bank operates including Tanzania. Looking on at the center is the Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Jaffari Matundu.

Exim Bank Group through its Corporate Social Responsibility (CSR) program dubbed “Exim Cares” has launched a Women Empowerment Program (WEP) that seeks to promote inclusive economic development in countries where the bank operates including Tanzania, Comoros, Djibouti, and Uganda.

During the launch, the first cohort of 20 aspiring women entrepreneurs graduated and received certificates and cash prizes for the top performers.

The bank’s program takes the shape of an ‘accelerator or incubator’ in which selected women-based startup companies and/or individual entrepreneurs will be helped to develop their businesses through a range of services including training, startup capital and financial facilities to kick start or scale up their businesses.

For Tanzania, the bank’s program aligns with the Tanzania Development Vision 2025 and the Zanzibar Development Vision 2050 and will be a catalyst in enhancing women’s socio-economic welfare.

Speaking during the launch of the WEP program in Dar es Salaam yesterday, the Exim Bank Chief Executive Officer Jaffari Matundu said his bank is committed to increase the integration of sustainability into its business models and approaches to deliver economic, social, and environmental benefits for all its stakeholders.

Monday 28 August 2023

BENKI YA NBC YASHIRIKI WOGGING YA AMREF ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani na utambuzi kwa Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC, Linley Kapya (wa pili kulia) kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoambatana na mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 kufanikisha kampeni hiyo. Wengine ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh (kushoto), Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa tayari kuongoza washiriki wa mbio fupi zilizo ambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar. Pamoja nae pia wapo Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh (kushoto kwa Rais Mwinyi), Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais Mwinyi) na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (kushoto kwa Naibu Hafidh).
Matembezi hayo yalianzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar.
Maofisa wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali wa benki hiyo, Linley Kapya (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (wa pili kushoto) mara baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani na utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoambatana na mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 kufanikisha kampeni hiyo.

Zanzibar; Agosti 28, 2023 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wadau wengine kushiriki kwenye mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar.

Kupitia tukio hilo ambalo ni sehemu ya kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs Milioni 200 vitakavyotumika kwenye hospitali mbalimbali za Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya visiwani humo.

Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi hayo yaliyoanzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar mwishoni mwa wiki, Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC Linley Kapya alisema mbali na mazoezi ya viungo, ushiriki wa benki hiyo ulilenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza na kuepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ambapo bado kiwango cha changamoto hiyo kipo juu.

"Kama ambavyo amebainisha Rais Dk. Mwinyi kwamba takwimu zinaonesha kuna vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017. Hali hiyo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu na tatizo la kukosekana kwa dawa.’’

RAIS MWINYI AZINDUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akitazama jiwe la msingi mara baada kuzindua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho uliofanywa na Rais Mwinyi mwishoni mwa wiki ikiwa pia ni sehemu ya uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi 2023. Wengine ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Hafidh (wa kwanza kushoto), Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (wa pili kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kulia) akimsikiliza Mhandisi wa mradi Mhandisi Fatma Kara (alieshika kipaza sauti) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho uliofanywa na Rais Mwinyi mwishoni mwa wiki ikiwa ikiwa pia ni sehemu ya uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi 2023. Wengine ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Hafidh (wa nne kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (katikati).
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Sehemu ya wakazi wa Kizimkazi wakifuatilia uzinduzi huo.
Meneja wa Biashara wa NBC,  Obeid Ngavatula akimuelezea huduma zinazotolewa na Benki ya NBC, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipotembelea banda la benki ya NBC kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi 2023 uliofanyika mwishoni mwa wiki Paje, Mkoa wa Kusini, Unguja.
Karibu tukuhudumie.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa tamasha la Kizimkazi 2023 ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara NBC wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kizimkazi 2023 uliofanyika mwishoni mwa wiki Paje, Mkoa wa Kusini, Unguja.

