Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 20 July 2021

BAA ZAENDELEA KUCHANGAMKIA FURSA YA SBL ‘RAISE THE BAR’ AU 'TUNYANYUKE PAMOJA’

Faith Mpawa, mmoja kati ya wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti akimwelekeza mmoja wa wafanyakazi wa Baa ya Meridian iliyopo Vijana Kinondoni namna ya kujisajili katika Mpango wa kuzisaidia Baa kunyanyuka maarufu kama "Raise the Bar" unaofadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.


Mwakilishi wa kampuni ya Bia ya Serengeti alimwelekeza mmoja wa wateja namna ambavyo anaweza kujaza fomu kwa ajili ya kuomba kunufaika na mradi wa kunyanyua baa baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa Corona unaojulikana kama "Raise the Bar".
Hassan Matata akimwelekeza mmoja wa wafanyakazi wa MK bar iliyopo jijini Dar es Salaam namna ya kujaza fomu ya maombi kwa ajili ya kuomba misaada mbali mbali inayotolewa na Kampuni ya SBL kupitia mpango wa kusaidia baa kunyanyuka maarufu kama Raise the Bar.

Mmoja kati ya wateja waliofika katika banda lililowekwa kwa ajili ya kuwaelekeza wenye mabaa namna ya kujisajili katika mpango wa kuyasaidia mabaa kunyanyuka unaojulikana kama "Raise the Bar" au Tunyanyuke Pamoja akipata maelekezo kutoka kwa wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.

No comments:

Post a Comment