Zanzibar, 28 Agosti 2023 - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amezindua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni jitihada za wadau hao wawili katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika mwishoni mwa wiki ikihusisha uwekaji wa jiwe la msingi eneo unapotekelezwa mradi huo ikiwa pia ni sehemu ya uzinduzi wa Tamasha la Kizimkazi 2023 hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka serikalini akiwemo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Hafidh, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi, viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Akizungumzia mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 4.4 ambapo benki ya NBC imechangia kiasi cha Sh milioni 400, Rais Mwinyi pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa hatua hiyo muhimu, alisema huo ni adhma ya serikali hiyo kuboresha huduma ya afya kwa kujenga vituo vya afya vyenye hadhi ya kipekee katika baadhi ya maeneo kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo katika maeneo hayo huku akiyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na eneo la Tumbatu, Fuoni na Kizimkazi.

STANBIC YAHITIMISHA PROGRAM MAENDELEO YA WASAMBAZAJI

Mkurugenzi wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara, Benki ya Stanbic - Fred Max.
  • Wahitimu 100 WA program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development program' waaswa kutumia Mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao
Wahitimu 100 wa program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' iliyotolewa na Benki ya Stanbic kwa Kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), (Biashara Incubation), wamehitimu program hiyo Agosti 26, 2023, Katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) jijini Dar es Salaam.


Wahitimu hao walipata program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development' kwa miezi tisa huku yakiwa yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Miezi sita ya kupewa masomo na miezi mitatu ya kufanya kazi katika maeneo ya miradi ikiwa na wanawake 52 na wanaume 48.


Incubator ya Biashara ya Stanbic sio programu tu ni harakati ambayo inasimamia ukuaji wa biashara ndogo na za kati, kukuza uwezo wao, na kukuza mfumo mzuri wa kijasiriamali unaonufaisha taifa kwa ujumla.


Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu amewaasa Wahitimu kutumia vizuri Mitandao ya kijamii kwaajili kutangaza biashara zao ili kujipatia kipato.


"Hata uwe na simu nzuri na ya gharama kiasi gani, kama haiingizi kipato ni kazi bure, simu itengeneze kipato...." Amesema Zungu


Pia amewapongeza benki ya Stanbic kupitia program ya Maendeleo ya Wasambazaji 'Supplier development
na baraza la NEEC kwa kutoa mafunzo kwa wahitimu hao kwani changamoto kubwa iliyopo ni jamii kukosa taarifa sahihi za uwekezaji.

TADB, SELF MF KUTOA BIL. 6 KWA WAKULIMA WADOGO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), David Nghambi (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa SELF MF, Mudith Cheyo (wa tatu kushoto), wakitia saini mkataba wa dhamana kwa wakulima wadogo wa taasisi hizo mbili wenye thamani ya shilingi bilioni 6. Mwanasheria wa Benki ya TADB, Emily Lukiko (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Sheria SELF MF, Angela Lushagara na Frank Lawi, Mwakilishi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu (Nyuma) wakishuhudia utiaji saini uliofanyika Jumatatu Agosti 28, 2023, katika ofisi za makao makuu ya TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), David Nghambi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa SELF MF, Mudith Cheyo (kushoto), wakikabidhiana mikataba ya dhamana kwa wakulima wadogo wenye thamani ya shilingi bilioni 6, itakayosaidia wakulima nchini kupata mikopo kwa riba nafuu. Mikataba hiyo imetiwa saini Jumatatu Agosti 28, 2023 katika ofisi za makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), David Nghambi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa SELF MF, Mudith Cheyo (kushoto), wakipeana mikono kama ishara ya makubaliano katika halfa ya utiaji saini mkataba wa dhamana kwa wakulima wadogo wenye thamani ya shilingi bilioni 6, ulioingiwa baina ya taasis hizo. Hafla hiyo imefanyika Jumatatu, Agost 28, 2023 katika ofisi za makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), David Nghambi (kulia) akijibu swali kutoka kwa waandishi wa Habari, katika hafla ya utiaji saini mkataba wa dhamana kwa wakulima wadogo wenye thamani ya shilingi bilioni 6, baina ya TADB na mfuko wa SELF MF. Pembeni ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa SELF MF Mudith Cheyo. Hafla hiyo imefanyika Jumatatu Agost 28, 2023 katika ofisi za makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), David Nghambi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa SELF MF, Mudith Cheyo wakionyesha mikataba ya dhamana kwa wakulima wadogo wenye thamani ya shilingi bilioni 6 waliyotia saini, itakayosaidia wakulima kupata mikopo kwa urahisi. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika ofisi za makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam, Agosti 28, 2023.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wake wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) imeingia mkataba wa Tshs. Bilioni 6 na SELF Microfinance Fund (SELF MF) kwaajili ya kutoa dhamana ya mikopo ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Mkataba ulioingiwa kati ya pande hizi mbili ni utawezesha TADB kuchagiza upatikanaji wa mitaji kwa wakulima kupitia SELF MF. SELF MF watatoa mikopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na uvuvi na TADB itatoa dhamana ya hadi asilimia 50 kwa mikopo yote. Wachakataji wa mazao wadogo na wakati (SMEs), wakulima wadogo wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi watanufaika kupitia ushirikiano huu kupitia ofisi zote za SELF MF kote nchini.

Akiongea katika hafla fupi ya kutia sahihi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB David Nghambi alisema kupitia mkataba huu, utaiwezesha SELF MF kuongeza wigo wa utoaji mikopo katika sekta ya kilimo hasa wanawake na vijana.

“Mfuko wa SCGS unaosimamiwa na TADB, unasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo. Kupitia ushirikiano wa TADB na taasisi nyingine za kifedha kama SELF MF. Dhamana tunayoitoa inasaidia taasisi hizi za kifedha kuvutiwa na utoaji wa mikopo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi. Pia kupitia mitandao ya taasisi hizi za kifedha wakulima wengi hasa walioko vijijini wanafikiwa.

JUMANNE HII NI CARABAO CUP KIFURUSHI CHA POA

VODACOM FOUNDATION YADHAMINI MBIO ZA MBUZI


Dar es Salaam – Agosti 28, 2023: Katika kuunga mkono jitihada za upatikanaji wa fursa za kielimu nchini, Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, sehemu ya kampuni ya Vodacom Tanzania PLC iliyojikita katika shughuli za kijamii na kimaendeleo, imeingia ushirikiano na Rotary Club ya Oysterbay ambao ni waandaaji wa mbio za mbuzi (Goat Races) kama wadhamini wakuu ambazo zitafanyika Septemba 9 katika viwanja vya the Green Oysterbay kuanzia saa 6 mchana mpaka saa mbili usiku jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa kutangaza ushirikiano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriett Lwakatare amesema kuwa taasisi hii imejikita kwenye kutumia ubunifu kiteknolojia na mawasiliano kwa kushirikiana na taasisi za umma na sekta binafsi kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa maendeleo nchini kote.


“Tangu kuanzishwa kwetu mwaka 2006 tumekuwa tukishirikiana kwa ukaribu na taasisi za umma na sekta binafsi, mashirika ya ndani na kimataifa kuungana mkono utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya serikali sehemu tofauti nchini. Miongoni mwa maeneo ambayo tumejikita zaidi ni sekta ya afya, elimu, mazingira, na uchumi jumuishi. Kwa upande wa elimu tunashirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na taasisi zake kama vile COSTECH, TEA, na Tanzania Data Lab kwenye miradi tofauti kama vile e-Fahamu au uungwanishwaji wa shule kwa kushirikiana na UCSAF pamoja na taasisi ya African Child Projects ambapo tunalenga kuzifikia shule 300 nchini kote,” alisema Bi. Lwakatare.

Saturday 26 August 2023

CMSA YAIDHINISHA CRDB KUTOA HATIFUNGANI YA KIJANI


Dar es Salaam, 24 Agosti 2023: Katika juhudi za kuongeza uwezo wake wa kufanya uwezeshaji wa miradi rafiki kwa mazingira, Benki ya CRDB imepata idhini kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuuza Hatifungani ya Kijani (Green Bond) yenye thamani ya dola 300 milioni za Marekani (takriban Shilingi bilioni 780). Benki ya CRDB inaweka historia ya kuwa taasisi ya kwanza kutoa hatifungani ya kijani hapa nchini inayoweka mkazo katika masuala ya mazingira na kubwa zaidi kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza wakati wa kupokea idhini ya kuuzwa kwa hatifungani hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ni furaha kubwa kupata idhini kutoka CMSA kuiuza hatifungani hiyo ambayo lengo lake si tu kupata rasilimali fedha bali kufanikisha utekelezaji wa miradi yenye mrengo wa kuhifadhi mazingira hivyo kushiriki ipasavyo katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.


“Pamoja na kuwa Benki ya CRDB inaweka rekodi ya kuwa taasisi kubwa zaidi ya fedha nchini kupata idhini ya kuuza hatifungani ya kijani, lakini Benki yetu sio ngeni katika uwezeshaji wa miradi yenye mrengo wa utunzaji mazingira kwani Novemba 2019 ilitambuliwa na kuingia makubaliano na Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (GCF) kufanikisha miradi ya kulinda mazingira. Hii pia ilikuwa ni mara ya kwanza benki ya biashara kusini mwa Jangwa la Sahara kutunukiwa sifa hiyo na tangu hapo, tumeshiriki kwa kiasi kikubwa kuwezesha miradi inayokusudia kulinda mazingira,” amesema Nsekela.

Kuhusu uwezeshaji wa miradi ya mazingira, Nsekela amesema kwa mwaka jana pekee, Benki ya CRDB ilikopesha jumla ya shilingi trilioni 6.978 ambazo ni sawa na asilimia 26 ya mikopo yote iliyotolewa na taasisi za fedha nchini. Katika fedha hizo, amesema shilingi bilioni 1.44 zilikopeshwa katika sekta ya misitu, kiasi hicho ni sawa na asilimia 55 ya mikopo yote iliyotolewa kwenye sekta ya misitu.


Kwenye kilimo, sekta muhimu kwenye uhifadhi wa mazingira na inayotoa ajira nyingi zaidi nchini na kulipa Taifa fedha nyingi za kigeni, amesema benki hiyo ilikopesha takriban shilingi trilioni moja ambazo ni sawa na asilimia 43 ya mikopo yote iliyotolewa kwenye eneo hilo na ikapeleka shilingi bilioni 55.88 kwenye sekta ya nishati mbadala.

Licha ya jitihada hizo, mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya fedha kuliko uwezo walionao hivyo kutafuta namna rafiki ya kufanikisha suala hilo.

“Kwa kutambua mahitaji yaliyopo, Benki ya CRDB imeona ni muhimu kutafuta vyanzo vipya vya fedha kuwezesha miradi hii. Leo nina furaha kuona jitihada zetu zimezaa matunda kwa CMSA kutupa idhini ya kuuza hatifungani yetu ya kijani (green bond) ambayo itauzwa kwa awamu tano ambapo katika awamu hii ya kwanza tunatarajia kupata shilingi bilioni 55,” amesema Nsekela.


Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama ameipongeza Benki ya CRDB kwa kufanikiwa kuwa Benki ya kwanza nchini kupata idhini ya kutoa hatifungani itakayowezesha kupata fedha za kutekeleza miradi ya kuhifadhi mazingira na matokeo chanya kwa jamii yaani green, social and sustainability bond.

Friday 25 August 2023

VITA YA MASHEKHE NA WAMAREKANI NDANI YA DStv


Kivumbi cha EPL wikiendi hii ni Liverpool wanaovaana na Newcastle, je ni timu ipi kuchukua point 3?

@dstvtanzania wanakusogezea mtananage huu Live Sebuleni kwako. Hakikisha unalipia mapema kifurushi chako kwa kupiga *150*53# ili usikose burudani hii.

Na Kama hujajiunga na DStv, Piga Sasa 0659 07 07 07 kujiunga Sasa na ofa ya TShs. 59,000/= tu.

#SokaPromax
#Unakosaje

MASTERCARD AND ZANZIBAR e-GOVERNMENT AGENCY COLLABORATE

 (L-R): Elsie Wachira – Kaguru, Director, Account Management, East Africa at Mastercard; Shehryar Ali, Country Manager for East Africa at Mastercard; Said Seif Said, Managing Director, Zanzibar e-Government Agency (eGAZ); and Namulisa Kombo, Director, Government Engagement, East Africa at Mastercard during the signing of the Memorandum of Understanding (MoU) that will see Mastercard provide technical assistance and expertise to support the Zanzibar Government’s digital transformation efforts.
  • The collaboration is the first MoU with eGAZ to support the implementation of their Digital Government Strategy 2023-2027
  • MoU to further support the government’s efforts in bringing more people into Zanzibar’s digital economy
Zanzibar, 22 August 2023: Mastercard has collaborated with the Zanzibar e-Government Agency (eGAZ) to support and accelerate its ambitious digital transformation journey. This will allow different sectors across the Zanzibar islands, including tourism, to digitize payments which will significantly contribute to robust economic growth.

The signing of the Memorandum of Understanding (MoU) took place at the launch of the Zanzibar Digital Government Strategy for 2023-2027, led by H.E Hussein Ali Mwinyi, President of the Revolutionary Government of Zanzibar.

The agreement is the first MoU signing by Mastercard aligned with Zanzibar’s digital transformation goals laid out in their Digital Economy Blueprint and Roadmap. The strategy's main objective is Zanzibar’s transformation into a strong digital economy which will secure digital systems, drive innovative information, communication and technology solutions and develop training for digital governance, ultimately reshaping public services.

Under the three-year collaboration, Mastercard will provide technical assistance and expertise to support the Zanzibar government's efforts. This includes setting up a digital transformation team, collaborating with the government's payment portal ZanMalipo to enable digital payments, and launch two million government cards for better access to services and tourism.

"The like-minded collaboration between Mastercard and the Zanzibar e-Government Agency will help power an inclusive, digital economy that benefits everyone, everywhere in Zanzibar. It is a testament to the profound impact of digitization and builds on Mastercard's global experience in enabling digital transformation and demonstrating the value of fostering cross-sector collaboration, fuelling economic growth and facilitating financial and digital inclusion,” said Shehryar Ali, Country Manager, East Africa, Mastercard.

Thursday 24 August 2023

NBC, TAIFA GAS KUTOA MIKOPO MFUMO WA GESI KWA TAASISI

Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (kushoto) na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (kulia) wakijipongeza huku wakionesha hati ya makubaliano baina ya taasisi hizo mbili yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini. Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (wa pili kushoto) na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (wa pili kulia) wakisaini hati ya makubaliano baina ya taasisi hizo mbili yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini. Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mahusiano ya kiutendaji kati ya benki hiyo Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (kulia) na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw. Raymond Urassa (kushoto).
Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas, Devis Deogratius (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mahusiano ya kiutendaji kati ya kampuni hiyo benki na benki ya NBC yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC, Bw. Elibariki Masuke (wa pili kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw. Raymond Urassa (kushoto).
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha maofisa waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo kwa upande wa NBC waliongozwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki hiyo, Elibariki Masuke (wa nne kushoto) huku upande wa Taifa Gas ukiongozwa na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Devis Deogratius (wa tatu kulia).
Dar es Salaam; Agosti 24, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Kampuni ya usambazaji gesi za majumbani, Taifa Gas wameingia makubaliano ya kiutendaji yanayotoa fursa kwa benki hiyo kutoa mikopo ya mifumo ya gesi ya kupikia kwa taasisi mbalimbali zikiwemo shule, hospitali, magereza, viwanda, vyuo na watoa huduma za vyakula.

Pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia miongoni mwa watanzania, hatua hiyo pia inatajwa kuwa itasaidia kupunguza gharama kubwa zinaelekezwa kwenye matumizi ya nishati miongoni mwa taasisi hizo.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam ikihusisha maofisa waandamizi kutoka pande zote mbili ambapo kwa upande wa NBC waliongozwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki hiyo Elibariki Masuke huku upande wa Taifa Gas ukiongozwa na Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo Devis Deogratius.

Kwa mujibu wa Bw. Masuke hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu zinazolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani kwa kuanza na taasisi zinazohudumia watu wengi.